Hayati Magufuli aliweza kuwatisha waovu, mifumo iliamka kufanya kazi

Hayati Magufuli aliweza kuwatisha waovu, mifumo iliamka kufanya kazi

Hapo nakubaliana nawe.

Sijachotwa na propaganda, maana propaganda ni fictious,

KAZI alizofanya Magu zinaonekana na kushikika,kamwe haziwezi kuwa propaganda.

Viongozi waliopo wangeiga kuziba mianya ya wizi wa PESA za umma kama Magu,

Tungekuwa mbali.
Nimekuambia pitia ripoti za CAG kipindi Cha Magufuli kuhusu wizi wa fedha, naona unazunguka tu. Nijuavyo ripoti ya CAG ndio kipimo Cha usalama wa fedha za umma. Lakini Hadi CAG aliondolewa kwa mizengwe na Magufuli. Sasa unapata wapi uhalali wa kusema hakukuwa na wizi wakati wa Magufuli, wakati hakutaka CAG afanye kazi yake vizuri?

Propaganda za majengo zilikubeba Hadi umekuwa kama mjinga. Kwani miundombinu Hadi sasa imesimama? Si ajabu ww ni mmoja ya waliotekwa na propaganda zake kuwa Tanzania ilijenga viwanda 4,000+.
 
Wezi walimchukia sana JPM
Yeah wezi kama kina Mwanyika walimuogopa JPM ndio maana licha ya kesi ya uhujumu uchumi wa ACACIA ila akazawadiwa ubunge!!

Waliotajwa wote kwenye kesi za Tanzanite, almasi, na dhahabu (Acacia) n.k hakuna hata mmoja ambaye amefungwa mpaka leo hii!! Aisee kweli wezi walimuogopa JPM!!

Bila kusahau mafisadi papa waliotajwa na kamati ya Bashiru kuiba mali za CCM sikuona hata mmoja akiburuzwa mahakamani au kufungwa!! Kweli wezi walimuogopa JPM!!

Eeh TAKUKURU walipewa agizo wawasake watoa rushwa kipindi cha chaguzi za CCM!! cha ajabu ripoti haikuwekwa public wala hakuna aliyefunguliwa kesi ya rushwa!

Oooh Nchambi!! Alikamatwa na nyara za serikali meno ya tembo ya kutosha na mabunduki kibao. Cha ajabu akaachiwa tu..... ilihali mtu ukidakwa na kilo moja ya nyama pori unafungwa miaka 20+

Kweli JPM aliogopwa na wezi
 
Ila waovu hawatishiki wanamizizi sana maana waovu wote siku zote wanamifumo ilijengeka kwa rushwa ili kuwatoa yakupasa kwanza kujenga mifumo yako kwanza vinginevyo utakuja juta!
 
Nimekuambia pitia ripoti za CAG kipindi Cha Magufuli kuhusu wizi wa fedha, naona unazunguka tu. Nijuavyo ripoti ya CAG ndio kipimo Cha usalama wa fedha za umma. Lakini Hadi CAG aliondolewa kwa mizengwe na Magufuli. Sasa unapata wapi uhalali wa kusema hakukuwa na wizi wakati wa Magufuli, wakati hakutaka CAG afanye kazi yake vizuri?

Propaganda za majengo zilikubeba Hadi umekuwa kama mjinga. Kwani miundombinu Hadi sasa imesimama? Si ajabu ww ni mmoja ya waliotekwa na propaganda zake kuwa Tanzania ilijenga viwanda 4,000+.
Huwezi kuongea lugha ya Ripoti ya CAG Kwa mkulima kijijini akakuelewa,

Ukimwambia mkulima kuwa Magu alikuwa Mwizi, Mimi nikamwonyesha mkulima BWAWA la JNHP wewe utapigwa mawe.

