Hayati Magufuli aliweza kuwatisha waovu, mifumo iliamka kufanya kazi

Kumbuka kama ni uovu yeye alikuwa mwovu wa waovu!
Na UOVU wake ni mzuri,
Sababu alimsaidia mama mjamzito kijijini kujifungua bila matusi ya manesi,

UOVU wake ulisababisha kutisha wakata umeme na wauza generators,

Makali ya umeme yalipungua,

UOVU wa aina hii wa kusaidia wananchi maskini ni UOVU mzuri.

Magu Abarikiwe.
 
Mbegu aliyoipanda jpm ipo siku itamea tu.

Ipo siku haya majizi yatalia na kisaga meno
Ni sisi Hawa Hawa tutasababisha imee,

Kwa Mfano, sasa hakuna Mtanzania utamdanganya kuwa Nchi Ina upungufu wa umeme kusababisha mgao,

Tunajua fika, kundi dogo lipo kufanya hayo Ili kutimiza maslah Yao binafsi.

Siku yaja.
 
Ok kama kweli hebu tuambie wewe ni kiasi gali hilo shetani lenu la Chato lilikusanya kupitia vile vitambulisho vya Magufuli vya 20,000.
Tuambie zilienda wapi.

Ukweli ni kwamba alitutia hofu mpk vyombo vya habari vikawa vinaogopa kuripoti mapungufu na maovu ya utawala wake.

Prof. Asad alipothubutu alipita nae.
Lisu alipothubutu alikiona.
Ben Sa8 alipothubutu kilichomfika anakijua mwenyewe.
 
Reactions: K11
KAZI za Magu zinaonekana wazi.

Pita pale kijazi flyover utaona alama yake,

Tembea Nchi nzima uone KAZI zake,

Ikiwa aliiba Kisha kwenda kujenga vinavyoonekana,

Wizi wake ni mzuri wenye TIJA.
 
Shabiby alipata Ubunge kupitia huyo huyo Magufuli wenu.
Acha umasikini wa kuchukia matajiri
 
Oops! We ran into some problems

You do not have permission to view this page or perform this action.
 
KAZI za Magu zinaonekana wazi.

Pita pale kijazi flyover utaona alama yake,

Tembea Nchi nzima uone KAZI zake,

Ikiwa aliiba Kisha kwenda kujenga vinavyoonekana,

Wizi wake ni mzuri wenye TIJA.
Hujajibu.
Alikusanya sh. ngapi ya vitambulisho.
Uliwahi ht kusikia japo kijuujuu tu kwamba Ngosha alikusanya kiasi gani kupitia vitambulisho uchwara vile?
Hata bajeti yake sijui ilikuwaje na sijui alizipeleka wapi mwizi yule
 
Hujajibu.
Alikusanya sh. ngapi ya vitambulisho.
Uliwahi ht kusikia japo kijuujuu tu kwamba Ngosha alikusanya kiasi gani kupitia vitambulisho uchwara vile?
Hata bajeti yake sijui ilikuwaje na sijui alizipeleka wapi mwizi yule
Pesa za vitambulisho ziliingia kwenye fuko kubwa,

Ndiyo maana Nchi nzima enzi zake, miradi haikusimana.

Karibu🙏
 
Umesema wewe ni mtumishi wa umma,

Kabla ya Magufuli, ulikuwa unafanya deal Gani Ukiwa Ofisini zilizokuwezesha kusomesha watoto international schools?
Nimefanya kazi kabla ya Magufuli, wakati wa Magufuli na baada yake, hivyo elewa usitawi wa jamii uliimarika zaidi enzi ya utawala wa Mh. J. Kikwete, wengi walipata maendeleo halisi ya vitu na watu.

Enzi za utawala wa Mh JPM usitawi wa jamii upande wa watu ulisimama, mzunguko wa fedha uliminywa na serikali ikaacha matumizi yanayochochea ongezeko la fedha katika jamii, mwisho wakaona haitoshi wakaanza ujambazi wa kufunga akaunti za watu benki na kuchukua fedha zao huku wengine wakiishia kwenye viroba au korokoroni.

Katika tawala zote, hakuna utawala ambao haujajenga barabara, madaraja, shule, hospitali au kutoa ajira.
Labda niwe ninaongea na vijana wa jana ambao hawajui tulipotoka, tulipo na tunakoelekea.

Hivyo sasa, nikija kwenye swali lako, nilipata fedha za kuendeshea maisha yangu na familia kupitia biashara, ufugaji, kilimo na ajira.

Chini ya utawala wa JPM alipunguza kipato changu cha kwenye ajira kwa kuacha kunipandisha madaraja, kuweka nyongeza ya kila mwaka kwa mujibu wa sheria, kufuta posho za kazi wakati bei za vitu zinapanda kila siku na shilingi ikishuka thamani kila wakati.

Pia aliathiri biashara zangu kupitia wale watu waliokuwa wakijiita wamepokea maelekezo toka juu ili waje kukushughulikia.

Upande wa kilimo, nilikuwa ninalima mazao ya biashara ambayo alienda kuathiri bei ya mazao yangu huku mengine akisema ni mboga tule tu na mengine akikorofisha mfumo wa stakabadhi ghalani.

Kwa hoja hizo usitegemee ningebaki bila kutetereka mfukoni ili kukidhi mahitaji yangu ya kila siku.

Hapo nimezungumza kwa upande wangu lakini mtu pekee aliyefurahia utawala wa JPM ni masikini hususani wale waliokuwa wanafurahia kuitwa wanyonge na watu wasio na elimu ya kutosha.

Vijana enzi za mtangulizi wake, baadhi ya kada wakihitimu wote walikuwa wanalamba ajira, ila baada ya huyo mtu wenu wengi wanalamba miguu na njia kila siku kusaka ajira bila mafanikio.

Acha niishie hapa kwa leo.
 
Mfuate alipo we kenge
 
Asingefariki lazima angelazimika kubadili mfumo, angechagua mfumo upi, hata mimi sijui.
Ingefika pahala asingeweza tena kuwatawala watu kwa hofu tena, kiasili a human being is rebel, ni vile tu watu walikuwa kwenye shock bado, kwa hiyo alitake advantage ya huo muda.

Kwa hiyo ni mbinu ya muda mfupi, watu wakijiadjust na kuanza kujitafuta na kujipata wapi palipo na udhaifu mambo hubadilika.
 
Kwani ni vipi katika hivyo hakijawahi kufanyika nchi hii, au ambacho hakifanyiki hivi sasa, au ndio mambo ya mahaba niue?
 
Maono yake juu ya Tanzania Tajiri yenye kujitegemea, itakayosaidia Nchi maskini ulaya,


Lazima tuhakikishe yanatimia.
Kuna Nchi Ulaya ni masikini zaidi yenu?
 
Kwani ni vipi katika hivyo hakijawahi kufanyika nchi hii, au ambacho hakifanyiki hivi sasa, au ndio mambo ya mahaba niue?
Mengi yamewahi kufanyika na yanafanyika,

Kutumia miaka mitano pekee kuanzisha ujenzi SGR, Daraja la Busisi, Flyovers, Ununuzi wa ndege, barabara Nchi nzima,

Jambo Hilo linashtua,

Magu ametupa kujua kuwa nchi yetu Ina pesa nyingi sana zinazopotea Bure.

Mimi siipendi CCM, ila Magu alisababisha tuitazame Nchi yetu Kwa jicho la tofauti.

Baada ya tarehe 17, tutaendelea na spana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…