Uchaguzi 2020 Haya ni mambo 10 niliyoona kwa CCM Vs CHADEMA mpaka sasa kuelekea kipute cha kampeni rasmi

Wakuu,

1) What a match!, Mpaka sasa CCM inabebwa na watu wenye experience ambao kipindi kama hiki ndio unajua uwezo wao. Wao kelele nyingi ziko kwenye mipango (strategies) kuliko kelele na matamko ya majukwaani.

2) Tundu Lissu is impressive as usual lakini seems Chadema hawakumuandaa, experience yake ya uanaharakati ndio unaofanya aonekane active uwanjani lakini bado hajawa na madhara kihoja ingawa bado mapema. Mambo ya kusema atamshtaki JPM kwa rushwa ya kununua jogoo laki moja ni uanaharakati si level zake tena kama mgombea Urais.

3) John Pombe Magufuli yuko composed sababu ya records zake awamu hii ya kwanza. Lakini pia kwasasa nguvu kubwa ipo kwenye kupanga vyema mabeki Majimboni na Udiwani. Hapo ndio unapoona timu kubwa na yenye watu wazoefu inavyohandle mchezo. Ni kama wameamua kuacha wapinzani wacheze huku wao wakikamilisha ramani ya ushindi.

4) Kimbinu Chadema wanahitaji timu bora kumzunguka Lissu wakiwemo waandamizi wa serikali zilizopita akiwemo Nyalandu ili kumshape Lissu kama Mgombea Urais lakini pia mipango ya kusaidia kampeni Majimboni ambako hali si nzuri

5) Kimbinu CCM wana kazi kubwa ya kumaliza mchakato wa wagombea Ubunge na Udiwani bila mpasuko lakini maeneo mengi kimbinu wamejipanga kushinda.

6) John Pombe Magufuli takwimu zinambeba na wananchi wanajua matokeo yake wakimchagua tofauti na Lissu ambaye anapaswa kujikita kwenye hoja zenye matarajio ya wananchi hasa wanyonge walio wengi. Je ataweza kuaminisha wananchi ili wamchague?

7) Financially CCM wako stable kuhandle kampeni kuliko CHADEMA ambayo imepanga pia kusimamisha wagombea majimbo yote.

8) John Pombe Magufuli amefanikiwa kuhakikisha watendaji wake wote wanajua takwimu za mambo yaliyofanyika awamu hii hivyo itabidi kila hoja za Lissu zinazogusa takwimu ajipange otherwise akikosea atapingwa hata na Makatibu Tarafa. Hizo takwimu zimeimbwa muda mrefu na hata wananchi wengi wamezikariri.

9) Angalizo, Lissu usihangaike na wimbo wa katiba mpya hauna mashiko kwa wananchi wanyonge na hautampa kura. John Pombe Magufuli pia awekeze hoja kwenye mipango mipya hasa mapinduzi kwenye kilimo na uwekezaji.

10) Wapinzani bila kusimamisha mgombea mmoja huu utakuwa uchaguzi mgumu hadi majimboni kuliko wakati wowote.

Mizania pima mwenyewe, hayo ni maoni yangu binafsi [emoji41]
hamna point ya msingi zaidi ya #9 kwa huu ugumu wa maisha nahc wananchi wenyewe ndo wamuzi
 
Hivi huyo magufuli takwimu gani zinambeba?

Hali ya kiuchumi Kwa wananchi ikoje? Kwa wakulima wa mbaaazi, korosho, tumbaku takwimu zikoje?

Suala la ajira kwa vijana kafanya nini? Ameua uwekezaji na sekta binafsi kaishia kufanya maelfu ya vijana kuwa jobless na watu kupoteza ajira

Ameua watu, kubambikia watu makesi, kuonea watu mpaka hata watoto wadigo wanajua

Ameharibu biashara kupelekea watu kufunga biashara zao na wengine kufirisiwa na mabenki?

Huyo magufuli kafanya ya nini zaidi ya haya? Njia ni nyeupe sana kwa Tundu Lissu mwaka huu.
Ameeen, na iwe hivyoooo
 
Huku mkisahau mbinu ya mwisho ya chama chakavu
..TL anatakiwa ajielekeze ktk kuwaelimisha wapiga kura jinsi gani ataboresha hali zao za kiuchumi.

..kwa mfano, kama ni bodaboda basi aeleweshwe mabadiliko yatakayomgusa na kumuwezesha kutoka kuwa na bodaboda moja kwenda mbili.

..kama ni kijana aliyemaliza masomo, basi anatakiwa aeleweshwe mabadiliko yatakayotokea ambayo yatamuwezesha siyo kupata ajira tu, bali kupata ajira anayoipenda au kuitamani.

..kama ni mzazi ana mtoto shuleni ahakikishiwe kwamba elimu itakayoipata mwanawe itamuwezesha kujitegemea na kuwa msaada kwa wazazi wanaomsomesha as long as anajituma. Na kwamba elimu na maarifa atakayoyapata yatamuwezesha kufanikiwa ktk soko la ajira za kazi ndani na nje ya Tanzania.

