Haya ndio maboresho ya Mtaala wa Elimu yanayoenda kufanyika Tanzania katika jitihada za kuboresha Elimu

Haya ndio maboresho ya Mtaala wa Elimu yanayoenda kufanyika Tanzania katika jitihada za kuboresha Elimu

Hapa elimu ya sekondari ni ipi? Ni ile kuanzia kidato cha 5 mpaka cha 6 au ni ipi, katika maelezo nikuwa elimu ya msingi itaishia kidato cha nne.Maelezo yanajichanganya, labda litafutwe jina jingine la kidato cha kwanza mpaka cha nne.
 
Kwenye Dini wamekosea sana, Serikali hii haina dini. Na kwa idadi ya madhehebu tuliyonayo sijui nani atatengeneza mtaala wa kufundishia dini.
DINI wangeiacha kabisa kwenye elimu zetu italeta mkanganyiko tu. Maana hii ni kama sisa kila mwenye dini yake anataka kuongeza vichwa na wananchi ni sisi hawa hawa.
Yetu macho tutasubiria maboresho.
Tatizo ni viongozi wapumbavu awawezi kuona jambo kubwa na la wazi kama hilo ....nikosa kubwa sana kuweka mambo ya dini kwenye shule za serikali...hata viongozi wa dini walitakiwa kukataa jambo kama hilo...tatizo hata viongozi wetu wa dini ni vipofu ...mzaha mzaha hijabu zikaingia kwenye shule za serikali ...mzaha mzaha hikabu nazo zitakuja kuingia shuleni na vyuoni ...haya mambo yadini na serikali mara zote viongozi wakuu wa hii nchi wakiwa waislamu ndiyo wanayaletaga kwenye serikali ...majuzi nilisikia waislamu vipofu wanasema kuwa hsta JKT mavazi ya dini yazingatiwe. TANZANIA TUNATAKIWA KUWA NA RAIS ATAKAYE ONDOA HAYO MAMBO NA KUYAPIGA MARUFUKU MASHULENI ....TATIZO LA HAYO MAMBO YA ITIKADI ZA KIDINI KUPENYA MASHULENI LINAPITIA UPENYO WA SOMO LA MAHADILI HILI SOMO LINATAKIWA KUWA SOMO.LA UHADILIFU SIYO MAADILI ...KWAKUWA KILA JAMII NA DINI ZINA MAADILI TOFAUTI TOFAUTI ILA SWALA LA UHADILIFU SIKUZOTE LINAFANANA KWA JAMII ZOTE.
 
Mkuu mitaala itabadilika yote kuanzia msingi mpka Elimu ya juu...
Na kuhusu Kusoma degree miaka Miwili nafikiri kuna masomo watayaweka Form six ambayo yataweza kumuandaa Mtu aweze kuwa na uwezo wa kuemdelea na Bachelor nafikir ndo maana wametaka lazma awe form six
Lakini mkuu, ni vigumu kubadilisha teaching curriculum ya higher learning institution! Vyuo vikuu (duniani) vinatumia mifumo inayofanana ili iwe rahisi kwa wanafunzi kutoka chuo kimoja na kwenda kusoma chuo kingine chochote hapa duniani!

Kwa kubadilisha mfumo, mnajiwekea (mnajifunga) mipaka wenyewe kutoweza kuendana na wenzenu. Mtu akimaliza undergraduate Tanzania, hataweza kwenda kusoma postgraduate mahala pengine, kwakuwa atakuwa hajakidhi vigezo.

Let's say, kigezo cha kusoma Masters ni lower second class ya undergraduate, je, lower second class ya mtu mwenye bachelor ya miaka miwili itakuwa sawa na mwenye bachelor ya miaka mitatu?

Kwa kigezo hicho, hatutawapeleka watu wetu kusoma nje; itabidi wasome hapahapa, maana vyuo vya nje havitaamini kuwa bachelor ya miaka miwili ni sawa na bachelor ya miaka mitatu (hata kama wote watakuwa na first class).

Elimu inatakiwa kuwa na mwingiliano kimataifa, kama ilivyo kwa muingiliano wa mambo mbalimbali. Watu wanaotengeneza vifaa, mfano vipuri vya machine, magari, ndege, nk, wanatengeneza kwa kuangalia/kuhakikisha vipuri hivyo (parts) vifit kwenye vifaa vilivyopo katika mataifa mbambali (interchangeability), na sio kuangalia vifaa vya taifa lenu tu!

Hivyo basi, tunapoingia kwenye mabadiliko haya, tusijiangalie wenyewe tu, bali tuangalie na wenzetu wanafanyeje ili mwisho wa siku tusije tukajikuta tupo peke yetu, na tukiharibikiwa kifaa chetu, hakuna mahali pa kupata spare!
 
Nawaza mfano somo la jiografia mpaka darasa la sita kiswahili,then ghafla inakua kiingereza....

Yaan tungeanza na kiingereza kuanzia darasa la kwanza inge make sense
 
HAYA NDO MABORESHO YA MTAALA WA ELIMU YANAYOENDA KUFANYIKA TANZANIA KATIKA JITIHADA ZA KUBORESHA ELIMU
Habari za mchana WanaJF

Katika kuboresha elimu, Hivi karibuni serikali ilitangaza mabadiliko ya Kisera Na marekebisho ya Mitaala na baadhi ya Sheria ili Elimu iweze kuenda sawa na Sayansi na Technoljia ya Dunia..

