Hayati Magufuli alikuwa 'system disruptor', kwa bahati mbaya hakuimaliza kazi, kwa sasa hakuna tumaini tena

Kama kutakua na nia ya kweli kujenga mfumo mpya kiutawala na mustakabali mzm wa maendeleo ya Taifa alipaswa kujenga taasisi imara kupitia katiba mpya!! Na sio kupitia individual.
Tujiulize kwanza ni kwanini Jk alishindwa kutupatia hiyo katiba mpya ??

Je ni yeye ndo alikuwa haitaki au ni mfumo ndio ulikuwa hauitaki hiyo katiba mpya ??

Au ni nini hasa ??!
 
Ili Tanzania mpya izaliwe, ilikuwa ni lazima ile ya zamani ife. Hapa nazungumzia 'system' ya zamani. Yale makundi ya watu yaliyohodhi madaraka na mamlaka ya nchi, ambayo yanabadilishana tu kutoka kizazi kimoja hadi kingine.

JPM, labda kwa bahati mbaya au kwa mipango madhubuti ya wazalendo alikwenda ikulu kwa kazi hiyo. Ilikuwa ni vita kwelikweli.

Kwenye madaraka haitakiwi kuacha 'vacuum', unapo ua system ya zamani ni lazima ujenge 'sytem' mpya. System ya JPM ilikuwa bado changa, haina mizizi wala mtaji wa watu kwenye chama na serikali. Na sasa imefagiliwa mbali.

'System' ya zamani imeshinda vita na imerudi madarakani, Tanzania ya zamani inasonga mbele. Kwasasa hakuna matumaini tena ya kuziondoa zile familia za kifalme kwenye madaraka ya nchi.

RIP JPM, you tried.
Mbona Marekani familia za Bush zilibadilishana madaraka baba na mtoto?

Familia za Kennedy zilibadilishana madaraka mtu na kaka ake?

Clinton naye alitaka mkewe achukue madaraka.

System yako iko poa tuu na bado imara. Sisi tumekwama wapi?
 
ilapasa kutokea yaliyotokea si kwa bahati mbaya bali kwa maslahi mapana ya nchi kwa uwezo wa MUNGU.
 
Angekuwa mzalendo wa kweli, angejenga mifumo na taasisi imara, kwa Bahati mbaya alianza kujijenga kwa Nguvu zote mfumo mbaya zaidi wa Jeshi la mtu mmoja . " Dictatorship stile.
Hakuna jipya alileta isipokuwa kuendeleza kwa ukatili zaidi mfumo wa chamadola.

Akaongeza sauti moja tu, ukilala ukiamka ni yeye tu.
 
Vyama vingi havikuanzishwa Tanzania ili siku moja vyama pinzani vishike madaraka.

Na mzizi wa tatizo uko hapo, vyama vingi halikua dai la wananchi, bali CCM iliamua kurejesha mfumo huo ili kuendana na vuguvugu la mabadiliko ya kisiasa la mwishoni mwa miaka ya 80. Ilikua ni badili au ukubali kubadilishwa, CCM wakaamua ku take control ya mabadiliko

Hivyo basi CCM wanajua namna ya kuishi navyo mwaka hadi mwaka. Wanaosema CCM itatawala milele sio wajinga, wanaujua ukweli mchungu.
Hiyo CCM ndiyo hizo systems za kimafia unazolalamikia ukidai JPM alikuwa akitaka kuleta mabadiliko. Hiyo kuishi kiakili na upinzani na kutawala milele ndio mkakati wa kuendelea kufisidi nchi na kuzima sauti ya wananchi milele.

In reality, nchi kutawaliwa na magenge ya kimafia milele ndio msiba mkubwa wa taifa hili (the national tragedy). Wananchi hawana uwezo wa kuchagua wala kuwajibisha viongozi wao kidemokrasia.

Mnaoshabikia CCM kutawala milele halafu hapo hapo mnalilia watu wa ajabu kama Magufuli kuja “kuokoa” nchi mnadhihirisha mkanganyiko mkubwa sana mlio nao. Kubali tu kuwa CCM kudumu madarakani kwa kuzima demokrasia maana yake hasa ni magenge ya kimafia kupokezana ulaji, period.
 
Ili Tanzania mpya izaliwe, ilikuwa ni lazima ile ya zamani ife. Hapa nazungumzia 'system' ya zamani. Yale makundi ya watu yaliyohodhi madaraka na mamlaka ya nchi, ambayo yanabadilishana tu kutoka kizazi kimoja hadi kingine.

JPM, labda kwa bahati mbaya au kwa mipango madhubuti ya wazalendo alikwenda ikulu kwa kazi hiyo. Ilikuwa ni vita kwelikweli.

Kwenye madaraka haitakiwi kuacha 'vacuum', unapo ua system ya zamani ni lazima ujenge 'sytem' mpya. System ya JPM ilikuwa bado changa, haina mizizi wala mtaji wa watu kwenye chama na serikali. Na sasa imefagiliwa mbali.

'System' ya zamani imeshinda vita na imerudi madarakani, Tanzania ya zamani inasonga mbele. Kwasasa hakuna matumaini tena ya kuziondoa zile familia za kifalme kwenye madaraka ya nchi.