..WAKULIMA nao waelimishwe jinsi gani wataweza kukua. Wakulima wadogo waelewezwe mipango itakayowawezesha kuwa wakulima wa kati. Wakulima wa kati waeleweshwe mipango itakayowawezesha kupanda daraja na kuwa wakulima wakubwa.

..Kwa maoni yangu, kufanikiwa au kutokufanikiwa kwa Tundu Lissu kutatokana na aina ya ILANI ya uchaguzi waliyoiandaa CDM na wasaidizi wake wa kampeni wanamuandaa vipi. Pamoja na umahiri wa TL ktk kujenga hoja na kulitawala jukwaa CDM wawe makini kumuongoza ktk kuzungumza yale yanayowagusa wananchi.
 
Tunatazama matendo yako juu na maneno yako tunajua rangi yako
We unaniita me Ni CCM lakini last week mashabiki wa CCM walikuwa wananiita me Ni mshabiki wa CHADEMA baada ya kuleta hoja ambayo haikuwapendeza sasa sijajua mnawazaga Nini?
 
Wanavamia mkutano na bado wanalindwa na polisi!!? hivi hii inaweza kutokea kunako mkutano wa ccm? jamani polisi nyieee

hamna mtu alievamia apo ndo maana mwandishi amehoji wote waliokuepo apo: acheni cheap politics
 
Sio cheap politics, hao polisi hujawaona? kwanini wahojiwe kwenye uwanja wa mkutano wa chama kingine? hizo fujo kweli huzioni?
 
Wakuu,

1) What a match!, Mpaka sasa CCM inabebwa na watu wenye experience ambao kipindi kama hiki ndio unajua uwezo wao. Wao kelele nyingi ziko kwenye mipango (strategies) kuliko kelele na matamko ya majukwaani.

2) Tundu Lissu is impressive as usual lakini seems Chadema hawakumuandaa, experience yake ya uanaharakati ndio unaofanya aonekane active uwanjani lakini bado hajawa na madhara kihoja ingawa bado mapema. Mambo ya kusema atamshtaki JPM kwa rushwa ya kununua jogoo laki moja ni uanaharakati si level zake tena kama mgombea Urais.

3) John Pombe Magufuli yuko composed sababu ya records zake awamu hii ya kwanza. Lakini pia kwasasa nguvu kubwa ipo kwenye kupanga vyema mabeki Majimboni na Udiwani. Hapo ndio unapoona timu kubwa na yenye watu wazoefu inavyohandle mchezo. Ni kama wameamua kuacha wapinzani wacheze huku wao wakikamilisha ramani ya ushindi.

4) Kimbinu Chadema wanahitaji timu bora kumzunguka Lissu wakiwemo waandamizi wa serikali zilizopita akiwemo Nyalandu ili kumshape Lissu kama Mgombea Urais lakini pia mipango ya kusaidia kampeni Majimboni ambako hali si nzuri

5) Kimbinu CCM wana kazi kubwa ya kumaliza mchakato wa wagombea Ubunge na Udiwani bila mpasuko lakini maeneo mengi kimbinu wamejipanga kushinda.

6) John Pombe Magufuli takwimu zinambeba na wananchi wanajua matokeo yake wakimchagua tofauti na Lissu ambaye anapaswa kujikita kwenye hoja zenye matarajio ya wananchi hasa wanyonge walio wengi. Je ataweza kuaminisha wananchi ili wamchague?

7) Financially CCM wako stable kuhandle kampeni kuliko CHADEMA ambayo imepanga pia kusimamisha wagombea majimbo yote.

8) John Pombe Magufuli amefanikiwa kuhakikisha watendaji wake wote wanajua takwimu za mambo yaliyofanyika awamu hii hivyo itabidi kila hoja za Lissu zinazogusa takwimu ajipange otherwise akikosea atapingwa hata na Makatibu Tarafa. Hizo takwimu zimeimbwa muda mrefu na hata wananchi wengi wamezikariri.

9) Angalizo, Lissu usihangaike na wimbo wa katiba mpya hauna mashiko kwa wananchi wanyonge na hautampa kura. John Pombe Magufuli pia awekeze hoja kwenye mipango mipya hasa mapinduzi kwenye kilimo na uwekezaji.

10) Wapinzani bila kusimamisha mgombea mmoja huu utakuwa uchaguzi mgumu hadi majimboni kuliko wakati wowote.

Mizania pima mwenyewe, hayo ni maoni yangu binafsi [emoji41]
Great thinker at his best 👍
 
Nikwambie ukweli ktk uchaguz ambao ccm hawakujipanga ni huu, pia ktk uchaguz ambao chadema wamejipanga ni huu, ccm hawakujipanga kwasababu hawakutegemea kama upepo ungebadili iv, ukweli ni kwamba ccm walipanga sana kutumia vyombo vya dola kupata ushindi, na mbinu iliyokuwa inategemewa kwa asilimia zote ni hiyo, Ila lissu baada ya kuja Lissu upepo umebadilika hawaelewi wafanye nini, wanashindwa kujibu hoja zinazowahusu, wanakimbilia kumtetea msajili ovyo kabisa, kiukweli Lissu kawashika pabaya sana, had mmeanza kula maindi ya kuchoma bilakupenda
 
Back
Top Bottom