Ukisema Magu ni Mwizi kupitia Ripoti ya CAG, Mimi nikamwonyesha mvuvi meli mpya ya Mv VICTORIA utaonekana hamnazo.

KAZI za Magu zinaonekana, hazipimwi na Ripoti ya CAG, Magu hakutumia Utaratibu Rasmi kuchukua pesa za umma kuzipeleka kwenye KAZI alizofanya.

Hivyo, kutofuata taratibu za kimfumo kufanya jambo jema, hakumweka katika kundi la waizi.

By the way, CAG alisema pesa hazijulikani zilipo, hakusema zimeibwa.
 
Nimekuambia pitia ripoti za CAG kipindi Cha Magufuli kuhusu wizi wa fedha, naona unazunguka tu. Nijuavyo ripoti ya CAG ndio kipimo Cha usalama wa fedha za umma. Lakini Hadi CAG aliondolewa kwa mizengwe na Magufuli. Sasa unapata wapi uhalali wa kusema hakukuwa na wizi wakati wa Magufuli, wakati hakutaka CAG afanye kazi yake vizuri?

Propaganda za majengo zilikubeba Hadi umekuwa kama mjinga. Kwani miundombinu Hadi sasa imesimama? Si ajabu ww ni mmoja ya waliotekwa na propaganda zake kuwa Tanzania ilijenga viwanda 4,000+.
Wanasahau CAG alizuiwa kukagua baadhi ya mafungu ikiwemo miradi kama SGR, Manunuzi ya ndege, Mafungu ya kwenda ikulu n.k alipokomaa sana akafukuzwa!!

Yaani unamkataza mkaguzi asikague pesa za umma alafu unajisifia ni msafi.... hawa wafuasi wa JPM sijui reasoning yao inafanyaje kazi.
 
Ukimwambia mkulima kuwa Magu alikuwa Mwizi, Mimi nikamwonyesha mkulima BWAWA la JNHP wewe utapigwa mawe.
Hapa ndio mnakosea.... humu JF tulimuita JK fisadi ila alikua amejenga shule kila kata, alianzisha mradi wa maji ya ziwa Victoria hadi yamefika Singida, alijenga lami na madaraja almost mikoa yote, alijenga bomba la gesi ambalo linachangia 80% ya umeme wa Tanzania, pia alijenga extension ya Airport ambayo ni ya kisasa sana, huyo huyo JK alijenga UDOM, let alone alileta mwendokasi Tanzania n.k

Sasa kama mambo ya kuonekana ndio hoja sidhani kama JK angetukanwa vile kuwa ni fisadi licha ya yote aliyojenga.
 
Yeah wezi kama kina Mwanyika walimuogopa JPM ndio maana licha ya kesi ya uhujumu uchumi wa ACACIA ila akazawadiwa ubunge!!

Waliotajwa wote kwenye kesi za Tanzanite, almasi, na dhahabu (Acacia) n.k hakuna hata mmoja ambaye amefungwa mpaka leo hii!! Aisee kweli wezi walimuogopa JPM!!

Bila kusahau mafisadi papa waliotajwa na kamati ya Bashiru kuiba mali za CCM sikuona hata mmoja akiburuzwa mahakamani au kufungwa!! Kweli wezi walimuogopa JPM!!

Eeh TAKUKURU walipewa agizo wawasake watoa rushwa kipindi cha chaguzi za CCM!! cha ajabu ripoti haikuwekwa public wala hakuna aliyefunguliwa kesi ya rushwa!

Oooh Nchambi!! Alikamatwa na nyara za serikali meno ya tembo ya kutosha na mabunduki kibao. Cha ajabu akaachiwa tu..... ilihali mtu ukidakwa na kilo moja ya nyama pori unafungwa miaka 20+

Kweli JPM aliogopwa na wezi
Nimeipenda hii 😍
 
HAYATI Magu ndiye anajadiliwa hapa.

Wizi wa Magu hauthibitishwi popote zaidi ya KAZI njema alizolifanyia Taifa.

