Mtu huyo ni Rais Samia!
Nashawishika kabisa kuamini kuwa huyu Samia alichaguliwa kutokana na jinsia yake tu [kama ilivyojuwa kwa Kamala Harris…the word salad queen…kule Marekani].
Kamala yeye alichaguliwa na Biden kuwa mgombea mwenza kwa sababu ni mwanamke mweusi [ingawa kiuhalisia ni chotara wa Kihindi na Kijamaica].
Kamala ni mweupe kabisa. Yaani hovyo to the nth degree. Anaongeaga mashudu tu [word salads].
Hana kabisa uwezo wa kuongoza. Yeye ni kucheka cheka tu na kuongea mambo yasiyoeleweka.
Ukimwangalia Biden, unaona kabisa jamaa anapaswa awe nyumbani. Kazi ya urais wa Marekani kwa sasa haiwezi.
He is a creepy old guy. Hebu angalia hapa
Hivi alikuwa anafanya nini hapo kwa hako katoto? Na hiyo ni wiki iliyopita alipokuwa Finland baada ya kutoka Lithuania kwenye mkutano wa NATO.
Biden muda wowote anaondoka. Iwe kwa kujiuzulu, kuamua kutogombea tena muhula wa pili, au hata kufa [ingawa kifo hakina mwenyewe].
Wazo la Kamala kuja kuwa Rais wa Marekani endapo Biden ataondoka, linatisha watu wengi sana.
Haya, tuje kwa huyu wa kwetu hapa.
Huyu naye alichaguliwa kwa sababu ya identity politics tu. Ni mwanamke na ni Mzanzibari.
Kwa ninayoyaona, ni mtu asiye na uwezo wa kiuongozi ngazi ya Rais wa nchi.
Hakuchaguliwa kutokana na sifa zake za kiuongozi.
Inavyoonekana Magufuli alikuwa anataka sifa ya kuwa na mgombea wa kwanza wa CCM kumchagua mwanamke kuwa mgombea mwenza wake.
Haiwezekani kabisa kuwa Samia alichaguliwa kutokana na sifa zake kiutendaji [kwa sababu hana].
Jahazi limeshamshinda hivi sasa. Kabaki kutoa vitisho na kutumia dola kukabiliana na wanaompinga.
Na ukiongeza na inferiority complex aliyonayo kutokana na jinsia yake, ndo kabisa anakuwa paranoid kwamba kila anayempinga, anafanya hivyo kwa kusukumwa na chuki dhidi yake kwa sababu yeye ni mwanamke!
Rais Magufuli hakuwa kiongozi mzuri. Nilishasema mara nyingi tu kuwa yeye alikuwa msimamizi/ mnyapara mzuri.
Yeye mpe kazi au mradi ausimamie, halafu umpe mamlaka ya kutosha kuweza kufanya maamuzi ndani ya ukomo fulani, utampenda maana hakuwa wa mchezo mchezo.
Sidhani kabisa kuwa Magufuli aliwaza kuhusu yeye kuishia njiani na kumwacha Samia ndo awe Rais.
Nadhani alidhani kuwa atamaliza vipindi vyote viwili na kustaafu kama walivyofanya waliomtangulia.
Lakini haikuwa hivyo. Tumeachiwa huyu Samia.
Makamu wa Rais, Dkt. Mpango, kwa mtazamo wangu, ni bora mara 100 kuliko Samia [I got bars too 😀].
asante sana kwa kuonyesha hisia zako juu ya Raisi Samiha Suluhu.
Kwa kweli Magu hakumpenda kabisa Mama lakini kama imeandikwa kuwa, litakuwa tu. Magu aliwatukana wapemba hadi mama akakasirika. Akamjibu Magu. Magu akarusha kofi, yule body guard wa mama akaushika mkono wa Magu kabla kufika usoni. Magu alishituka sana. Usalama wa taifa wakamchukuwa Magu kando na kumpumzisha. Yule binti bado yupo na mama na ndio mlinzi wake namba moja. Baada ya kisa hicho, wazee wastaafu (ALI H MWINYI) wakaingiliya kati. Na ndipo mahusiano yakazidi kuwa tete. Viongozi wenu waliokuwepo zanzibar waliiba Dola millioni 75 za mtoto wa mfalme wa Qatar.
Magu alikuja akakaa siku tatu anaongea na watu wake namna gani fedha zimepotea. Walikula Dr. Shein na watoto wake, Sefu Ali Iddi(mkongo), na makada kadha waCCM. Baada ya hapo, Haji kheri amejenga hoteli kumi na moja za kitalii. Wote hawa ni wapenzi wa Magu hatujui katika wizi huu na mahoteli haya , share ya Magu ni kiasi gani.
Paul Makonda alikuwa akitumiwa kufanya kazi ya bwana mkubwa mpaka siku alipogusa sehemu isioguswa, uhusiano ukapunguwa. Kweli ukiwa hutaki kufuata amri ya Bwana Magu utakuwa mbaya. Makonda alikuja zanzibar baada ya wafanya biashara wawili kutuhumiwa kuiba madini. Basi katika makubaliano, alitumwa Makonda kuja zanzibar kuchukuwa dola zaidi ya elfu ishirini. Hiyo ndio hukumu ya MAGU.
Kama ni wizi , makada wote wa CCM ni wezi.
Mama hakukubaliana na mambo mengine ya Magu ndio maana akawa mbaya. Wizi wa maduka ya dhahabu, forex kufungiwaetc etc zote wakati wa Magu. Mimi nawashangaa sana wanao msifia Magu kuwa kaleta maendeleo. Mikataba aliyositisha imetugharimu mara kadhaa kwa kuwa hakutumia ujasiri.
Kiburi cha Magu kilipita mipaka. Halafu, kama sisi wazenji tumsifu Magu kwa kitu gani wakati alituletea jeshi kutuuwa wakati wa kupiga kura. Hadi leo wameshindwa hata kuomba samahani kwa vitendo vyao. Mwinyi ambae yupo pale kwa nguvu za Maguhawezi hata kupata 5% ya kura za wazenji ndio wakauwa watu ovyo.
Sisi tuna kitu gani kizuri cha kumsemea MAGU na HUSSEIN wake?. Mama ameonyesha ujasiri na uungwana kututuoa kwenye mkwamo..