Umesema vizuri sana. Labda tu nikwambie kwamba hatuwezi kwenda kwa approach ile ile ya tangu uhuru tukategemea matokeo tofauti. Vitu kama elimu, ujuzi, teknolojia ndio msingi wa maendeleo na kujitegemea. Vitu kama hivi haviombwi ili upewe kama msaada (hapa ndipo tunapokosea); vitu hivi hununuliwa kwa gharama nyingi sana. Mzungu haji eti akusaidie teknolojia, na ni kitu hakiyamkiniki, mtu katumia gharama kubwa sana kujenga ujuzi, maarifa, na teknolojia yake, aje akupe bure? Hizi ni intellectual property rights na hazigawiwi kama njugu, maana ndiyo siri yao ya mafanikio, nguvu na ukwasi.
Kama kweli tunataka kujitegemea, kujitawala na kupata nguvu kiasi ni lazima tuwe tayari kutumia pesa kuwekeza katika ujuzi, maarifa na teknolojia. Wachina walifanya hivyo wakapeleka watu wao Havard, MIT, Princeton ili wavune maarifa na teknolojia za kigeni, waliporudi wakaijenga nchi yao kwa mchanganyiko wa maarifa na teknolojia mpya na zile zilizobuniwa locally.
Sisi tulipeleka watu nje ya nchi na bado tunapeleka, lakini nadhani mwanzoni mwa uhuru mahitaji ilikuwa tupate watu wanaoweza kuongoza serikali kisasa. Msukumo huo bado uko hivyo hivyo na matokeo yake nchi yetu imejaa policy makers na makarani wengi badala ya kuwekeza kwenye watu wenye real talents za ubunifu wa teknolojia.
Kwa hiyo sisi tunaweza kufanya hivi, kwamba serikali iendelee kuweka msisitizo wa uwekezaji wa viwanda, na factories zinaoongeza thamani ya raw materials zetu. Watu wetu wakiajiriwa katika technical departments za uwekezaji huo ndio namna ya kujiongeza katika maarifa na teknolojia za kisasa. Wakati huo huo ziwepo jitihada za makusudi, za kupeleka vijana wetu wenye talent kwenye mataasisi ya kibabe huko duniani ya elimu za teknolojia. Hawa wawe national assets wakirudi wasiachwe kwenye mataa kama tulivyozoea. Wawe incubated kama sehemu ya private na public sector, na ndivyo China ilivyofanya, ndivyo Ulaya inavyofanya, nashangaa kwa nini sisi tunafanya tofauti.