By the way, tupo kimtizamo chanya zaidi kuliko mitizamo hasi.
 
Wanasahau CAG alizuiwa kukagua baadhi ya mafungu ikiwemo miradi kama SGR, Manunuzi ya ndege, Mafungu ya kwenda ikulu n.k alipokomaa sana akafukuzwa!!

Yaani unamkataza mkaguzi asikague pesa za umma alafu unajisifia ni msafi.... hawa wafuasi wa JPM sijui reasoning yao inafanyaje kazi.
Huyu jamaa aliyekuwa na mahaba na Magufuli anadhani Kila mtu ni mjinga aliyetekwa na propaganda za Magufuli, halafu wanadhani wote tumesahau ukweli ule. Anaanzisha na Uzi kabisa kuonyesha kuwa Magufuli alikuwa msafi kwenye fedha! Namuambia atupe ripoti za CAG kuibeba hoja yake, anasema niweke ripoti za CAG pembeni. Sasa kama ripoti ya serekali kuhusu usafi wa fedha, ni kipimo gani anatumia kuhusu usafi wa Magufuli kwenye fedha?

Halafu analeta zile propaganda mfu walizokuwa wanalizimisha watu kwa lazima kuwa maendeleo yake yanaonekana kwa macho. Inakuwa kama ni mara ya kwanza hiyo miundombinu kujegwa hapa nchini. Enzi za Magufuli akipika data sijui za viwanda na vituo vya afya, niliwaambia wafuasi wake waweka jedwali kuonyesha viwanda vilipo, Kijiji/mtaa, wilaya, Mkoa na gharama ya mradi. Hakuna aliyekubali kufanya hivyo walitaka tuamini tu kwa wao kututajia idadi za kupika.

Crimea Jingalao
 
Yaani Kwa Mfano uingie mikononi mwa wazee na unadeal na drugs,

Unadhani njia Gani zitatumika kuwafanya uwataje Wana mtandao wenzio?

Coin Ina two sides. Amani na maendeleo haviwezi kuja katika Taifa usiposhughulika na waovu.

Yaani kuhesabu kura ni drugs au ??
 
Yeah wezi kama kina Mwanyika walimuogopa JPM ndio maana licha ya kesi ya uhujumu uchumi wa ACACIA ila akazawadiwa ubunge!!

Waliotajwa wote kwenye kesi za Tanzanite, almasi, na dhahabu (Acacia) n.k hakuna hata mmoja ambaye amefungwa mpaka leo hii!! Aisee kweli wezi walimuogopa JPM!!

Bila kusahau mafisadi papa waliotajwa na kamati ya Bashiru kuiba mali za CCM sikuona hata mmoja akiburuzwa mahakamani au kufungwa!! Kweli wezi walimuogopa JPM!!

Eeh TAKUKURU walipewa agizo wawasake watoa rushwa kipindi cha chaguzi za CCM!! cha ajabu ripoti haikuwekwa public wala hakuna aliyefunguliwa kesi ya rushwa!

Oooh Nchambi!! Alikamatwa na nyara za serikali meno ya tembo ya kutosha na mabunduki kibao. Cha ajabu akaachiwa tu..... ilihali mtu ukidakwa na kilo moja ya nyama pori unafungwa miaka 20+

Kweli JPM aliogopwa na wezi
Kwenye ile ripoti ya professor Ossoro, Andrew Chenge, Daniel Yona nk walitajwa kabisa kwa majina, na ripoti ikashauri wakamatwe kutokana na kuingiza nchi kwenye mikataba mibovu, hakuna aliyeguswa. Sasa Hawa mitume wa Magufuli sijui wanatuona ni wajinga kiasi gani. Cha ajabu walikuwa wanalazimisha Magufuli anakubalika na wananchi, na ilipofika wakati wa uchaguzi ambayo ndio kipimo halisi ya kiongozi kukubalika akapora uchaguzi!
 
