Daaah ! Hii kesi ya mauaji ya kimbari umewauzia Watanganyika ?
We nI nouma aiseeh !.....tafuteni sababu nyingine ya kuvunja muungano bana !
Mkuu wangu Boko haram, nimeishamwambia sioongei na mbwa naongea na mwenywe mbwa, mabwana zake hawapo kabakia huyo Yericko tu, Nguruvi3, Mag3, wameishamtosa, kama anayaweza aingie... analeta dharau eti uzi wetu umefungwa sababu yake yeye eti alihoji atukujiaandaa, teh teh, sisi kila siku uzi zetu zinafungwa tu wala kwetu siyo tatizo, kuandika uzi humu kunaitaji maandalizi gani uzi zimejaa kila kona, uzi zetu huwa ni hatari zinafunkika uzi zingine mpaka wao wanakuja.
Wewe acha unafiki hebu hapa jisome mwenyewe mabwana zako hawapo sijui utawaita kina nani.
Mnafiki ni chakula ya mamba, wewe kila siku na ulikuwa unatumia hizi hizi video kama ushahidi wa kumtetea bwana wenu Okello leo eti unasema ya kughushi.
Cc.. gombesugu, Boko haram,
kwani ni siri hiyo kwamba jeshi la tanganyika liliivamia zanizbar na kufanya mauwaji ya halaiki ya kinyama na kikatili dhidi ya watu wasio na silaha, wengi wao wakiwa wanawake, watoto, vizee wagonjwa hata walemavu
mazoezi walifanyia tanga na wakatumia bandari ya bagamoyo kuingilia znz, walikuja kidogo kidogo kama raia wa kawaida
muungano hatutaki uvunjike kwa yaliojiri 1964, tunataka uvunike kwa yanajiri sikuhzi
ahsante
Naongea na mwenye mbwa siongei na mbwa.
Kwani kufungwa kwa uzi wetu leo ndiyo siku ya kwanza mbona kawaida uzi zetu kufungwa, wewe umeonya nani humu JF zaidi ya mnafiki tu kauzu wewe.
uloyasema hapa ni kweli tupu 100%.
hata leo znaizbar hatuoni raha kutawaliwa na tanganyika na hili tunalitizamia njia ya kulimaliza pia.
Lakin iinakupasa ujuwe kwamba kuanzia mwaka 650 AD warabu tayari wamefika zanzibar. Na vitabu vipo ziloandika juu ya hilo
Hakuna mtu leo anayethubu kusema znzn ni ya wafrika. Mimi binafsi ninaamini kwamba hakuna mtanganyika alokuwa na sababu ya kuja znz katik amiaka ya 1800s, isipokuwa wale walioletwa.
watu walisafiri sababu ya shida za maisha na huko tanganyika kulikuwa kuko poa sana, wanyama na mazao yalikuwa yanawatosha wenyeji wa huko siku hizo, yaani yata watu kusini hawakuwa na sababu ya kwenda kaskazini
kwa mtazamo huo mwarabu alipokuwa zanzibar alikuwa yupo nyubani kwao kabisa.
Faza; Baada ya salaam
1. Nikusifu kuwa ulijiandaa vizuri sana na mada yako na vielelezo vyako. Hii inaleta raha ya mjadala. Ile video ya KWANZA YA RANGI. ILE NILIYOITILIA MASHAKA TOKA AWALI KWA VIGEZO VYA KAMA PHOTOGRAPHER NI FILAMU YA KUIGA. INAITWA AFRICA ADDIO. LINK HIYO HAPO CHINI
‫
MAELEZO YAKE YA KUTHIBITISHA PIA KUWA NI FILAMU YAPO KWENYE KITABU CHA KWAHERI UHURU...... PG 352
".....Takwimu zinatafautiyana kuhusu binaadamu waliyouliwa katika mapinduzi ya Zanzibar kuanziya watu 5,000 mpaka 18,000.81 Ingelisaidiya sana kama serikali ingewaomba watu waripoti juu ya watu wao waliouwawa ili lithibitike jambo hili. Ile filam ya Kitaliana Africa Addio, imezidisha kuthibitisha kutendeka kwa mauwaji ya halaiki katika Mapinduzi. Idadi ya watu waliouliwa haiwezi kufikiwa kwa sababu wapo watakaotaka idadi iwe ndogo sana ili wajikoshe na wapo ambao watakaotaka idadi iwe kubwa kwa sababu wanawajuwa watu katika kila familia waliyopoteza mtu au watu wao." Kwaheri Uhuru...... pg 352 of 485.
