Wilderness Voice
JF-Expert Member
- May 19, 2016
- 921
- 1,649
- Thread starter
- #201
Unadhani dhambi ni hiyo tu! Ha ha ha ha!Mimi kwangu ni poa tu hata nikifa kesho maana sijifanyi Mungu mtu.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Unadhani dhambi ni hiyo tu! Ha ha ha ha!Mimi kwangu ni poa tu hata nikifa kesho maana sijifanyi Mungu mtu.
Sawa mkuu, tuseme uko sahihi, hapo lugha ya hovyo ni ipi?Hiyo si chuki nakupa ukweli, ndo maana nimesema usihukumu. Neno linasema ukihukumu nawe utaukumiwa. Jenga hoja si kuleta lugha za hovyo kwangu. Humu nadani mnadhani ukija kwa matusi utaogopwa. Unavyokuja nami nakuja kihivyo! Pia usiwadharau wasukuma. Ebu nawe weka wazi kabila lako uchambuliwe!
Ondoa chuki za kikabila, huo ni ushetwani!
Mimi nasewa Jiwe huko aliko afe tena, haya nenda kalie au kashitaki huko.Ok, sasa unavyo mhukumu umepata faida gani! Zaidi unamkosea Mungu alie sema usihukumu na we ukaja hukumiwa! Watu mnashindana na marehemu, sijawahi ona akili kama hii nchi yoyote!
Ni kujifariji kusiko na fikra!
Hiiiiiiii bha ghoshaaaaaaaHawa watu wenye chuki kwa magufuli wanadhani wanaogopwa. Wanakuja na matusi. Acha nile nao sahani moja. Wasidhani tunawaogopa! Wakajiona ndo wenye kusema. Upumbavu utajibiwa kipumbavu! Heri niwe mwehu lakini nibaki nikitetea ninacho kiamini! Nitasema kweli daima fitina kwangu mwiko! Let me enjoy them, nina muda na ninanguvu za kuwajibu!
Huwezi kuzuia furaha za watu kwa kifo Cha yule binadamu katili Kama mpaka Leo tunafurahia kifo Cha Hitler na IDI amini hata Cha jpm ni shangwe maana hata yeye alifurahia kifo Cha lisu Ben Azory akwilina nk
Hata kuelewa point uliyoulizwa hujui unakalia kuruka ruka kama bisi. Lini ulikemea maovu ya huyo mwendakuzimu kipindi akiwa hai? Au wewe hukuona tatizo ila umeona kipindi hiki watu wanafurahia mtesi wao kwenda kuzimu ndiyo umeona kosa. Kuna mdau kasema acha mahaba kwani yamekupotosha macho.Mwenye hukumu ni Mungu pekee na si mwanadamu.
Mungu aliona hatma ya taifa na ndio maana aliingilia Kati ; trust me angeongoza miaka kumi Kuna watu uzalendo ungewashinda na uvumilivu ungeisha watu wangeanza kukinukisha live na damu nyingi ingemwagika magufuli alikuwa analipeleka taifa ukingoni mwa uvumilivu wa kawaida.
Dah kweli Mungu Fundi...manake tuliteseka vya kutosha miaka mitano ya awamu ya JPM ...Asante Mungu kwa kuturudishia ubinadamu,amani na upendoKifo ni tukio la kiasili. Katika imani kadhaa za kidini zina elezea kifo kilitokea baada ya Adamu na Hawa (Eva) kwenda kinyume na mapenzi ya muumba wao (MUNGU). Ndipo Mungu alitamka kuwa tutakufa, au kurejea katika mavumbi.
Binadamu wa kwanza kufa alikuwa Abeli. Ambaye aliuliwa na kakaye aitwae Kaini. Kaini japo alimuuwa Abeli, bado Mungu alimlinda Kaini na hata akasema atakae muuwa kaini basi atalaaniwa. Hivyo Mungu alimpeleka Kaini nchi ya mbali. Hii yote kumuepusha na kumlinda na mabaya. Mungu alifanya haya yote japo Kaini alikuwa na dhambi ya kumuuwa nduguye.
Mungu utazama tofauti, na macho ya binadamu. Na Mungu ndiye mwenye uweza wa kuhukumu. Siku hizi Tanzania hii kumezuka, tabia ambayo inaonesha watu kufurahia kifo au vifo vya watu wengine. Na kama walikuwa hawampendi huyo mtu au watu; ndo watazusha mengi. Wabaya wake watajifanya wao ni mungu (Mungu), watahukumu, watasema huyu alifanya mabaya ndo maana kafa.
