Bin Faza; Aslaam aleykum.
Awali ya yote narudia kama awali, kusema tena. POLE. Sasa kwa tunajua kuwa hiyo ni FILM/FILAMU, na sio live shooting ya DOCUMENTARY mawazo yangu ni kama yafuatayo.
1. Haingewezekana jamaa watoke Tanga/Pangani kuja na kujua waliko WAARABU na WAISLAMU bila KUWAPO mwenyeji wa kuwapokea na kuwaongoza mitaa.
2. Huyu MWENYEJI NDIYE MWENYE DHAMANA KUBWA ya yaliyotokea. Hiyo kesi ya The Hague anzeni na huyo Mwenyeji kama mnamnjua hamna haja ya kusubiri. Ila sio dawa.
3. Katika kitabu cha Dr. Harith imeandikwa wazi kuwa WALIPOFIKA WALE FFU 100 toka Tanganyika, haya mauaji YALIKOMA na shwari ikarudi Angalia Kwaheri UHURU pg 62. Angalau TZ tuna ushahidi kuwa tuliokoa maisha hadi ya sultan mwenyewe.
"......
Kusimama [mapinduzi] lililetwa kundi kutoka Tanganyika, la Field Force. Likasimamisha vile vita. Matatizo kutuliza.
Lakini anaendelea chini yake pg 63 kusema
".....wakabaki memba tu wa Baraza la Mapinduzi, kuna chuki sasa za moyo, wakiwaona watu wamekaa au wanasali kuwapiga risasi bure. Yaani ni uwehu tu. Ufahari wao wenyewe, mwenye akili chafu, kutumia vile vitendo"
Faza hawa walijawa na hasira ya siku nyingi kwa kama anavyojieleza mmoja (pg 62);
"....Kifikra na kikubwa ilikuwa, kikambi pale [Sakura] watu walipokuwa wamekaa, tunapoingia, Mungu katusaidia tumeweza, tunapovamia, kwa sababu Waarabu wametuuwa, ili ndipo tulivoweza kupata kutawala pale, kwa sababu wametutia minyororo, wametupofowa macho, wametufanya ngombe kututoa khaswa, wanaake zetu kupasuliwa mimba kuonyeshwa watoto, kwa hivyo na sisi nasi tuwafanye hivyo, waone uchungu.
Wakiona wale watoto wamepasuliwa, mke kapasuliwa na tunamwita mtoto wa Kiafrika, yamefanyika hayo, yamefanyika hayo Unguja, yamefanywa. Kuwa bibi njoo hapa uone mtoto anavokaa ndani ya tumbo. Nani asojuwa Unguja. Walofanya wamefanya. Kwenye vikao vyote walikuwa hisia hiyo wanayo. Ipo tayari. Hiyo ip
Zingatia kuwa kitendo cha kuwaletea askari kulinda maisha na mali ndicho kiliokoa watu zaidi
4. Faza; Kweli historia ni chungu lakini ndio tufanyeje? mimi nadhani dawa ipo kwenye kuridhiana na kujenga hali ya kuamianiana. Mkianza saa hizi tena nani kaja mwaka 650 kamkuta nani, na yupi kaletwa mwaka 1800 kama mtumwa au vinginevyo, hamtaishi kwa amani hata kidogo.
Mimi nadhani hamuwezi kuepuka ukweli kuwa baadhi yenu wana uhusiano na bara arabu kwa wingi kama ilivyo wengine walivyo na uhusiano na bara-afrika kwa wingi. Huo ndio ukweli wa nasaba. Kwisha. matabaka shehe wangu hayataleta amani hapo. Rangi makabila yenu ni kusaidia identity tuuuu, lakini mbora ni mwenye taqwa iliyozidi ndugu yangu. Tulieni mjemnge nchi yenu ustadh wangu kama wa-zenj 100%.
5. Wala jibu sio kauli hii hapa chini
Sultan Jamshid Sultan of Zanzibar
Kauli hizo zinajenga nia ya kulipiza.
Allah Allam
Shukran.