Hayati Magufuli alikuwa Rais mwovu, Samia Suluhu ni Rais dhaifu. Binafsi heri Rais dhaifu kuliko mwovu

So OCD wilaya ya kaliua ni dhaifu eeh?🤣🤣🤣hapana yule ni mwamba manake wilaya yake Ina misitu na kutosha kuchochea uhalifu,ila anapambana Sana,umemwonea bana🤣🤣🤣
 
Kwaiyo ili tusonge tunahitaji rais wa kaliba gani?

In my opinion tunahitaji Rais mwenye combination hizi

1. 20% Nyerere- Visionary
2. 20% Mwinyi- Accomodative
3. 20% Mkapa- Planner
4. 20% Jakaya- Diplomatic
5. 20% Magufuli- Executor
6. 0% Samia- Laxer ( hili nalo mkalitazame…)

Ufafanuzi

Visionary- Bado nchi iko nyuma kimaendeleo na Dunia inaenda kasi sana hivyo Raisi ni lazima awe na maono ya mbali ili tuyafanyayo sasa yawe na tija na relevant mbeleni na hasa katika uwekezaji katika miundo mbinu, technologia na Elimu kwa vijana! Kuendelea kuweka misingi ya kujitegemea kila maeneo na hasa kiuchumi na utamaduni

Accomodative- Nchi yetu ina watu wa caliber mbalimbali hivyo Raisi ni lazima aweze ku balance wasaidizi wake kutoka maeneo na taaluma mbalimbali, kuliko ku recycle [emoji3534] mijitu ileile hata inapoharibu. Pasiwe na manung’uniko kwamba jamii fulani immeachwa. Uwepo Uhuru wa kutosha wa watu kufanya biashara na pia demokrasia itamalaki.

Planner- Nchi bado inahitaji ku re-enforce institutional and legal frameworks ili kuweza kuhakikisha taasisi za uma zinauwezo wa kuakisi matarajio ya watu na hasa wawekezaji bila usumbufu na uchelevu usio lazima. Sheria ziwe up to date hasa katika mikataba ya nje ku safeguard national interests. Institutions ziwe na mifumo inayosomana ilikubaini dosari au forgeries kwa haraka kuepuka hasara na uvujaji wa mapato ya serikali. Adhabu kali sana kwa wakosaji kwa mujibu wa sheria kama China [emoji630] zitungwe

Diplomatic- Our country is not living in isolation hivyo Raisi ni lazima awe mwana diplomasia ili kuweza kuimarisha mashirikiano na nchi rafiki na majirani pia jumuia za kikanda. Hapo kuna fursa za kibiashara, mabadirishano ya uzoefu katika Nyanja mbalimbali kama technology, agriculture, fisheries, military….pia misaada pale inapo lazima.

Executor- Raisi ni lazima awe mfuatiliaji wa utendaji wa serikali yake maana uzoefu unaonesha watanzania wengi hasa serikalini bila “viboko” hawaendi! Aweke SMART KPIs kwa kila wizara na waziri husika na idara na kurugenzi husika kama Raisi Kagame wa Rwanda.

Laxer- Raisi asiwe mtu wa mipasho na wa “ Hili nalo mkalitazame”

Kufanikisha haya Raisi ashauriwe vizuri na kupanga timu sahihi itakayo tekeleza majukumu kwa uzalendo wa kweli ! Hawa watendaji wake Ndio wakamilishe ile gap ya 80% kwa maana penye wengi hapaharibiki neno midhali wengi hao ni wakweli na wazalendo. HAPO NDIPO TUTAKAPOONA MAENDELEO

MIHIMILI YA BUNGE NA MAHAKAMA IWE TRULY INDEPENDENT! NA IIDHIBITI SERIKALI NA KUISHAURI IPASAVYO

TAASISI KAMA TAKUKURU NA MDHIBITI NA MKAGUZI MKUU WA HESABU ZA SERIKALI NI MUHIMU SANA REPORT ZAO KUFANYIWA KAZI ILI KULETA NIDHAMU KWA WATENDAJI SERIKALINI

Hayo maoni yangu
 
Kumbe ndio maana kuna kipindi wale wanawake vikongwe wenye macho mekundu kanda ya ziwa walikuwa wanauwawa tu bila nafasi ya kujitetea!
 
