Hayati Magufuli aliweza kujenga miradi kwa fedha za ndani, hizo fedha za ndani kwa sasa zinafanya kazi gani au mapato yameshuka?

Wajinga kama ninyi ndio mlikuwa mmeridhika kuwa kuna "fedha za ndani".
Maana mlikuwa hamuoni wafanyabiashara wakiporwa fedha zao, na Bureu de Change zikiporwa, mishahara hakuna increment, wafanyakazi wakifukuzwa eti hawana vyeti.

Sasa wajinga mkiwa wengi, nchi ndio itajengeka!
 

Kiwango cha kufikiri na kuchambua ukweli na uwongo ni duni sana kwa Watanzania walio wengi. Magufuli alijuwa UJINGA uliopo kwa Watanzania na akautumia kwa KUWADANGANYA
Magufuli alikuwa anajuwa kiwango cha ujinga wa Watanzania walio wengi na ndiyo ukawa mtaji wake kwa propaganda za UWONGO. Wasomi na wajuzi wa mambo akawanyamazisha kwa sheria mbaya za mtandao, takwimu na sheria ya habari. Amedanganya na ikawa ndiyo hulka yetu na mpaka alipokufa tukadanganywa kwa siku 7 kuwa yupo anachapa kazi.
 
Nani kakwambia magufuli hakukopa? Fuatilia ripoti ya CAG ya mwaka jana
 


Kudanganywa na kuona miradi ya maendeleo na kudanganywa halafu unaletewa chandarua wapi tumepigwa..
 
Kwa hiyo mkuu nawe ulikuwa unaamini ni fedha za ndani. Na huku wakizunguka kwenye makorido ya benki ya dunia, shirika ka fedha duniani kukopa fedha za miradi.
 
Kudanganywa na kuona miradi ya maendeleo na kudanganywa halafu unaletewa chandarua wapi tumepigwa..
Unashangaa chandarua Leo kupewa na USAID? Huyo Magufuli wako akiwa primary school au secondary alikunywa uji au ugali ulioletwa kwa msaada wa USAID.

Waulize wasomi wote wenye umri 55+ wakuambie Bulga ni nini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…