Haya ndio makadirio ya gharama (ukitumia rate za kiserikali) kusafirisha wasanii 40 Korea

Haya ndio makadirio ya gharama (ukitumia rate za kiserikali) kusafirisha wasanii 40 Korea

Hivyo kusafirisha wasanii hao katika kipindi hiko kama zitatoka gharama za serikali itachukua jumla mil 80+160+400 = mil640, au kiufupi ni 0.64 Bilioni, na kama ni serikali imegharamia hii inamaana Fedha hizi zilipitishwa katika finance bill ya Mwaka 23/24!
Kina mwijaku nimesikia wakisifia Silent Ocean, wale huwa hawasifii bure!!
 
Hata hivyo, kinachouma zaidi ni vile tutakavyopewa Kofia, Tshirt, Vitenge na Elfu kumi mwakani. Halafu kwa wingi wetu tutaipigia kura ya ndio ccm. Kwangu hilo linaniuma zaidi.

Tunahongeka kirahisi sana.
 
Na bambo naye kaenda? Na Steven, naye ?
Acha waende, sisi walipa kodi ndiyo tumewasafirisha, watushukuru.
 
Wivu unakutesa...omba na ww next time uende nao
 
Haya mambo yote huwa yapo kwenye finance bill kwenye wizara husika, wakati inapopitishwa bungeni nyie wananchi huwa mpo busy kushabikia yanga na simba sasa utekelezaji wake unapaanza unaanza kulia lia humu!!! Muwe mnafuatilia finance bill sio kuja kulia lia hapa!
 
Wasanii wa kaole wametupwa kule 😄

Ova
 
Kaka utaitwa mchochezi nyamaza - maadamu vijana ambao ndiyo Taifa la leo wamelala fofofo sisi ni kina nani?
 
Gharama mbuzi kabisa hiyo. Imelipwa na watu hata hawaifikirii. Sio serikali. Yaani hiyo imeandikwa kwenye one bank risit au cheque. 640ml ... Wazee tuwe serious. Serikali ingetumia zaidi ya B 1. Gharama za hao watu ni pesa mbuzi sana
 
Kwanza nieleweke, hapa natoa mfano wa Makisio ya jumla ya gharama endapo kama serikali au mtu binafsi ameamua kugaramia safari za wasanii 40 kwa kutumia rates za kiserikali kuwasafirisha kwenda Korea wasanii 40 wa tasnia ya bongo movie kwa ajili ya kwenda kujifunza mambo ya tasnia ya uigizaji kimataifa.

Angalizo wasanii ni watu wenye kipato kikubwa sana sasa huenda walijigharamikia wao wenyewe, ama matajiri wanaosaport serikali waligharamikia safari hii kwa ajili ya kuisaport tasnia ya filamu, japo ni ngumu kwa wafanyabiashara matajiri kutoa fedha pasipo wao kunufaika.

Ndege safari ya kwenda na kurudi Korea ni 4,000,000 x wasanii 40 = 160milioni.

Hotel, ya kiwango cha kawaida ni kama 2,00,000 za Kitanzania Kwa wasanii 40 kwa siku 10 ni kama ni 400*200,000 = 80 milioni.

Posho kwa wasanii 40 arubaini kwa siku kumi itakuwa jumla ya 400 mil.

Hivyo kusafirisha wasanii hao katika kipindi hiko kama zitatoka gharama za serikali itachukua jumla mil 80+160+400 = mil640, au kiufupi ni 0.64 Bilioni, na kama ni serikali imegharamia hii inamaana Fedha hizi zilipitishwa katika finance bill ya Mwaka 23/24!
Bil 1 kasoro
Mama yenu karudi Toka Korea anawafokea watz walipe Kodi
 
Mkuu mambo mengine usipende kuyafukua! Unaweza kupata mgandamizo wa damu usiokuwa wa kawaida.
 
Back
Top Bottom