Kwa maana hiyo nakushauri usitumie lugha kuwa waitalia waliipiga LIVE, hii ni MOVIE. Ukiiangalia inavyoanza utaona hadi Title.
Tujadiliane hayo mengine.
Usiku mwema.
Nani asiyejua "mapinduzi" ya Zanzibar yalikuwa Tanganyika sponsored genocide against minority Arabs.
Sio mwalabu,ni mwarabu,bora kukaa kimya kuliko kusema usichokijuwaNicholas
Kwani sheikh yahya na yeye alikuwa mwalabu,
kwani kuna kosa mtu kuwa mwalabu?
kwani kuna kosa mtu kuwapenda waarabu?
Wickama
Mkuu angalau wewe huleti masuala ya vitunguu, maharage na viazi nakushukuru kwa hilo, maana kuna watanganyika humu akili zao zimekufa kabisa wanadhani vitunguu vinaota tanganyika tu na si popote pale duniani kote
sasa raha ya takwimu za kisomi ni hivi, katika uchambuzi wa kitaalamu juu ya mada fulani kila ripoti moja inayotelowa KUSAPOTI ujuwe kuna riporti nyengine inayosema kinyume cha hiyo
Kuhusu kuwa video ya kitaliana ni filamu ya kuekt mimi hainingii akilini, sisemi kama Dr Harith hajui kuhusu video hiyo lakini, hebu tuzingatie haya
1. Kwasabau gani wataliana wafanye documentary hiyo
2. Ni wapi waliirikodi documentary hiyo
3. Ilikuwa mwaka gani?
4. Unajuwa waarabu wa znz ndio walioleta usilami east afrika, wataliana walileta ukiristo, kwanini wafenye documentary inayosapoti uislamu, umewasikia wakisema kwamba waliokuwa wakiuliwa ni waislamu
Kuhusu idadi ya watu waliouliwa katika mauwaji hayo ya kinyama ya watanganyika huko zanzibar, idadi hiyo ya 17,000 elfu ilitolewa an waingereza. Ipo filamu nyengine kabisa walioirikodi waingereza lakini nimeshindwa kuipata.....
lakini nijuwalo mimi ni kwamba maiti zilizagaa mitaani mote mji mkongwe, mwera na kila sehemu ambazo waarabu walikuwa wanaishi. maiti hizo zilizikwa katika makaburi halaiki kwasabau zilikuwa zimeanza kuoza siku wazanzibari walipoanza kuota maiti hizo.
sasa kwa njia moja au nyengine mauwaji haya yamo katika group la genocide
na nakuomba uiweke email hii
siku znz ikochomoka katika makucha ya mkoloni mweusi KESI ITAFUNGULIWA HUKO THE HAGUE MAHAKAMA KUU YA DUNIANI DHIDI YA WATANGANYIKA NA MAUWAJI HAYA
Bin Faza; Aslaam aleykum.
Awali ya yote narudia kama awali, kusema tena. POLE. Sasa kwa tunajua kuwa hiyo ni FILM/FILAMU, na sio live shooting ya DOCUMENTARY mawazo yangu ni kama yafuatayo.
1. Haingewezekana jamaa watoke Tanga/Pangani kuja na kujua waliko WAARABU na WAISLAMU bila KUWAPO mwenyeji wa kuwapokea na kuwaongoza mitaa.
2. Huyu MWENYEJI NDIYE MWENYE DHAMANA KUBWA ya yaliyotokea. Hiyo kesi ya The Hague anzeni na huyo Mwenyeji kama mnamnjua hamna haja ya kusubiri. Ila sio dawa.