Watajiona wao waliobaki ndo wajanja, hawana makosa au dhambi mbele ya Mungu. Najiuliza hivi kuna mahala popote pale iwe katika misaafu au maandiko yoyote ya kidini na imani zinginezo, pana sema mtu anae kufa mapema au kabla ya wenzie ana dhambi na Mungu kaamua kumkomoa?
Nachojua Mungu alisema tutakufa, hakuna atakaeishi milele hapa duniani. Ndo maana watu ufa wakiwa watoto wachanga, wakiwa vijana, wakiwa wazee, na hata watoto wengine ufia tumboni mwa mama zao kabla ya kuzaliwa.
Tukidai kufa mapema ni kukomolewa na Mungu, ebu tuangalie, hawa mitume wetu, walikufa bado wakiwa vijana, na walikuwa na maadui wengi, hawakupendwa. Yesu kristo aliishi miaka isiyozidi thelathini na tatu. Na alianza kazi ya kuhubiri akiwa na miaka thelathini tu. Vile vile kwa mtume Muhamad S.W.A alikufa mapema. Si hao tu ni wengi!
Hivyo kifo ni asili. Nachoamini kila mtu anakusudi la kuwepo duniani. Na pia ana muda wake wa kuishi. Haijalishi ni miaka mingapi. Muda ukifika Mungu ndo mwamuzi wa yote, uondoke au aseme bado ubaki.
Katika kila jambo Mungu anamakusudi yake. Laweza kuwa baya au zuri, lakini Mungu anatazama tofauti na tunavyotazama sisi wanadamu.
Kikubwa tusijipe kazi ya Mungu ikawa kazi yetu. Tusijipe kuhukumu kwani hukumu ya maisha yetu utolewa na Mungu. Usihukumu usije hukumiwa.
Nimeongea haya yote ni kutokana na watu wengi, wapinzani na wana CCM kuonekana kumhukumu alie kuwa Rais wa Tanzania, J.P. Magufuli na hata kumzodoa kuwa kafa mapema, yako wapi, kuonesha tu Mungu ati kamuondoa kwa mabaya yake. Nilishangaa hata Mchungaji mmoja anajiita mzee wa upako kuongea kama vile nae anaonesha kufa kwa magufuli ni kama adhabu, eti kisa Lowasa hakuchaguliwa Urais na kuwataka watu wakamuombe Msamaha Lowasa.
Mimi niseme kwa maandiko viongozi wote wakuu wa nchi uwekwa na Mungu. Mungu angeamua Lowasa kuwa Rais angekuwa tu. Mchungaji kasahau maandiko anatumia akili za kibinadamu. Kufa kwa Magufuli si kwamba Mungu hakutaka Magufuli awe Rais, la asha. Mungu hutenda kwa wakati wake.
Jiulize katika maandiko tunaambiwa kuwa Yusufu aliuzwa utumwani na nduguze, bado huyo Yusufu akafungwa gerezani. Lakini cha ajabu akaja kuwa ndiye waziri mkuu wa nchi. Hata nduguze walipojihisi atalipiza kisasi kwa kuwafanyia mabaya, aliwaambia. Mlikusudia mabaya kwangu, lakini katika hayo mabaya Mungu alikusudia mema ili nije niwaokoe katika baa la njaa.
Mungu uona mbali zaid ya binadamu. hatujui ni kwanini Mungu aliepusha Lowasa asiwe Rais japo ilitumika njia mbaya au nzuri, lakini Mungu anakuwa na makusudi yake. Mchungaji katafakari neno la Mungu ndo utoe tamko. Hakuna lifanyikalo duniani bila Mungu kuridhia. Mungu huyo aliruhusu Ayubu apate mateso, akaruhusu watoto wake Ayubu kufa na hata mali kuharibika na kupotea lakini alikuwa na kusudi. Kifo cha Magufuli kinakusudi liwe baya au zuri ila watanzania tutajifunza kutokana na hicho kifo siku moja. Kikubwa tusijichukulie mamlaka ya kuhukumu na kusema kafa kwa sababu alikuwa katiri na kadharika. Mbona Mungu alimlinda Kaini japo alikuwa muuwaji?