Yaani kuhesabu kura ni drugs au ??
Nimesema Kwa Mfano,

Hilo la wizi wa kura, pia Mimi siliafiki kabisa, kupotoa HAKI ya Sanduku la kura ni jambo baya.

Ingawa hayo hayajadiliwi hapa,

Tunakumbuka mema yake, Hasa katika uchapakazi na kusimamia vizuri pesa za umma zisiporwe na waizi.
 
HAYATI Magu ndiye anajadiliwa hapa.

Wizi wa Magu hauthibitishwi popote zaidi ya KAZI njema alizolifanyia Taifa.

By the way, tupo kimtizamo chanya zaidi kuliko mitizamo hasi.
Usilazimishe mjadala ukae kwenye mahaba yako. Tunakuambia msifie upendavyo, lakini ukae kwa kutulia ukipewa ukweli wake Ili tumpe kipimo Cha haki.
 
Wengine walilalamika kuwa wauza drugs hawatendewi HAKI,

Zamani ilikuwa, ukikamatwa Mzigo wa drugs, polisi wakiwa na mtuhumiwa, njiani watapigiwa simu na mkubwa na kuambiwa wausindikize Mzigo sehemu husika wakiulinda,

Magufuli alifanikiwa kudeal na mtandao wa dawa za KULEVYA Kwa mkono wa CHUMA.

Huo ndio Hasa uongozi.
Oya nakumbuka kipindi chake mateja hawakuisha salasala alitokomeza wapi uuzaji wa madawa ya kulevya?
 
Usilazimishe mjadala ukae kwenye mahaba yako. Tunakuambia msifie upendavyo, lakini ukae kwa kutulia ukipewa ukweli wake Ili tumpe kipimo Cha haki.
Naheshimu mawazo Yako,

Nami naheshimu uamuzi wangu wa kukumbuka maeneo ambayo HAYATI Magufuli aliyatendea HAKI.

Abarikiwe huko aliko.
 
Salaam, Shalom.

Ili pawe na Amani, huna budi kuwatisha waovu, KAZI hii ya kuhakikisha waovu hawachezei Sharubu za Serikali, Mungu alimsaidia Hayati Magufuli kuifanya kazi hiyo kwa ufasaha.

Maeneo yafuatayo, alidhibiti kwelikweli;

1. MTANDAO WA WIZI WA PESA ZA UMMA

Tumesikia Rais Samia analalamika Badala ya kuamrisha mifumo, asema kuwa umerudi mtandao wa kuiba pesa za umma, yaani pesa inatoka hazina kuja halmashauri, wanatokea watu, wanachepusha pesa hizo zinaingia katika account zao, na pesa hizo ni za mikopo tuliyokopa!

Miradi aliyeanzisha Magu, ilienda kwa kasi sababu ya ufuatiliaji wa karibu na wezi walidhibitiwa hasa.Usingeweza kukwiba pesa ya umma ukabaki salama.

2. UJAMBAZI WA KUTUMIA SILAHA.

Katika kipindi chake, majambazi walienda likizo, hilo litoshe kutupa kujua kazi kubwa aliyoifanya hasa katika kuifanya mifumo ya ulinzi na Usalama kutenda kazi Kwa viwango vya juu.

3. KUDHIBITI MTANDAO WA DAWA ZA KULEVYA

Kabla ya Magufuli kuingia madarakani, Nchi yetu ilikithiri kwa kutapakaa kwa dawa za kulevya, lakini baada ya miaka kadhaa, mateja wengi walijisalimisha katika sobber houses, sababu kuu ikiwa ni kuadimika Kwa dawa za kulevya mtaani. Hilo litoshe kutuonyesha jinsi ambavyo palifanyika kazi kubwa underground.

