Inaonekana ni kweli, ndio maana Sabaya licha ya kurekodiwa na camera akivamia maeneo ya watu na silaha mkononi, lakini hakuwahi kuwa na hofu yoyote na hilo.
Hili linathibitisha kweli alikuwa anatumwa akijua ana ulinzi wa kutosha upande wake, ndio maana siku ya kumuaga Magufuli jamaa alilia kama mtoto akijua fika mwisho wake umewadia.
Lakini pia hili linazidi kuthibitisha yale madai kuwa utawala wa Magufuli ulikuwa unaichukia mikoa ya Arusha na Kilimanjaro, huu unyama uliokuwa unafanywa na Sabaya, akitanguliwa na Mnyeti mikoa hiyo, haukuwahi kuonekana ukifanywa mikoa mingine Tanzania.