Kwa vipimo vyote magufuli alikuwa kiongozi mbaya ila kwakuwa Watanzania ni watu wenye upeo mdogo aliwa win mioyo yao.
Magufuli alihakikisha mifumo yote ya good governance anai paralyze au kuiuwa kabisa ili yeye ndio awe sheria alisahau kwamba binadamu hupita ila continuity ya taifa inategemea mifumo imara na sio mtu imara.
Watu huja na kupita ila mifumo hubaki kwa muda mrefu. Stability ya taifa hutegemea mifumo sio mtu.
Magufuli alihakikisha bunge linakuwa mfukoni mwake na ndio maana alidiriki kununua wapinzani na kuvuruga uchaguzi wa 2019 na 2020.
Kwakuwa watanzania wengi wana upeo na uelewa mdogo walimpongeza kwa vile waliona akiwajengea miundombinu mizuri na kwa bahati nzuri watanzania ni watu wa kuridhika haraka na kwa vitu vidogovidogo.
Wanasahau kwamba popote penye utawala bora au good governance kwa kizungu hayo yote ya barabara madaraja stendi masoko ya kisasa huja automatically.
Kwahiyo Magufuli alitumia ujinga wa watanzania kuwarubuni na wao qakarubunika. Magufuli alikuwa anajinasibu kuwa mtetezi wa wanyonge huku akigawa hela barabarani na kukaa chini ili wananchi wamshangae wampende kumbe ule ni utapeli wa kisiasa angeishi hata mwaka mmoja taifa lingeangamia.
Hii ni kulingana na mtzamo wako tu,
Maybe katika maamuzi magumu ulikutwa na ukajenga chuki moyoni mwako.
Ila kuna shahidi mbalimbali kama ulivyosema wewe, Magufuli aliwini mioyo ya hao unaowaponda kuwa wanaupeo mdogo.
Kumbe nchi yetu hii ina percentage kubwa ya wenye upeo mdogo kiasi hiki. Hii ni ajabu, ila kheri yako wewe unaupeo mkubwa sana.
Unaposema kuwa aliua utawala bora, means mwanzoni kabla yake utawala bora ulikuwepo.
Wanasahau kwamba popote penye utawala bora au good governance kwa kizungu hayo yote ya barabara madaraja stendi masoko ya kisasa huja automatically.
Je hayo mambo madogo kwa wenye upeo mdogo kama tuflyover, tusoko twa kisasa, tudaraja na tubarabara kipind hicho mwanzoni tulishindwa vipi kuwepo?.
Huoni hata kasi yake ya kutujenga huto tujitu tunampa credit mwendazake?
Alivyotackle lile janga la corona na kuihandle pressur, napo huoni kuwa alituwini sisi wenye upeo mdogo..
Wenye upeo mdogo wanakila sababu ya kukamatwa na mwendazake.
Wewe na utawala bora uliopo mmefanya nini zaidi ya lawama tu kila siku, mara migao ya maji, umeme, bei za vitu vinapanda tu, mnarudisha corona redioni..
Dharau ofisi za umma.. Na saizi wenye upeo mdogo mmeshindwa hata kuwajibu kuhusu bandari ili wasiwe na hofu na nchi yao... Ninyi hamjali kisa mnamamlaka.
Muacheni Magufuli, wewe unapambana hadi na marehemu hadi leo?