4. UTAKATISHAJI FEDHA

Pesa haramu, chafu zilizotokana na biashara ovu ya kuiba pesa za umma, uuzaji dawa za kulevya, biashara chafu za ukwepaji kodi, zilidhibitiwa kwa kiasi kikubwa, jambo hilo lilileta mtikisiko kwenye Uchumi kwa kuwa Kwa namna moja au ingine, pesa hizo zilisaidia kutengeneza ajira sekta binafsi.

5. MFUMO WA EFD ULIFANYA KAZI

Vituo vya mafuta kwa Mfano, vyenye kuingiza pesa nyingi, hazikuwa zikitoa EFD, na walipobanwa kutoa risiti, walitishia kugoma.

Ujasiri wa Magufuli, ulisaidia wafanyabiashara hao kurudi mezani na kukubali kutoa EFD bila masharti.

6. UFANISI KATIKA MIFUMO YA UTOAJI MIZIGO BANDARINI

Ni katika uongozi wa Hayati Magufuli, document za kutoa Mzigo bandarini zilipungua, mwanzoni palikuwa na utitiri wa karatasi na mizunguko iliyochelewesha ufaulishaji mizigo bandarini.

Scana ya ukaguzi wa vitu vinavyopita bandarini ULIFANYA KAZI utawala wa Magufuli, alipambana kweli kweli na ufanisi ulionekana.

HITIMISHO

Pamoja na mapungufu wa kibinadamu na makosa kadhaa aliyoifanya Hayati Magufuli, itoshe kusema, Mungu alimwezesha kukaa katika KITI cha maamuzi sawasawa na kuhakikisha mifumo inafanya KAZI. Magufuli hakulalamika, alichukua hatua.

OMBI: Wananchi tunaomba atokee kiongozi atakayefuta BETTING nchini, hivi sasa, vijana wa CCM+ CDM na wasio na vyama wametekwa na jinamizi hili, HAYATI Magu hakuliweza hili. Maisha hayajawahi kuwa Bahati nasibu.

Tunamshukuru Mungu kwa zawadi ya Rais Magufuli.

Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo Tanzania🇹🇿.

Amen.
Ni propaganda tu ndiyo zilitawala na kutisha vyombo vya habari visiripoti uhalisia. Uwizi wa mali ya umma ulikuwapo kama kawaida. Kama unabisha kaangalie CAG report za 2016-2018, kuna Tsh 2.4 Trillion. CAG Assad alipohoji akamfukuza kazi.

Pili aliwatupa watu wengi rumande kwa hisia bila kufuata utaratibu. Watu hao tuliodhani ni mafisadi walikaa rumande kuanzia 2016/17 hadi mwaka 2021 alipokufa bila Mahakama kusikiliza kesi zao.

Kesi hazikuwa na ushahidi, ila yule Shetani Magufuli akikuchukia tu anakupeleka rumande. Nahisi Magu alikufa ili Tanzania ibaki mahali salama pa kuishi
 
Oya nakumbuka kipindi chake mateja hawakuisha salasala alitokomeza wapi uuzaji wa madawa ya kulevya?
Unajinadi kuwa uliendelea kusambaza dawa za KULEVYA waziwazi kipindi kile?

Au sijakuelewa.
 
Nimesema Kwa Mfano,

Hilo la wizi wa kura, pia Mimi siliafiki kabisa, kupotoa HAKI ya Sanduku la kura ni jambo baya.

Ingawa hayo hayajadiliwi hapa,

Tunakumbuka mema yake, Hasa katika uchapakazi na kusimamia vizuri pesa za umma zisiporwe na waizi.
Angekuwa anasimamia vizuri pesa za umma asingemuhujumu CAG, ambaye kisheria ndio mkaguzi na msimamizi wa pesa za umma. Alikuwa anagoma kabisa CAG asikague fedha kwenye miradi mikubwa. Mtu muaminifu wa pesa za umma, hazuii taratibu za kikaguzi kufanyika.
 
Back
Top Bottom