Yes, hiyo ilikuwa ni miaka 15 iliyopita na mwaka 2018 alipata tatizo lingine linalofanana kama hilo
Hilo tatizo lilikuwa kama ni ukichaa, watu wakasema amelogwa, mume wake ikabidi ampeleke kwa kanisani aombewe.
Baadaye zikarudi taarifa mchungaji kapigwa na kiti cha plastic halafu kuna uharibifu aliufanya. Ikabidi uongozi wa kanisa umfunge kwenye chumba ambacho yuko pele yake.
Halafu mikono wakaifunga kwenye bomba la chuma, sisi tunaenda kumuona tunakuta ile kamba imemchuna mikono mpaka damu kwasababu alikuwa anahangaika kujitoa kwenye ile kamba.
Niliingiwa na hasira kwa jinsi nilivyomuona Sister ila nilijizuia ikabidi niombe kumchukua Sister kumpeleka hospitali.
Huko alikutwa na Malaria ya kichwa akapewa dripu za kutosha akaandikiwa na dawa
Ambapo mpaka saizi bado yupo kwenye dose ya hizo dawa