3. Katika kitabu cha Dr. Harith imeandikwa wazi kuwa WALIPOFIKA WALE FFU 100 toka Tanganyika, haya mauaji YALIKOMA na shwari ikarudi Angalia Kwaheri UHURU pg 62. Angalau TZ tuna ushahidi kuwa tuliokoa maisha hadi ya sultan mwenyewe.
"......Kusimama [mapinduzi] lililetwa kundi kutoka Tanganyika, la Field Force. Likasimamisha vile vita. Matatizo kutuliza.
Lakini anaendelea chini yake pg 63 kusema
".....wakabaki memba tu wa Baraza la Mapinduzi, kuna chuki sasa za moyo, wakiwaona watu wamekaa au wanasali kuwapiga risasi bure. Yaani ni uwehu tu. Ufahari wao wenyewe, mwenye akili chafu, kutumia vile vitendo"
Faza hawa walijawa na hasira ya siku nyingi kwa kama anavyojieleza mmoja (pg 62);
"....Kifikra na kikubwa ilikuwa, kikambi pale [Sakura] watu walipokuwa wamekaa, tunapoingia, Mungu katusaidia tumeweza, tunapovamia, kwa sababu Waarabu wametuuwa, ili ndipo tulivoweza kupata kutawala pale, kwa sababu wametutia minyororo, wametupofowa macho, wametufanya ngombe kututoa khaswa, wanaake zetu kupasuliwa mimba kuonyeshwa watoto, kwa hivyo na sisi nasi tuwafanye hivyo, waone uchungu.
Wakiona wale watoto wamepasuliwa, mke kapasuliwa na tunamwita mtoto wa Kiafrika, yamefanyika hayo, yamefanyika hayo Unguja, yamefanywa. Kuwa bibi njoo hapa uone mtoto anavokaa ndani ya tumbo. Nani asojuwa Unguja. Walofanya wamefanya. Kwenye vikao vyote walikuwa hisia hiyo wanayo. Ipo tayari. Hiyo ip
Zingatia kuwa kitendo cha kuwaletea askari kulinda maisha na mali ndicho kiliokoa watu zaidi
4. Faza; Kweli historia ni chungu lakini ndio tufanyeje? mimi nadhani dawa ipo kwenye kuridhiana na kujenga hali ya kuamianiana. Mkianza saa hizi tena nani kaja mwaka 650 kamkuta nani, na yupi kaletwa mwaka 1800 kama mtumwa au vinginevyo, hamtaishi kwa amani hata kidogo.
Mimi nadhani hamuwezi kuepuka ukweli kuwa baadhi yenu wana uhusiano na bara arabu kwa wingi kama ilivyo wengine walivyo na uhusiano na bara-afrika kwa wingi. Huo ndio ukweli wa nasaba. Kwisha. matabaka shehe wangu hayataleta amani hapo. Rangi makabila yenu ni kusaidia identity tuuuu, lakini mbora ni mwenye taqwa iliyozidi ndugu yangu. Tulieni mjemnge nchi yenu ustadh wangu kama wa-zenj 100%.
5. Wala jibu sio kauli hii hapa chini
Sultan Jamshid Sultan of Zanzibar
Kauli hizo zinajenga nia ya kulipiza.
Allah Allam
Shukran.
Wickama
Mkuu angalau wewe huleti masuala ya vitunguu, maharage na viazi nakushukuru kwa hilo, maana kuna watanganyika humu akili zao zimekufa kabisa wanadhani vitunguu vinaota tanganyika tu na si popote pale duniani kote
sasa raha ya takwimu za kisomi ni hivi, katika uchambuzi wa kitaalamu juu ya mada fulani kila ripoti moja inayotelowa KUSAPOTI ujuwe kuna riporti nyengine inayosema kinyume cha hiyo
Kuhusu kuwa video ya kitaliana ni filamu ya kuekt mimi hainingii akilini, sisemi kama Dr Harith hajui kuhusu video hiyo lakini, hebu tuzingatie haya
