Hayati Magufuli alikosea kwenye mambo mengi mno. Kubwa mojawapo ni kumchagua huyu mtu

Umesema ukweli kabisa hujabakiza hata moja.huyu alichaguliwa ili kubalance muungano na jinsia na siyo vinginevyo.bahati mbaya magufuli kafariki katuachia mzigo mzito wa misumari kichwani.katiba ibadilishwe hawa warithi watawale mwaka mmoja ili kuzuia hasara kubwa itakayofanywa na wao kama haya ya kuuza mali za tanganyika na kuacha za nyumbani kwao zanzibar
 

Vipi kuhusu JK kuusaka urais?
 
Wamachinga hawawezi kuigeuza Tanzania nzima kama sehemu ya kufanyia biashara, hawapo peke yao na haitatokea wakawepo wao tu wa kusikilizwa kwa kisingizio cha unyonge.

Huo unyonge ni lugha ya hayati JPM ni lugha ya ulaghai unaowadanganya wafanya biashara wadogo kiasi cha siku zote kujiona wao ni wadogo tu. Mentality ya kijamaa ya kudumaza akili.

Maasai wametoka Loliondo wamekwenda huko Tanga mahali wanapojinafasi pengine kuliko walivyoishi huko Arusha.

Waliomshauri atafute mwekezaji wa bandarini ni ndugu zetu wafanyabiashara waliochoshwa na magumashi ya mahali pale, waliochoshwa na wizi usiokwisha wa bidhaa zetu.

Waliomshauri awatafute DP ni wadau wa bandarini watu ambao maoni yao ni ya muhimu kuliko hizi kelele nyingi za mtaani kutoka kwa watu wasiojua A wala B kuhusu biashara kwa maana pana.

Kwa akili zetu za kitanzania hakuna rais mwenye afadhali siku zote ni kulialia tu.
 
Unachangia mada ipi maana nineona ghafla bin vuu umemtaja musa Hassad
 
Hilo mi mwenyewe sijawai kukubali kuwa tuna rahisi namna hii.
Jiwe kabla hatujategemea kilichotokea hatukujiandaa.
Ila hatuna kiongozi.
Bora Majaliwa huyo mwingine ndo kabisa anatakiwa akae ofisini tu afanye kazi zingine
 
Naona unakuja vizuri sasa😂😂 kama machinga wana makosa ndo mpaka waharibiwe mali zao? Je kama wana makosa hao wafanyabiashara unaosema waliumizwa kipindi cha jpm hawawezi kuwa na makosa?
Bajeti ya kuwahamisha Masai ilitengwa na bunge gani na ni fungu gani? Kama hakuna je hiyo sio rushwa kutaka kwa waarabu? Unasema walipohamishiwa wanajinafasi je waliwahi kulalamika kwamba walipokuwa palikuwa hapawatoshi? Na kwa nini muwatoe mumpe mwarabu? Na mbona mliwaua na kuwabambikizia kesi ya mauaji waliogoma kuhamishwa?
Kwenye bandari alishauriwa na wafanya biashara gani kwenye kikao gani? Na kama walimshauri jambo kama hilo walimshauri awachague DPW? Je walimshauri awachague bila kufata mchakato wa sheria ya manunuzi ya umma? Kama sheria ya manunuzi ya umma ilifatwa je mwarabu alishindanishwa na nani moaka akashinda yeye? Kama alishindanishwa je tangazo lilitolewa kwenye gazeti gani au tovuti gani? Je hao wafanyabiashara walimshauri aingie mkataba tata na usio na maslahi kwa taifa kama huu? Mkataba wa upande mmoja kuwa na haki tu (upande wa mwekezaji) na upande mwingine kuwa na wajibu tu (upande wa Tanzania) je kama alikubali ushauri wa wafanya biashara kuingia mkataba kama huu huoni unakubali japo kwa maneno tofauti hoja ya mtoa mada kwamba kama nchi tumepigwa na kitu kizito kwenye utosi linapokuja suala la namba moja?
 
Mengi unayouliza yameshajibiwa rasmi na serikali, tafuta taarifa hizo kwani zimo humu mitandaoni.

Hizi nongwa zote ulizoziandika zimeshatolewa maelezo rasmi, tusitake kuumizana vichwa bila ya sababu.

Samia anaweza kuwa mwepesi lakini hayati JPM alikuwa na udhaifu wake tena mwingi tu.
 
Kupigwa na vitu vizito hatukuanza leo wala jana, ni miaka na miaka, Na wakati mwingine tunapigwa kwa ujinga wetu wenyewe kama taifa.
 
Hakumchagua yeye, bali chama, aliwahi sema hata mimi niliiona hiyo taarifa live na akasema bila kuwa mwañamke mimi nilikuwa namhitaji, Mh Hussein Mwinyi.
 
Kupigwa na vitu vizito hatukuanza leo wala jana, ni miaka na miaka, Na wakati mwingine tunapigwa kwa ujinga wetu wenyewe kama taifa.
My point is Magufuli alikosea kutupa makamu ambaye sasa ni rais wa hivi. Kwa hilo nitamlaumu yeye na chama cha mapinduzi. Walikuwa na nafasi ya kutupatia mgombea mwenza bora na sasa tungekuwa na rais bora ila ona yanayolikuta taifa sasa
 
Amebaki kununua magoli ya yanga na simba ,hiyo ndo kazi anyoimudu kww 90%
 
My point is Magufuli alikosea kutupa makamu ambaye sasa ni rais wa hivi. Kwa hilo nitamlaumu yeye na chama cha mapinduzi. Walikuwa na nafasi ya kutupatia mgombea mwenza bora na sasa tungekuwa na rais bora ila ona yanayolikuta taifa sasa
Wapo wengi wanaomuona bora sana kumbuka hata slogan ya KAZI IENDELEE ni muendelezo wa kile alichokianzia hayati JPM

Hawa wakurugenzi nyeti kina Hamza, Kadogosa ni wale wale wa hayati JPM, na miradi yote anakwenda kuimaliza mmoja baada ya mwingine.

Hakuna rais atakayependwa na kila mtu, hayupo duniani pote.
 
Kwa Samia sikupingi mkuu ila hapo kwa Biden alivyokuwa anamfanyia hivyo huyo dogo Kuna shida gani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…