Haya mazungumzo ndio ya kumkamata Slaa?!! Mbowe kweli anapewa msaada na dola kubaki CHADEMA?!! Mbowe aaminiwe ama amegeuka kua dalali wa watawala?!

Haya mazungumzo ndio ya kumkamata Slaa?!! Mbowe kweli anapewa msaada na dola kubaki CHADEMA?!! Mbowe aaminiwe ama amegeuka kua dalali wa watawala?!

CCM janja janja sana wamechonganisha Kisha wao wako pembeni, wanakula haruwa na kashata. Hizi akili wangekuwa wanatumia Kwa maendeleo ya nchi hii, SGR isingezima kisa umeme kukatika, upungufu wa ajira rasmi ungekuwa chini ya 1%, na sisi tungekuwa tayari tumetuma chombo Kwenye lunar surface.
 
MODERATORS: Tafadhali msiunganishe Uzi huu kwani una umuhimu,unatoa insights kadhaa za miaka mitatu nyuma na yajayo.

Kwa mustakabali mpana wa yanayojiri kwa Slaa,Mbowe,Lissu na CHADEMA kwa sasa,nakuomba ungana nami kwa dakika chache tutafakari na kuamua baada ya kusoma,kutazama na kusikiza mambo haya matano yafuatayo!

1. Sikiliza dakika 5 za Dr Slaa alichokiongea humu kwneye space, tafakari. Tunajua amekamatwa,tunajua amenyimwa dhamana!!
View attachment 3198292

Kwa alichokizungumza humo,alistahili kufuatwa saa 7 usiku kwake mtu ambae amekua Balozi,amekua Katibu Mkuu,Mbunge?!! Kwa nini asingepelekewa wito na akaenda mapambazuko?!! Nani aliekasirika kiasi cha kwenda kumkamata Slaa kama panya road ama jambazi usiku wa manane?!!

2. Tazama clip ya Kisutu mawakili wa Slaa wakieleza sakata na kisa kizima cha Slaa kunyimwa dhamana na mbinu zilizotumika
View attachment 3198300

3. Ikumbukwe Mbowe amekiri kua kabla ya kuachiwa jela alifuatwa na maaskofu wawili na sheikh mmoja ambapo walisema kua wametumwa na Samia kua hawataki kuendelea kumshitaki kwa ugaidi ila akapewa masharti ya kwenda kukutana na muhisani wake huyo,Mbowe alikubali- Je Slaa alichokisema hakiakisi ukweli?!!
Tutazame taarifa rasmi ya siku hiyo baada ya Mbowe kuibukia Ikulu.
View attachment 3198304

4. Ikiwa mdhamini wa Mbowe kumfutia kesi alitoa taarifa kiujumla walikubaliana nini na Mbowe na taarifa bayana inaeleza kua washirkiane,kumbuka baada ya hapo muda mchache Mbowe alilalamikiwa kwenda Kijijini kwao akajenga makazi binafsi ya gjorofa la kifahari huku baadae pia akiomba apewe 150mln cash kwa ajili ya kanisa la Kijijini kwake,ana akapewa na mdhamini yule yule- Slaa anapotosha?!! Mbowe aaminiwe?!!
Haikutosha,baada ya muda mchache Mbowe alimpa na zawadi mtu anaetuhumiwa kua amekua mfadhili wa Mbowe na hatimae Mbowe akiwa Mwanza alisema hadharani kua hawezi kumkosoa Samia,anamuunga mkono Samia na ushahidi huu hapa kwenye clip,Mbowe aaminiwe?!! Mbowe anafanya kazi ya CHADEMA ama ya mdhamini wake?!
View attachment 3198310

5. Kwa kua Dr Slaa ameshikiliwa kwa tuhuma za kusema anapotosha kua Mbowe kapewa fedha za kubaki madarakani, Lissu ambae amejitokeza hadharani na kusema kua Abdul na Mama yake wamepeleka hela za kuhonga watu CHADEMA na yeye alifuatwa kawafukuza- kwa nini Lissu hawamkamati?!! Ama kwa kua kweli Wenje amekiri kua Abdul walienda kwa Lissu ila kuongea fedha za matibabu?!! Je Abdul ni waziri wa fedha ama wa Afya?!! I

Lissu anasemaje kuhusu mwenendo wa Mbowe baada ya kukutana na Samia na kuteta mambo yao?!!
View attachment 3198316

Baada ya kuelekezana kwa viambatanishi kadhaa,ukiwa kama mpenda haki, demokrasia na Mtanzania wa kawaida- Je Mbowe amehongwa?!! Je Mbowe aaminiwe?!! Je Dr Slaa kwa historia yake ya kupinga na kufichua ufisadi kuanzia list ya mafisadi papa mpaka akiwa mbunge, mgombea uraisi,amedanganya umma?!!

Je Watanzania na wajumbe wa mkutano Mkuu CHADEMA- kati ya Lissu na Mbowe- nani anataka kukiua chama?!! Nani apewe kura zote za kukiongoza chama?!!

Tafakuri njema!!
Umepiga pale pale kwenye mshono
 

Attachments

  • IMG-20241214-WA0050.jpg
    IMG-20241214-WA0050.jpg
    9.9 KB · Views: 2
Hapana,wamuhurumie mzee kachoka sana kiafya,
Slaa sijui anatafuta nini?
Alijiondoa mwenyewe Chadema mchana kweupe akakimbilia CCM baada ya kuenguliwa kugombea uraisi.
Aliporejea kwao CCM wakambatiza upya Balozi Sweden.
Na pale walipoamua kumpumzisha kazi hiyo akawasemea mbovu nao wakakata mzizi wa fitina wakampoka title ya kuitwa Ambassador.
Dr Slaa kaja Chadema upya kupitia tresspass!!!
Ugomvi wa wana Chadema kinda kinda tena miamba wa chama chao anauingilia ili iweje? Kwanza Sio mwanachama,kibaya zaidi ni mtoro aliekisaliti chama kikielekea uchaguzi mkuu 2015.
 
Kama Maza anamtuma Abdul kwenda kuzungumza na Lissu na kumhonga, ni mjinga peke yake hataamini kuwa hawezi kumsaidia FAM.
Hapo hapo hembu rejea Mange Kimambi kusema hadharani kua Abdul alimtafuta sana na akafunga safari mpaka California kwenda kumtaka ampe fedha ila aachane na kumsakama Mama Abdul!!
 
Hapo hapo hembu rejea Mange Kimambi kusema hadharani kua Abdul alimtafuta sana na akafunga safari mpaka California kwenda kumtaka ampe fedha ila aachane na kumsakama Mama Abdul!!

Asiyeamini maneno ya Dr Slaa ana matatizo. Yaani Maza atoe pesa za kununua magoli, amwage pesa makanisani halafu asitoe pesa kulinda mamlaka yake.
 
Back
Top Bottom