Haya hapa chini ni baadhi ya Maboresho yanayoenda kufanyika Katika Elimu ya Msingi, Elimu ya Secondary, Elimu ya Juu ya Sekondary na Ualimu.

SHULE YA MSINGI

Haya ni masomo kwa mujibu wa Rasimu Ya Elimuu..
Elimu ya Ufugaji nyuki ndio nini? Huo ni upuuzi.Bora ingekuwa Elimu ya mazingira,Landscape na Gardening.

Pili Elimu ya Kilimo na Ufugaji inatakiwa ivunjwe vunjwe Ili humo ndani mtoto achague fani za ;

Ufugaji nyuki
Ufugaji wa Kisasa wa mifugo
Kilimo biashara

Najiuliza kwani mtoto akichagua Kilimo atajifunza nini kipya hasa ambacho hakifanyiki kwao Hadi aweze kujiajiri Kwa kutumia gani ya Kilimo na mifugo?

Pili Vyuo vya Veta vitafutwa au vitatumika kama kufanya nini ikiwa mtoto ameshajifunza masoko kama useremala?

Mwisho mbona fani za Ufundi nyingi sana zimeachwa kwa level ya Mafunzo ya Elimu ya msingi?

Kiufupi sijaona kama itakuwa na Tija sana Kwa mhitimu wa Elimu ya msingi kama hakuendelea na Elimu zaidi.
 
Ningependa nione in deep hiyo computer science wanayosoma ina mawanda gani , sababu computer science tu kwa kuitaja it is more that what we think.

Mitaala ningependa ipunguze miaka ya kukaa darasani iwe 12 tu na pia inclusion ya STEM ipewe kipaumbele otherwise itakua hakuna walichobadili.
Screenshot_20231108-191719.png

Screenshot_20231108-191613.png
 
Elimu ya Ufugaji nyuki ndio nini? Huo ni upuuzi.Bora ingekuwa Elimu ya mazingira,Landscape na Gardening.

Pili Elimu ya Kilimo na Ufugaji inatakiwa ivunjwe vunjwe Ili humo ndani mtoto achague fani za ;

Ufugaji nyuki
Ufugaji wa Kisasa wa mifugo
Kilimo biashara

Najiuliza kwani mtoto akichagua Kilimo atajifunza nini kipya hasa ambacho hakifanyiki kwao Hadi aweze kujiajiri Kwa kutumia gani ya Kilimo na mifugo?

Pili Vyuo vya Veta vitafutwa au vitatumika kama kufanya nini ikiwa mtoto ameshajifunza masoko kama useremala?

Mwisho mbona fani za Ufundi nyingi sana zimeachwa kwa level ya Mafunzo ya Elimu ya msingi?

Kiufupi sijaona kama itakuwa na Tija sana Kwa mhitimu wa Elimu ya msingi kama hakuendelea na Elimu zaidi.
Mkuu jaribu kupitia curriculum yote vyote vimeelezwa
 
Attachments

HAYA NDO MABORESHO YA MTAALA WA ELIMU YANAYOENDA KUFANYIKA TANZANIA KATIKA JITIHADA ZA KUBORESHA ELIMU
Habari za mchana WanaJF

Katika kuboresha elimu, Hivi karibuni serikali ilitangaza mabadiliko ya Kisera Na marekebisho ya Mitaala na baadhi ya
Asante...

Haya ni masomo kwa mujibu wa Rasimu Ya Elimuu..
Asante mkuu,ila nina kaswali kadoogo km itawezekana naomba jibu.

Hapo kwenye masomo ya jumla kwa O level naona yapo 14,je mwanafunzi atalazimika kusoma yote ama anaweza kuchagua ayatakayo?
Je ni yapi ni lazima ayasome kati ya hayo?
 
Tuna heri tuliosoma zamani, maana kwa sasa elimu inazidi kuvurugwa tu...

Kinavhofanyika ni kuifanya elimu ionekane nyepesiiiii....
 
Shida yetu kubwa huwa kwenye utekelezaji. Tu wapangaji wa mipango na waongeaji wazuri sana. Kwenye utekelezaji sasa ndiyo penye changamoto haswa.

Mf. Hao walimu wa kufundisha hayo masomo stadi wapo? Maabara zake je? Au watu wataishia tu kuchora injini ya gari na kuainisha sehemu zake basi imetoka?
 
Asante mkuu,ila nina kaswali kadoogo km itawezekana naomba jibu.

Hapo kwenye masomo ya jumla kwa O level naona yapo 14,je mwanafunzi atalazimika kusoma yote ama anaweza kuchagua ayatakayo?
Je ni yapi ni lazima ayasome kati ya hayo?
Ili nimeliandika hapo juu kwenye maelezo kuhusu Secondary soma tena Ndugu mnafiki
 
Katika vitu ambavyo watunga sera Bado hajatupeleka mbele ni kubaki kutumia lugha ya kufundishia kuwa ni kiswahili, badala ya English
 
Back
Top Bottom