Pre GE2025 Haya ndiyo makosa ambayo BASATA wanamtuhumu Nay wa Mitego kutokana na wimbo wake wa "Nitasema"

Pre GE2025 Haya ndiyo makosa ambayo BASATA wanamtuhumu Nay wa Mitego kutokana na wimbo wake wa "Nitasema"

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Mbona Mwigulu alisema watu wahamie Burundi??
 
basata ni masalia ya ujamaa wa kijima uliotaka kulazimishiwa wabongo na viongozi wake wa mchongo ambao bado wapo na wanazidi kurudi nyuma kwenye akili zao
 
ney ni mpumbavu wenzie wanatafuta hela yeye anaangaika uhanaharakati uchwara, kaingia kwenye kumi na nane za maria sarungi yule mwanamke ni nyoka
Mpumbavu ni wewe ambaye unaona hali mbaya ambako wanaotegemewa kutulinda (polisi) wanatajwa na wahanga kama Sativa wanawataja akina Mafwele lakini wanaowataja wanafunguliwa mashtaka kama Boni Yai.

Ukiamua kuwa muoga na huna guts bure ukae kimya ila anayesema kweli aache aseme kweli
 
Kwani yule aliedai kwamba "Tuhamie Burundi" kisa wananchi kukataa matozo yao yasiyo na kichwa wala miguu, yeye alifunguliwa KESI ya aina gani?
Kuhakikishiwa kula kwenye nafasi nyeti pale hazina kiasi cha kuwa na hela ya kununua timu ya mpira
 
Katika watu hawajui kuimba ni huyo Ney wa mitego alikosea kila kitu kwanzia kuchagua jina lake la sanaa mwanaume unajiitaje Ney alaf wa mitego!
Aachwe asifungiwe
Hivi wewe ni jinsia gani unayemuonea wivu mwenzio
 
Hivi yupo mtaani huyu alifaa kumfuata Bon yai aliko

USSR
 
ney ni mpumbavu wenzie wanatafuta hela yeye anaangaika uhanaharakati uchwara, kaingia kwenye kumi na nane za maria sarungi yule mwanamke ni nyoka
Screenshot_20240927-082932.png
 
ney ni mpumbavu wenzie wanatafuta hela yeye anaangaika uhanaharakati uchwara, kaingia kwenye kumi na nane za maria sarungi yule mwanamke ni nyoka

Huyo Ney wa mitego kama hatafutu hela wewe ndio unamtunzia familia yake!? Nyimbo za harakati ni nyimbo sawa na nyingine ,unataka waimbaji wote waombe nyimbo za mapenzi!?au inataka wote wawe machawa!?Kila mmoja na maudhui yake
 
Wakuu,

Ndio walikuwa wanajitapa na uhuru wa kutoa maoni kuongezeka. Kauli za kichochezi inatakiwa kutolewa maana. Huku ni kutufanya mabubu wazi wazi.

======
HATI YA MAKOSA

KOSA LA KWANZA

Kutoa wimbo kwa walaji bila kibali, kinyume na Kanuni ya 25(1) ya Kanuni za Baraza la Sanaa la Taifa, 2018.

MAELEZO YA KOSA

Msanii Emmanuel Elibariki Nay wa Mitego mnamo tarehe 24/09/2024, huku ukijua kwamba ni kinyume na Kanuni, ulitoa wimbo unaoitwa NITASEMA kwa walaji kabla ya kupewa kibali cha kuthibitisha kuwa maudhui yake yamezingatia maadili.

KOSA LA PILI

Kutoa wimbo ambao maudhui yake yanahamasisha uchochezi kinyume na Kanuni 25(6)(d) ya Kanuni za Baraza la Sanaa la Taifa, 2018.

MAELEZO YA KOSA

Msanii Emmanuel Elibariki Nay wa Mitego mnamo tarehe 24/09/2024, huku ukijua kwamba ni kinyume na Kanuni, ulitoa wimbo unaoitwa NITASEMA ambao baadhi ya mashairi yake yanahamasisha vitendo vya uchochezi dhidi ya Serikali kwa madai kwamba Serikali inahusika katika kufanya vitendo vya utekaji na mauaji ya watu.

KOSA LA TATU

Kutoa wimbo ambao maudhui yake yanapotosha jamii, kinyume na Kanuni 25(6)(b) ya Kanuni za Baraza la Sanaa la Taifa, 2018.

MAELEZO YA KOSA

Msanii Emmanuel Elibariki Nay wa Mitego mnamo tarehe 24/09/2024, huku ukijua kwamba ni kinyume na Kanuni ya 25(6)(b), ulitoa wimbo unaoitwa NITASEMA ambao baadhi ya mashairi yake yanapotosha jamii kwa kuiaminisha kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameshindwa kutekeleza majukumu yake hivyo nchi inazama, na kwamba miradi ya maendeleo ilioachwa na mtangulizi wake imetelekezwa.

KOSA LA NNE

Kutoa wimbo ambao maudhui yake ni kukashifu mataifa mengine kinyume na Kanuni 25(6)(h) ya Kanuni za Baraza la Sanaa la Taifa, 2018.

MAELEZO YA KOSA

Msanii Emmanuel Elibariki Nay wa Mitego mnamo tarehe 24/09/2024, huku ukijua kwamba ni kinyume na Kanuni ya 25(6)(h), ulitoa wimbo unaoitwa NITASEMA ambao baadhi ya mashairi yake yanakashifu nchi ya Rwanda na nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa kudai kwamba nchi hizo hazina usalama, jambo ambalo linaweza kusababisha nchi ya Tanzania kuingia kwenye mgogoro wa kidiplomasia na nchi hizo.

E.E. Buganga
Kny: KATIBU MTENDAJI
27/09/2024​

Nakala: Katibu Mtendaji aione kwenye Jalada

Soma Pia: Ney wa Mitego aitwa BASATA kujadili wimbo wake wa ‘Nitasema’

View attachment 3108238View attachment 3108237

 
Hakuna kesi hapo...

Huu Moja kwa moja ni uvamizi na tishio la uhuru wa watu kujieleza katika mtindo wa kukosoa...

Makosa yote ni kwa sababu tu "Rais Samia" na "serikali" wameguswa kwa kukosolewa....

Na kwa hiyo logic ya kila kosa ni kumlinda mtu, binadamu mwenye cheo cha "Rais" na watu wake wanaoitwa "serikali..."

Wajinga hawa. Rais na serikali ni kitu gani kwani? Hawa si ni watu/binadamu tu ambao wanakosea na kustahili kukosolewa kwa ukali wote...?

Badala taasisi zetu hizi zihangaike kulinda nchi/taifa letu, zinahangaika kutetea na kulinda mtu/watu wajinga na wapumbavu wanaojiita "serikali" lakini walioshindwa kuongoza taifa hili zuri la Tanganyika na watu wake kuelekea katika nchi ya asali na maziwa...
 
Back
Top Bottom