The Supreme Conqueror
JF-Expert Member
- Feb 13, 2017
- 458
- 1,280
Wanajukwaa kumekua na Siasa mpya ndani ya Nchi yetu iliyopewa jina "Maridhiano" umekua ngumu kutofautisha vyama vya upinzani na chama tawala kwasababu ya Viongozi wao kuwa machawa wa Rais nazungumza hili kwa uhalisia uliopo sasa. Lakini nina mashaka ndani ya hii Siasa mapya inayoitwa Maridhiano. Je, inamjenga Rais au inabomoa Taasisi ya Urais na Rais mwenyewe Kisiasa kuelekea uchaguzi Mkuu wa 2025?
Hoja zangu ni hizi:
1. Rais amesahau kujishughulisha na hali ngumu ya Maisha kwa Wananchi na kupanda kwa gharama za maisha kwa ujumla.
2. Wale wapinzani wanaomsifia leo ndiyo hao kesho watasimama jukwaani na kupigia kelele hali ya Maisha yalivyo sasa.
3. Kuwakumbatia wapinzani ni sawa na kumkumbatia nyuki kwa maono ya kupata asali kiganjani.
Mimi nahisi Kama CCM wametafuta namna ya kumtoa Samia katika Siasa za ushindani ili iwe rahisi kwao kumuwekea kauzibe ugombea 2025.Mama Sasa anasifiwa anaupiga mwingi lakini wengi wanaomsifia ni Viongozi wa vyama vya Upinzani ambao kiidadi hawafiki hata 10 lakini rest ya Watanzania wenye sifa ya kupiga kura takribani M15-20wanalia na hali ngumu ya Maisha na upandaji wa Bei ya vitu kila uchwao na vilio kwasasa vimeongezeka zaidi na kuvuka mipaka.
Soma, Pia: Ujio wa Rais Samia Suluhu Hassan: Hadi sasa sijaona dalili yoyote ya utashi wa kuwepo kwa maridhiano ya kisiasa nchini
Hadi uko ndani ya chama tawala hali siyo shwari.Wengi wanatamka hadharani hawamuelewi hata kidogo Bora hata JPM kila kitu ndani ya Nchi akishkiki Bei za vyakula,mzunguko wa biashara TRA wamekua kero na Watu wengi kwasasa wanafunga biashara kutokana na mlolongo wa Kodi zisizo na kichwa Wala miguu,kwa kifupi gharama za Maisha hazikamatiki Nchi inaendelea kukopa kwa kasi ya ajabu, umeme umekua kero Kubwa.
RASILIMALI za Nchi zinaliwa na kundi dogo la watu ndani ya Nchi Mama hata ajali yeye Yuko bize na Wapinzani na Sasa hili limekwenda mbali zaidi mbele za kamera za waandishi wanaomsifia Ila nyuma ya kamera wanatoa Siri na udhaifu mkubwa kuwahi kutokea wa serikali yetu tangu Uhuru katika awamu hii.
Ni Nani atanusuru huu mkatiko? Au Mama ameamua liwalo na liwe yeye 2025 hana haja Tena ya kugombea? Ukitizama kwa makini Mama maejichimbia kaburi lake mwenyewe Kisiasa kwani hao wanaomzunguka ndani ya chama ndiyo wanaofanikisha mipango yote ya kuhakikisha kwamba 2025 hagombei tena.
Mama anamalizwa kijasusi na hii slogan ya Maridhiano Bora angebaki njia kuu a deal na mfumuko wa Bei unaoendela Nchini biashara nyingi zinafungwa hali Ni tete Sana. Mwisho namuombea kwa Mwenyezi Mungu amuepushie hiki kikombe, Mungu Ibariki Tanzania.