Samia sio dhaifu na pia hana ushamba wa uongozi. Hataki kutumia madaraka yake makubwa kufanya maamuzi yanayoumiza watu kwa kipindi kirefu.
ta
Nyerere aliamuru tumpige Idi Amini ile vita ikaingiza nchi katika umaskini kwa miaka mingi iliyofuata.

Hayo ndio madaraka ya rais usipokuwa na busara wala hekima utaumiza wengi na kuingia katika dhambi kwa kigezo cha kupambana na rushwa.

Kutowataja wezi haina maana TAKUKURU haiwashughuliki kwa sasa, masuala haya yanajumuisha sheria huwezi kukurupuka kutenda ili fulani na fulani wakauone eti unafanya kazi vizuri.
 
Ni bora mpaka pale huo uovu utakapokugusa na wewe au mtu wako wa karibu ndipo utaelewa uzito na ubaya wake.
Kwangu mimi bora mwovu mwenye focus ya uovu wake na sio dhaifu
 
Sasa mbona hueleweki, unamtaka Samia ama Magufuli?
 
Mfumo dume unatesa akili yako. Tazama miradi yote aliyoiacha marehemu JPM namna inavyomalizwa mmoja baada ya mwingine.
 
Magufuli alilea kikundi cha wahuni kiliweza kumuua au kumteka yeyote anaemkosoa magufuli kiufupi ile serikali ilikuwa ya kuzimu,,Samia mpenda watu ila ni dhaifu mpaka anatia wasiwasi anawaogopa mpaka watumishi wa halmashauri sijui karogwa!!

Anawaogopa mpaka kina nani ? [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kiongozi mwovu hawezi kuleta maendeleo, ukisema JPM alikuwa mwovu unajikanyaga, hujui usemalo. Kaa chini uelimishwe alichofanya JPM.
 
Porojo hizi dhaifu ni dhaifu tu, alikuwa dhaifu mkwere sembuse mpemba
 
Samia Suuhu ndo nini?
Rais anaitwa Samia Suluhu Hassan.
Simple majina yetu haya kinyumbani kabisa.
Unasema suuhu km huna meno, au keyboard yako haina meno?
Hivi nani aliwafikisha kwenye forum GT watu km nyinyi

[emoji23][emoji23][emoji1787][emoji1787]
 
1.5T toka Tanzania iumbwe hakuna upotevu mkubwa wa pesa kiasi hiko. Yet unasema hilo tu na kupotea pesa sio jambo geni nchini zimepotea mno ila unfortunately kwa 1.5T aliyetueleza upotevu ndio kawajibishwa. Na sababu ya kuwajibishwa ni kuumbua uozo wa the so called Serikali Makini.

Nakubaliana na wewe tuikemee serikali maana tunapigwa mno.
 
Kujiuzia mgodi wa serikali kwa Bei ya kutupa kwa familia yake. Iwe kukiuka maadili na sio wizi inakuaje? Kwani wizi sio kukiuka maadili? Hivi kashfa za EOTF ya mkewe kujimilikisha Mali za serikali inabaki kuwa kukiuka maadili na sio wizi? Labda unipe tofauti ya wizi na kukiuka maadili!! Halafu labda hujui kuhusu IPTL hii ni kampuni iliyoundwa kwa mkataba wa kifisadi na TANESCO Na Wala haikuwa kipindi Cha kikwete
Halafu wizi kujulikana kipindi Cha kikwete hakuondoi ukweli kuwa ulifanyika kipindi chake

Makampuni hewa yote yaliyochukua hela za EPA ilikuwa kipindi chake Sasa sijui hulijui hilo au ndio utetezi usio na mantiki
 
Mkuu umemaliza kila kitu na naunga mkono.

Kweli tunaweza kupata wenye kaliba hiyo aliyekamilika kila kitu, na je kama hatuna mwenye kaliba yote ulizotaja, atleast awe vipi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…