Hayati Magufuli alidhibiti ukatwaji wa umeme au mazingira yalimbeba?

Hayati Magufuli alidhibiti ukatwaji wa umeme au mazingira yalimbeba?

Wewe dogo usinilinganishe na wenzio. Nenda uka click jina langu mwenyewe uone joining date yangu. Mimi nimeingia humu wakati wewe hata kuvaa boxer hujajua
Halafu unakuja kusema watu walikuwa hawamkosoi Magufuli humu et walikuwa wanaogopa!
 
Unajichanganya, waziri anasema umeme ulikuwa haukatiki sababu mitambo ilikuwa inalazimishwa kufanya kazi sana ndio sababu sasa hivi imechoka. Wewe unasema ulikuwa unakatika. Waziri ni muongo?
Huyo linapokuja suala la Magufuli anaweza kuongea lolote lile.
 
Huyo linapokuja suala la Magufuli anaweza kuongea lolote lile.
20230302_103040.jpg

Akiwagawia mapapai namna hii ndiyo wajinga mlikuwa mnamuona mtetezi wa wanyonge. Papai tu?? Nimewadharau sana watu wanaoitwa wanyonge
 
Hakuogopwa bali alikuwa katili!!

Watu katili kila siku hufurahi kutisha wengine na wao kutamani kuabudiwa na kila mtu.
Alikuwa katili Kwa watu ovyoovyo Kama wenye vyeti feki,wanasiasa ovyo ndo Sababu alipendwa na watanzania na wasio watanzania.kama wewe ni Kati ya hao watu ovyo Sawa.
 
Watu wa ovyo kama wanasiasa ovyo kama lisu,vyeti feki na wapiga dili lazima mchukie Magu.
Vyeti feki siyo issue kwa kuwa hata Magufuli alikuwa na PhD feki. Na Makonda naye alikuwa na cheti feki kwa kuwa jina lake ni Daud Bashite
 
Alikuwa katili Kwa watu ovyoovyo Kama wenye vyeti feki,wanasiasa ovyo ndo Sababu alipendwa na watanzania na wasio watanzania.kama wewe ni Kati ya hao watu ovyo Sawa.
Alipendwa na Watanzania wajinga tu kama wewe
 
TANESCO walikuwa wanajilazimisha ila waliua ma transformer mengi mno kwa kulazimisha kumfurahisha mwamba ili asitumbue mtu.
Nyingi ziliungua ila umeme ulikuwa haukatiki haya maajabu.
 
Hapana hii ni taarifa ya kitambo sana na iko kisayansi zaidi hata kama anayeitoa humpendi. Miundo mbinu ya kusambaza umeme kwa nchi yetu imechakaa na inahitaji ukarabati.

Kumbuka pia ongezeko la matumizi ya umeme vijijini kutokana na mradi wa REA pia yanaongeza mahitaji kwenye miundo mbinu yetu ya kusambazia umeme!.
Umeme unavuja duuu,eti taarifa za kitalaam, wataalaam wanawatizama wanacheka, watawadanganya nyinyi msiojua,

Uwe na uwezo wa kusambaza umeme kwa miaka zaidi ya mitano bila PM,mnapendwa kudanganywa,hako kajenereta tu ukiendesha kwa miezi hata sita bila kukifanyia PM hakiwaki.
 
Acheni kuabudu shetani. Hata wakati wa dikteta Magufuli umeme ulikuwa unakatika. Tofauti pekee ni uwazi wa taarifa. Hata wewe Allen Kilewella kipindi cha dikteta usingeweza kuandika kitu kinahusu udhaifu wa serikali yake
Kwama umeme ukikatika unahitaji uambiwe umekatika au
 
View attachment 2547827
Akiwagawia mapapai namna hii ndiyo wajinga mlikuwa mnamuona mtetezi wa wanyonge. Papai tu?? Nimewadharau sana watu wanaoitwa wanyonge
Ni mtazamo wako kama hivyo ndivyo unavyoona wewe basi sawa ila hata Samia anagawa hela kwa simba na yanga ila hao wanyonge hawajamuona kuwa ni mtetezi wao.
 
Ni mtazamo wako kama hivyo ndivyo unavyoona wewe basi sawa ila hata Samia anagawa hela kwa simba na yanga ila hao wanyonge hawajamuona kuwa ni mtetezi wao.
Wacha kumlinganisha Mama yetu na Shetani aliyekuwa anataka masifa ya kishamba!!
 
Vyanzo vya maji kwa ajili ya Mabwawa makubwa matatu ya kuzalishia umeme, yaani Bwawa la Mtera, Kidatu, na Kihanzi, vyote kwa asilimia tisini (90%) vinategemena na sehemu kubwa vinatokana na vyanzo vile vile. Kwa mfano sehemu kubwa ya maji yanayojaza bwawa la Mtera na Kidatu chanzo chake ni kile kile.

Kwa miaka miwili mfululizo kumekuwa na ukame mkubwa sana kwenye maeneo yanayotoa maji kwa ajili ya mabwawa ya Mtera na Kidatu. Wiki hii nilikuwa Mtera na kwa kweli hali ni mbaya sana kiasi kwamba inawezekana upungufu wa maji mtera umeweka historia kwa miaka ya hivi karibuni.

Sasa kama sehemu kubwa ya umeme wetu tunategemea umeme unaozalishwa kwa maji, na ukame ndiyo huu umeshika kasi, tunategemea muujuzi gani utakaotuzalishia umeme?

Enzi za Magufuli kulikuwa hakuna mgao mkubwa wa umeme, lakini jee pia kulikuwa kuna ukame kama ulioko sasa? Mara hii tumeshasahau ni kwa nini Enzi za Kikwete wafugaji walihamishwa toka hifadhi ya bonde oevu Ihefu?
Hakuna alichofaulu
 
Back
Top Bottom