Hivi kazi yetu ni kuhukumu, kwani tuliobaki hatutakufa? wangapi tumefiwa na ndugu na wazazi, je kutangulia kwao ni kwamba walitenda mabaya Mungu kawahukumu? Kwa uzoefu wa haraka tu mara nyingi watu wema hawadumu? Iwapo hadi sasa unaishi lazima ujiulize, unatakiwa kulifanyia nini Taifa lako la Tanzania, na familia yako. Si kushambulia marehemu, na kujifanya wewe ni mungu unahukumu. Leo hata viongozi wetu utasikia, oooh! Magufuli hakutenda haki, alikuwa kiongozi mbaya, alikuwa muuwaji, alitisha, hakuwa na demokrasia!
Hivi ninyi viongozi mnao sema haya si mlikuwa nae ktk uongozi wa serikali? Kwanini amkumwambia wakati huo akiwa hai kuwa ni kiongozi mbaya.
Nacho jua Magufuli alikubali kukosolewa. Naibu Waziri wa afya kipindi hicho alimkosoa kuhusu matumizi ya kujifukiza. Akamwondoa katika nafasi. Lakini baadae alimrejesha ktk wizara tofauti.
Leo wanao mkosoa magufuli haohao, wanapinga Mhe. Rais Samia kukosolewa. Wakati Rais alidai kuwepo uhuru wa kukosoa. Lakini chama chake na Bunge Wanataka asikosolewe, tumsifie hata kwa yale yasio sifiwa. Wakati wanadai wao ni wanademokrasia. Ukikosoa unahesabika msaliti, Bunge litakuita kwenye Kamati. Chama kitakaa kukuita kikuhoji kwa nini huko kinyume na Rais. Chama kinachoongozwa na mwenyekiti ambae ni Rais alie ruhusu kokosolewa.
Mungu hapendi wafitini na watu waongo, wenye roho za usaliti. Viongozi mjitafakari. Na msijione ninyi hamta kufa. Kifo kipo akijali madaraka yako. Hakuna atakae ishi milele. Kuwepo kwako pengine Mungu anataka utimize mambo fulani. Ghazabu ya Mungu ni kubwa tusihukumu tukaja hukumiwa. Magufuli kaondoka kamaliza yake. Alifanya kwa nafasi yake na kwa staili yake. Watu wote hatufanani.
Tusijione sisi ni bora kwakuwa tu watu wanatuchekea na kutusifia. Tukachekelea na kuota kiburi kuona tuko sahihi na hatukosei! Pamoja na yote Magufuli aliwapenda watanzania. Hakuwahi kusema waondoke wakaishi Burundi.
Leo kauli hiyo inaongewa na kiongozi aliepewa dhamana na watanzania. Viongozi wamejiona wako juu ya sheria, wanauwezo wa kusema chochote. Viongozi wamekuwa na dharau. Wanajiona nchi ni yao. Hata wananchi kulalamika hawaoni haja ya kuomba msamaha.
Hata kiongozi wa nchi hawakanyi anawaacha je naye kafurahishwa na hayo maneno? Je kawatuma?
Harafu hawa hawa ndo wanasema watakuwa wapole na kuwabembeleza wananchi kuliko JPM ambaye kapewa mabaya yote.
Tukumbuke kutangulia kufa si dhambi. Na ukibakia si ujanja wa kufanya kutukana waliotangulia. Bali chukua muda wa kujitafakari.
Mungu alimlinda Kaini japo alikuwa muuwaji wa nduguye. Mungu ndiye mwenye kuhukumu. Na ndiye ajuaye mwisho wa maisha yetu. Jiulize hapo ulipo matendo uyafanyao ktk vificho au wazi, je ni mema? Je wewe ni msafi zaidi ya waliotangulia kufa?
Je, wajua kifo chako kitakuwaje? Lini utakufa? Je utakufa ukiwa na umri gani? Je alie kutangulia kafa akiwa na miaka mingapi?
Si ujanja wala umaarufu kutukana marehemu, au kutafuta umaarufu ati unajilinganisha na marehemu. Huyo kesha maliza wakati wake hayupo tena. Tuache kashfa hatujui kesho yetu. Tanzania ya leo imekuwa na siasa za kujipendekeza, sifa za kijinga, badala ya kufikiria maendeleo ya kweli. Walio tangulia tuwaache, tujenge nchi.
