Wakuu,
Ndio walikuwa wanajitapa na uhuru wa kutoa maoni kuongezeka. Kauli za kichochezi inatakiwa kutolewa maana. Huku ni kutufanya mabubu wazi wazi.
======
HATI YA MAKOSA
KOSA LA KWANZA
Kutoa wimbo kwa walaji bila kibali, kinyume na Kanuni ya 25(1) ya Kanuni za Baraza la Sanaa la Taifa, 2018.
MAELEZO YA KOSA
Msanii Emmanuel Elibariki
Nay wa Mitego mnamo tarehe 24/09/2024, huku ukijua kwamba ni kinyume na Kanuni, ulitoa wimbo unaoitwa NITASEMA kwa walaji kabla ya kupewa kibali cha kuthibitisha kuwa maudhui yake yamezingatia maadili.
KOSA LA PILI
Kutoa wimbo ambao maudhui yake yanahamasisha uchochezi kinyume na Kanuni 25(6)(d) ya Kanuni za Baraza la Sanaa la Taifa, 2018.
MAELEZO YA KOSA
Msanii Emmanuel Elibariki
Nay wa Mitego mnamo tarehe 24/09/2024, huku ukijua kwamba ni kinyume na Kanuni, ulitoa wimbo unaoitwa NITASEMA ambao baadhi ya mashairi yake yanahamasisha vitendo vya uchochezi dhidi ya Serikali kwa madai kwamba Serikali inahusika katika kufanya vitendo vya utekaji na mauaji ya watu.
KOSA LA TATU
Kutoa wimbo ambao maudhui yake yanapotosha jamii, kinyume na Kanuni 25(6)(b) ya Kanuni za Baraza la Sanaa la Taifa, 2018.
MAELEZO YA KOSA
Msanii Emmanuel Elibariki
Nay wa Mitego mnamo tarehe 24/09/2024, huku ukijua kwamba ni kinyume na Kanuni ya 25(6)(b), ulitoa wimbo unaoitwa NITASEMA ambao baadhi ya mashairi yake yanapotosha jamii kwa kuiaminisha kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameshindwa kutekeleza majukumu yake hivyo nchi inazama, na kwamba miradi ya maendeleo ilioachwa na mtangulizi wake imetelekezwa.
KOSA LA NNE
Kutoa wimbo ambao maudhui yake ni kukashifu mataifa mengine kinyume na Kanuni 25(6)(h) ya Kanuni za Baraza la Sanaa la Taifa, 2018.
MAELEZO YA KOSA
Msanii Emmanuel Elibariki
Nay wa Mitego mnamo tarehe 24/09/2024, huku ukijua kwamba ni kinyume na Kanuni ya 25(6)(h), ulitoa wimbo unaoitwa NITASEMA ambao baadhi ya mashairi yake yanakashifu nchi ya Rwanda na nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa kudai kwamba nchi hizo hazina usalama, jambo ambalo linaweza kusababisha nchi ya Tanzania kuingia kwenye mgogoro wa kidiplomasia na nchi hizo.
E.E. Buganga
Kny: KATIBU MTENDAJI
27/09/2024
Nakala: Katibu Mtendaji aione kwenye Jalada
Soma Pia: Ney wa Mitego aitwa BASATA kujadili wimbo wake wa ‘Nitasema’
View attachment 3108238View attachment 3108237