Leonel Ateba Mbinda
JF-Expert Member
- Feb 20, 2023
- 644
- 2,695
Kwa wasiofahamu, Murtaza Mangungu ni mmatumbi wa Kilwa Kaskazini, kwao ni Kipatimu kule kulikoanza vita ya Maji Maji, Mangungu amekuwa mbunge wa jimbo la Kilwa Kaskazini, baadae akaangushwa na mbunge wa Cuf ambaye ni mpwa wa marehemu Kingunge Ngombale Mwiru aitwae Vedasto Ngombale.
Baadae Mangungu alikuwa mshauri wa Waziri Mkuu katika masuala ya siasa, akaondolewa katika nafasi hiyo, mwaka 2020 Mangungu alishinda kura za maoni CCM akimshinda mbunge wa sasa wa jimbo hilo Francis Ndulane, hata hivyo Magufuli alimkataa Mangungu na akakata jina lake.
Mangungu akakimbilia dar kutafuta kazi ya kufanya, akaingia Simba na sasa tunapambana naye.
Mwakani tukiamka salama Mangungu atarudi tena kupambania nafasi yake aliyopokwa na Magufuli mwaka 2020, Magufuli hakukata jina lake kwa bahati mbaya, vyombo vilimshauri Ndulane ndio anafaa hivyo Mangungu akatemwa.
Mangungu alikasirika sana lakini hakuwa na la kumfanya Magufuli.
Mangungu anakubalika sana jimboni kwake, hata kesho zikipigwa kura za maoni Mangungu atashinda, anakubalika Kipatimu, anakubalika Namayuni, anakubalika Somanga, anakubalika Tingi, anakubalika Chumo, anakubalika Kinjumbi.
Ni mjanja sana katika masuala ya siasa, kwenye mpira Mangungu hayupo.Mangungu sio mtu wa mpira, Mangungu hana uwezo wa kuchambua mpira, Mangungu ukimuuliza kati ya Prince Dube vs Pa Omary jobs kwake anampa Jobe 100%.
Simba tuna tabia za kijinga sana, sisi tunaojua mpira tunaonekana mafala, malofa kwa sababu tu hatuonekani kwenye social media au tukienda uwanjani hatukai VIP, dharau zimekuwa nyingi ndio maana leo kwenye uongozi kuna watu wenye CPA lakin mpira hawaujui, kuna wanasiasa ambao hata kikosi cha kwanza simba hawajui kupanga.
Kazi tunayo.