Hayati Magufuli alikuwa na uelewa mdogo wa masuala ya dini, asilaumiwe

Huko pengine sina Uelewa Napo Sana

Ila kwenye dini Mara nyingi alikuwa akipotosha.

Viongozi wote wa dini waliozidisha unafiki waondolewe.

Kuna yule Mufti aliyesema Bwana Yesu asifiwe sijui Kwa nini Waislam hawamuondoi.
Nimeishia hapa kusoma comments,

Hapa kidogo umetoka nje ya mada yako nzuri, Kwa mtazamo wangu.
 


Hii mada yako ingekuwa na maana sana kama ungalidadavua ni kitu gani Magufuli angefanya katika kadhia nzima ya Corona kwani Wote tunao amini Mungu na dini tunajua kwamba Mungu anayo nafasi kubwa katika kila nyanja ya Maisha yetu na ni kutokana na jambo hilo ndipo Magufuli alitutaka tumtegemee Mungu zaidi, Suala ni; kwa namna gani na wakati upi Mungu ategemewe.

Magufuli alikuwa sahihi kwa kiwango fulani na hakuwa sahihi kwa kiwango fulani, tumsimlaumu moja kwa moja katika jambo hili.
 
Mkuu andiko lako nimelipenda.
umeandika ambavyo ninataka kuandika. Asante.
 

Magufuli hawezi laumiwa na watu waliokuwa wanajua kuwa Hana Uelewa na mambo ya Kidini anayoyazungumzia.

Watakaomlaumu ni Wale wanaomuona Kama mjuvi WA kila kitu.

Magufuli makosa yake ni kumuona Mungu Kama mwenye wajibu wa maisha ya binadamu Kwa 100% Jambo ambalo sio kweli.

Mungu ananafasi yake katika maisha ya wanadamu, Ila Kwa kiasi kidogo kabisa cha lazima.

Makosa ya JPM ni kuchochea mara kadhaa na kuwadhihaki viongozi wa dini waliokuwa wakivaa Barakoa Kwa kuwaona hawana Imani, yaani hawamuamini Mungu.

Jambo ambalo halikuwa Sahihi.

Magufuli alichokuwa hajui ni kuwa kumuamini Mungu ni kufanya wajibu wetu Kama Wanadamu Kwa kufuata taratibu sahihi za Nyanja za kimaisha

Huwezi Muamini Mungu Kwa mdomo au kumuomba au kusali.

Mungu anaaminiwa Kwa wajibu wa matendo, kwani matendo ndio Imani.
 
Asilaumiwe, kwani Hakuwa na Uelewa wowote wa mambo ya Kidini

Muhimu wafuasi wake waelimishwe tuu, waambiwe waliyemuamini Hakuwa na uelewe
Unasema asilaumiwe? Kama huna uelewa wa jambo fulani, lakini ukajifanya wewe ni bingwa, na wale wataalam waliopaswa kukuongoza uelewe zaidi ukawapuuza, utaacha kulaumiwa? I mean kwa nini alikuwa anawaponda viongozi wa dini wakati wao ndiyo wenye elimu ya dini kuliko yeye? Punguza kuwa diplomatic kwenye hoja yako.
 
nimeamini itachukua miaka 50 ya kizazi hiki kumtaja magufuli.iwe kwa wema au mabaya.
Ni kweli atatajwa kwa miaka mingi maana amefanya mabaya mengi. Hitler na Musolin wana zaidi ya miaka 50 tangu watoke duniani lakini mpaka Leo wako midomoni mwa watu kuliko Mama Theresa.
 
Nimekuelewa sana, kifupi alikuwa ni mpagani wa kikristo
 
Aliamini PHD yake ya mafuta ya korosho, tena ya kupewa ingeweza kumfanya ajue kila kitu, tatizo ushambaa.
 

Asamehewe Kwa maana hakujua atendalo
 
Magufuli na Mungu wapi na wapi. Angekuwa anamjua Mungu asingeua watu wala kuwashikilia watu milioni 60 mateka kwa miaka mitano yote. Huyo alikuwa ni wakala wa shetani kabisa.
 
Rais Magufuli alijitofautisha sana na Marais waliopita naamini ata kwa wanaokuja, Nisime Rais Magufuli alitumia 90% ya ubongo wake kuamua masuala ya kitaifa kuliko Marais wengine. Rais Magufuli hakuwa mtu wa kumpelekea karatasi asome na asaini hapana! Alikuwa mtu anaesoma asopopata majibu yakulidhisha alikuwa anatafuta majibu kwa njia zake.

Kuhusu issue ya Corona sioni sehemu yoyote yakumlumu cos angekuwa amekosea basi 60% ya wananchi wa ili Taifa tungekuwa hatuko Duniani, Ugonjwa wa Corona ni ugonjwa uliombatana na propaganda na ndiyo maana alipiga stop farmigation kuwa haiui kirusi lakini wakati anasema mkamtungia mpaka wimbo kumcheka kupitia wakina Roma mpaka WHO walipokuja kisema kuwa kweli farmigation hakiui kirusi cha Covid, alikataa Lockdown ata barakao alisisitiza kama kuvaa vaa uliyotengeneza hapa nchini. Leo ukiniambia Rais Magufuli alifail kwenye issue ya Covid nitakuomba unipe ulinganifu nani alifauru zaidi yake?

World Bank juzi amewahakikishia bara la Ulaya muwa atahakikisha kufikia 60% ya waafrika watakuwa wamepata chanjo ya Covid, Rais magufuli hakukataa kabisa chanjo ila alisema lazima tujilidhishe hipi ni sahihi kwetu! Sio mtu analeta chanjo huku anakupa mkopo alafu anakuambia kama unataka hii hela lazima uchukue chanjo ya Covid..! Na ndiyo maana ata ilani ya chama 2020-2025 iliona ielekeze serikali kutenga bajeti ya kutosha kwaajili ya utafiti NIMR.

Hayati Rais Magufuli alikuwa akituambia wazi tuendelee kuchapa kazi ila tujifukize, tungwe tangawizi ikibidi na mazoezi na kweli mi binafsi nilipata hicho kitu kinaitwa Covid wimbi la kwanza na niliponea kwa Tangawizi na malimao + kitunguu swaumu na sikuwai kulala ata siku moja eti nisiende kibaruani
 
Uwe makini ulikohuko ,wepesi sana wakuolewa Mali ukinunua kitanda kwajili yawakwe habari imeisha
 
Mungu ananafasi yake katika maisha ya wanadamu, Ila Kwa kiasi kidogo kabisa cha lazima.


Hebu fafanua hapa.


Kosa la Magufuli ni kutokujua Mungu anategemewa na Mtu kwa namna gani, katika mazingira gani na wakati gani.---- hilo ndilo kosa lake, juu ya yote mtu katika kila hali lazima amtegemee Mungu hivyo Magufuli alikuwa na maono sahihi ila hakuwa sahihi katika njia ya kufikia hayo maono yake.

That is to say; a good intention in a wrong way.
 
Askofu Mkuu wa Jimbo la Darces Salaam Yuda-Thadei Ruwa'ichi aliimiza waumini wavae barakoa Mwendazake akaenda St . Peter akasema hana imani , yalikuwa mambo ya ajabu sana kushindana na kiongozi wake wa kiroho Mwendazake alijifanya yeye ni kila kitu hakimu yeye, jaji. spika, mwanasheria mkuu, dpp kila kitu alikuwa yeye, mbaya zaidi akatundanganya hata papai lina corona
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…