Hayati Magufuli alipokuwa hai hakukuwa na uhaba wa mvua na ukame nchini kama sasa

Hayati Magufuli alipokuwa hai hakukuwa na uhaba wa mvua na ukame nchini kama sasa

YEHODAYA

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2015
Posts
36,902
Reaction score
52,001
Mcha Mungu Magufuli alipokuwa hai hakukuwa na uhaba wa mvua na ukame nchini Kama sasa

Kuondoka tu mcha Mungu Magufuli nchi ukosefu wa mvua kila Kona, ni ukame nchi nzima na tishio la njaa kila kona ya nchi hali ya hewa vipimo vyao vinaona ukame, ukosefu wa mvua na njaa tu inayokuja.

Mwenyewe mcha Mungu angekuwepo haya yasingekuwepo

Serikali badala ya kuitisha maombi wanaenda kuhudhuria mkutano wa Mabadiliko ya Tabia nchi kuomba pesa kwa wazungu kwani pesa zaweza leta mvua msimu huu?

Magufuli angeshaitisha maombi ya kitaifa lakini kwa kuwa alikuwa mcha Mungu, Mungu alihakikisha kipindi chake mvua ipo ya kutosha, ukame haupo na njaa haipo pamoja na yeye kutohudhuria mkutano wowote wa Mabadiliko ya Tabia nchi popote duniani.
 
snoop.png

Hivi ile Ngo ya TWAWEZA Ilisema nini kuhusu Watu wanaovutiwa na CCM?
 
Ndio lipo neno katika biblia lisemalo mwenye haki akitawala nchi hufurahi!ila sidhani kama tumefika huko mama samia wa watu amejikuta ni rais by default je leo Mungu huyu mwenye upendo aanze kumwadhibu kwasababu ipi.
 
Amosi 4:6-9

[6]Mimi nami nimewapa usafi wa meno katika miji yenu yote, na kutindikiwa na mkate mahali penu pote; lakini hamkunirudia mimi, asema BWANA.
[7]Tena nimeizuia mvua msiipate, ilipobaki miezi mitatu kabla ya mavuno; nami nimenyesha mvua juu ya mji mmoja, nikaizuia mvua isinyeshe juu ya mji mwingine; sehemu moja ilipata mvua, na sehemu isiyopata mvua ilikatika.
[8]Basi kutoka miji miwili mitatu walitanga-tanga kuendea mji mwingine wapate kunywa maji, wasipate ya kuwatosha; lakini hamkunirudia mimi, asema BWANA.
[9]Nami nimewapiga kwa ukavu na koga; wingi wa bustani zenu na mashamba yenu ya mizabibu, na mitini yenu na mizeituni yenu imeliwa na tunutu; Lakini hamkunirudia mimi, asema BWANA.
 
Back
Top Bottom