RIP JPM, you tried.
Mungu wa watanzania yuko kazini hata Sasa. Mtu
Hizi ni takataka haziwa na binu hata kidogo zaidi ya mabavu
Mtume Mwingira alisema hadharani kuwa wakat wa awamu ya Tano SHETANI ALIKUWA AMEKAA IKULU WAKATI HUO, watu kupotea,lisu kupigwa risasi nk ilikuwa ni ishara kuwa mfumo alipkuwa anaujenga Magufuri ulikuwa niwa kuipeleka nchi yetu kuzimuni Kwa mjibu wa mtume Mwingira. Akina sabaya na makonda ni zao baya la mfumo huo. Tunamuombea raisi Samia Kwa Mungu Ili aongoze nchi yetu Kwa upendo,haki na uhuru Ili pawe ni mahali salama pa kuishi. Heri mfumo hou wa magufi ufe kuliko kuendelea kuwepo na kuleta matatizo Kwa watanzania. Hata Bashiru naye apewe ubalozi Ili atupishe hapa kwetu kama Pole pole alivyoondolewa
 
Nadhani kwenye system yake alipanga kuwajaza wasomi wa vyuo vikuu na watu wengine aliowainua toka jalalani.

Somehow the gaps had to be filled with the available human resources.

Akina Happy, Sabaya na Bashite ni kwa ajili ya kufanya 'dirty work' ambayo ni lazima iwepo wakati wa kuvunja mfumo wa zamani. Hauwezi kuwatuma wa jalalani kufanya kazi hizo
I got great point 🤗.
 
Alivunja mpaka mifumo mizuri. He was creating hell

Sent from my itel W6004P using JamiiForums mobile app
 
Njia pekee ili system iliyopo sasa ife, sharti upinzani uingie ikulu.

Mbali na upinzani kuongoza ni kujidanganya tu.

Tatizo Tanzania hakuna upinzani ambao uko serious, kuweka maslahi binafsi pembeni na kuwaunganisha Watanzania wote wa dini zote na wasio na dini, makabila yote, kanda zote, matajiri, middle class na maskini, wafanyabiashara na wafanyakazi.

Ikitokea TZ kupata chama chenye kuzingatia haya, maslahi mapana ya Taifa, kinachukua nchi mapema.
 
Na afadhali alifia mbali maana alikuwa anaanzisha system ya kihuni. Imagine eti waendesha system walikua kina Sabaya, Makonda, Mahita, Mnyeti na wahuni etc
..unamiaka mingap bwashee, mbona huna akili Ivo, system yake ilkua ni kujaza wasomi wa vyuo vikuu, hao watu uliowataja ilkua ni lazma wawepo ili kuivunja Ile system iliokuepo lasivyo isingewezkana
 
Ili Tanzania mpya izaliwe, ilikuwa ni lazima ile ya zamani ife. Hapa nazungumzia 'system' ya zamani. Yale makundi ya watu yaliyohodhi madaraka na mamlaka ya nchi, ambayo yanabadilishana tu kutoka kizazi kimoja hadi kingine.

JPM, labda kwa bahati mbaya au kwa mipango madhubuti ya wazalendo alikwenda ikulu kwa kazi hiyo. Ilikuwa ni vita kwelikweli.

Kwenye madaraka haitakiwi kuacha 'vacuum', unapo ua system ya zamani ni lazima ujenge 'sytem' mpya. System ya JPM ilikuwa bado changa, haina mizizi wala mtaji wa watu kwenye chama na serikali. Na sasa imefagiliwa mbali.

'System' ya zamani imeshinda vita na imerudi madarakani, Tanzania ya zamani inasonga mbele. Kwasasa hakuna matumaini tena ya kuziondoa zile familia za kifalme kwenye madaraka ya nchi.

RIP JPM, you tried.
Naona unakata tamaa bure. Mama ni mpito tu 2025 kazi ndio inaendelea. Usisikie ngonjera za mama. 2025 anapatikama magufuli mpya nakwambia.
Unaona sasa tony blair kila siku yuko ikulu anachojia eti kusafisha nchi nje toka picha ya magufuli? Yaani dili hili napata hasira hadi basi.
 
Mungu wa watanzania yuko kazini hata Sasa. Mtu

Mtume Mwingira alisema hadharani kuwa wakat wa awamu ya Tano SHETANI ALIKUWA AMEKAA IKULU WAKATI HUO, watu kupotea,lisu kupigwa risasi nk ilikuwa ni ishara kuwa mfumo alipkuwa anaujenga Magufuri ulikuwa niwa kuipeleka nchi yetu kuzimuni Kwa mjibu wa mtume Mwingira. Akina sabaya na makonda ni zao baya la mfumo huo. Tunamuombea raisi Samia Kwa Mungu Ili aongoze nchi yetu Kwa upendo,haki na uhuru Ili pawe ni mahali salama pa kuishi. Heri mfumo hou wa magufi ufe kuliko kuendelea kuwepo na kuleta matatizo Kwa watanzania. Hata Bashiru naye apewe ubalozi Ili atupishe hapa kwetu kama Pole pole alivyoondolewa
Kinachofuata atapewa ubalozi maana tayari yeye ni balozi
 
Back
Top Bottom