1. Kwasabau gani wataliana wafanye documentary hiyo
2. Ni wapi waliirikodi documentary hiyo
3. Ilikuwa mwaka gani?
4. Unajuwa waarabu wa znz ndio walioleta usilami east afrika, wataliana walileta ukiristo, kwanini wafenye documentary inayosapoti uislamu, umewasikia wakisema kwamba waliokuwa wakiuliwa ni waislamu
Kuhusu idadi ya watu waliouliwa katika mauwaji hayo ya kinyama ya watanganyika huko zanzibar, idadi hiyo ya 17,000 elfu ilitolewa an waingereza. Ipo filamu nyengine kabisa walioirikodi waingereza lakini nimeshindwa kuipata.....
lakini nijuwalo mimi ni kwamba maiti zilizagaa mitaani mote mji mkongwe, mwera na kila sehemu ambazo waarabu walikuwa wanaishi. maiti hizo zilizikwa katika makaburi halaiki kwasabau zilikuwa zimeanza kuoza siku wazanzibari walipoanza kuota maiti hizo.
sasa kwa njia moja au nyengine mauwaji haya yamo katika group la genocide
na nakuomba uiweke email hii
siku znz ikochomoka katika makucha ya mkoloni mweusi KESI ITAFUNGULIWA HUKO THE HAGUE MAHAKAMA KUU YA DUNIANI DHIDI YA WATANGANYIKA NA MAUWAJI HAYA
kaka wapi mimi natako haina umuhimu sana,lakini nitakwambia kuwa umejijibu mwenywe katika hapo nilipoweka red,na hicho ndicho kitu ninachojaribu kuongelea hapa
haya ninayoyaongea hapa nimesoma kwenye vitabu,nimefanya utafiti wangu mwenyewe,lakini namshukuru sana bibi yangu ukoo wake ulikuwa unatokea kisiwa kimoja kinaitwa Tumbatu pale Unguja kutoka na hadith zake alizozisikia kwa bibi zake na kutuhadidhia sisi wajukuu zake ndio nimepata picha kamili ya zanzibar na wazanzibari
kama umesoma vizuri hizi comments zangu nimeandika sehemu nyingi tu wako baadhi ya wazanzibar walikuwa wanamiliki watumwa lakini hakuna mzanzibari aliekuwa mtumwa,kwaufupi kama walikuwa watumwa basi wameletwa hao kutoka nje ya zanzibar,kama unawajua watumwa na unajua sehemu walipozikwa tayari nimeshajbu swala lako,kumbuka zanzibar lilikuwa soko kubwa la kuuza watumwa, watumwa walikuwa wakiletwa kutoka sehemu mbali za bara Afrika,sehemu kama kongo nk,mmoja kati ya wafanya biashara za watumwa alikuwa mswahili mmoja anaeitwa kwa jina la Tiptip huyu jamaa alikuwa na jeshi la watu 2000 ambalo alikuwa anaingia nalo ndani ya Afrika na kuchukua watumwa!!,Notorious
Nani wazanzibari nimeshaeleza kwenye moja za commets zangu,haina haja ya mimi kurudia kuandika tena hapa,Haya yote ninayoandika sio tu kama nimesoma bali pia ni history iliopo katika ukoo wangu,wazee wanaongea watoto tunasikiliza halafu tuna weka moja na moja tunapata jibu 😉
Sio kila mtu mweusi allikuwa mzanzibar na sio kila mwarabu alikuwa mzanzibari 😉
haya kaka siku jema au usiku mwema
ni matarajio yangu kwamba msumari umechoma ndipo
Bin Faza,
Salaam.
Nimetimiliza ile ahadi yangu na nimerejea.
Yawezekana ni kweli hayo ulosema, yakuwa ule msumari ulichoma palipokusudiwa!?
Tuko pamoja!
Ahsanta.