Pote
Potelea mbali sijaiba Cha mtu sijauwa mtu sijateka mtu sijafunga watu kwa kesi za uongo sijaikufuru Wala kuinajisi altare ya Mungu naamini mungu muumba wangu atanipa kifo Cha amani na cha heshima.
Eti kifo Cha mwenzio isiwe kicheko kwako unakumbuka magufuli alikataza hata watu kumuombea lissu Yani alitufikisha viwango vya uadui wa juu Kama taifa kuvaa fulana za kumuombea lissu ikawa jinai kwenda hospital kumpa pole ikawa jinai khaaa baba yule hapana aisee na aendelee kuwa carbon.
Dah kweli Mungu Fundi...manake tuliteseka vya kutosha miaka mitano ya awamu ya JPM ...Asante Mungu kwa kuturudishia ubinadamu,amani na upendo
Before 2015 Tanzania ilikuwa Kwenye kundi la G20 siyo?Chama chakavu vs chama chakavu
Dodoki refuu la kumsafisha marehemu la nn?
Kama alitenda mabaya atahukumiwa kwa maovu yake haina haja ya dodoki la kumsafisha marehemu
2015-2021 UCHUMI WA NCHI ULIKUWA HATIANI SANA KAMA S MUNGU SIJUI INGEKUWAJE
Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
Sasa kama hukumu anatoa Mungu wew hizi hukumu za Wananchi zinakuuma nini? Kwanini usiangalie hiyo hukumu ya Mungu ambayo bado sana na kufanya mambo yako kuliko kuonekana hayawani hapa.Hukumu utolewa na Mungu, si Binadamu!
Mwenye matusi uwa namashaka na malezi aliyoyapata kwa wazazi wake, na udhihirisha namna asivyoelimika kwa upuuzi, na malezi yasiyofaa. Nzi ufuata harufu mbaya. Na inzi ukulia chooni! Na siku zote nzi akiona kinachonuka ufuata akijua ni choo. Hii utokana na malezi ya chooni kwa huyo nzi.
Jamaa bonge la hayawani, anasema msihukumu huku yeye anahukumu, yale yale ya msemakweli ni mpenzi wa Mungu, lakini alikuwa akiambiwa ukweli anapiga mtu shabaSasa mbona unahukumu. Mkuu huna ukomavu kiimani. Kaa utulie.
Umejuaje binadamu mwenye matusi imetokana na malezi ya wazazi wake? Kumbe hujui hata uliposimamia. Kama upo upande wa Imani kubali matusi mkuu
Ndio maana tunakuambia umezidiwa na mahaba mpaka sasa unakana hata maneno yako mwenyewe, mchelea mwana kulia hulia yeye, ndilo linalokukuta sasa, ulikuwa na wkati mzuri wa kumkumbusha mahaba wako huu uzi ulioweka leo hapa labda yeye angekusikia, kwa kuwa tulimuasa sana hapa kuwa aache visasi, hakusikia, mbona husemi kuwa kisasi ni Cha Mungu! Sisi hapa hatuhukumu bali tunakumbusha kuwa kama ilivyo wema kuwa ni mbegu ubaya nao ni mbegu lazima iote. Hata hukumbuki andiko juu ya kuikumbusha nyumba ya Yakobo dhambi zao!Unajiona unajua, wendawazimu ni kufanya jambo kwa staili ilele na kurudia yaleyale na kujiona unaakili! Kuna msemo usemao, baharini avumae ni papa lakini....! So usijione much know nakuleta lugha za dharau. Mtu mwelevu hata sikumoja ajisifii bali usifiwa!
Kuja na lugha za kujifanya unajua huo ni ulimbukeni na ushamba! jenga hoja acha kujifanya unadharau! Unajitutumua weee! pole sana!
Kuendelea kuelezea mapungufu ya mwenzako ni kuonesha kuwa uwezo wako ni mdogo. Ni kama vile mtu anabomboa nyumba ya jirani yake ambayo ni nzuri kuliko yake ili kuonesha yeye ana nyumba nzuri kuzidi mwezake. Mnashindwa nini kuhubiri mazuri yenu ili muonekaneMungu aliona hatma ya taifa na ndio maana aliingilia Kati ; trust me angeongoza miaka kumi Kuna watu uzalendo ungewashinda na uvumilivu ungeisha watu wangeanza kukinukisha live na damu nyingi ingemwagika magufuli alikuwa analipeleka taifa ukingoni mwa uvumilivu wa kawaida.
Ila hayupo sasa