...miongoni mwa dhambi ya wageni wote waliokuja afrika ni pamoja na kupindapinda ukweli, mfano huo wa ati "zanzibar hapakuwa na maisha rasm"...lol..lugha ya wakoloni wote ilikuwa hivyo..!..unasema mshirazi na mwarabu si watu wa mbali..swadakta..je mwafrika na mwarabu? hapa ishu ni ukoloni wa waarabu ktk zanzibar..! kwenye kikao cha wakoloni cha mwaka 1884, sultan wa oman alikuwepo..! na kwenye mgawo alipewa zanzibar na pwani yote ya afrika mashariki(mogadishu to beira)...! hujui hiyo historia? umesomea wapi kaka, arabuni? hunajua kuwa kulikuwa na tawala nyingi ktk afrika lkn sababu hazikuwa na malengo ya kikoloni hazikushirikishwa kwenye mkutano huo...!hivi ndugu yangu we hujui kuwa ukoloni ni ukoloni tu? kisha nakuona we ni "mwelewa", niambie tafsiri ya kisomi ya ukoloni, kisha uniambie ukoloni wa tanganyika ktk zanzibar..mbona unakuwa na hoja za "kichimvi mno" ambazo ni kichekesho kinachoashiria mapungufu ya kujenga hoja kwa mwanazuoni wa kiwango cha kuchangia kwenye jf?...! jamsheed alikuwa msomi yakhe..! msomi kweli kweli..! na anajua kwenda na ukweli na wakati, bahati mbaya waliomzunguka ambao aliwaamini hawakuwa wakimpa ukweli wa mitaani ili afanye mabadiliko yaliyohitajika ambayo yangeepusha dhulma iliyowakuta maelf ya wanyonge ambao walidhulumiwa nafsi zao na mapinduzi matukufu..! stay blessed bro..! salaam!RED Xs
Kwanza sio kweli kwamba washirazi walifanya mapinduzi, washirazi ijapokuwa wanajisema wao ndio wenyeji wa znz lakini kabila lao linatokea Persia, irani ya siku hizi katika mji uitwao Shiraz. Hassan Bin Ali alikuja na watoto wake 7 wakaanzisha Zenj Empire ya kwanza, znz hapukuwa na maisha rasmi, wao wakapafanya ndio kituo chao kuchukuwa maji na mapuumziko kidogo kidogo ndio pakawa na life.
Kwahivo mshiraji na mwarabu sio watu mabli sana, wao hawakushiriki katika mapinduzi
Mapinduzi yalifanywa na watanganyijka, na ikiwa kwa ukweli huu unananihisi mimi ninakuchukieni basi ndio ninakuchukieni kwa kuivamia nchi yetu na kutuulia jamaa zetu kiholela.
wewe utafurahi kama sisi wazanzibar tutakuja tabora au iringa au popote huko tanganyika na kukuuweni kiholela? Jee kwa hilo utatupenda sisi wazanzibari?? be honest pleae!!!!!!
...unazungumzia jambo la kuja kwetu tabora na iringa..tuwekane sawa..mi mzaznibar pia..mngazija...si mshirazi wala si mwarabu..alhamdullillah..lkn nawehishim na nawapenda washirazi na waarabu..! lkn naupenda zaidi ukweli..!na ikitokea baadhi ya wazanzibar wakataka kwenda iringa au tabora au mahali popote pale kwenda kuwatendea yasiyofaa wenyeji wa huko mimi nitakuwwa wa kwanza kukabiliana nao..! na ilikuwa bahati mwaka nazaliwa mapinduzi yalikuwa tayari, vinginevyo nachelea ningefanya nini, sababu, nisingeukubali ukoloni..! isitoshe mafundisho matakatifu ya imani yangu yananifundisha kuwa usultan na ufalme, na uongozi wowote wa kurithishana ni kinyume na mafundisho yangu matakatifu...alivyotoka bwana mtume (saw) hakufuata hadhrat ali (as) sababu mojawapo ni nasaba yao, ingekuwa ni kurithishana madaraka ya dola ya kwanza na ya pekee ya kiislam..!RED Xs