Hayati Magufuli aliweza kuwatisha waovu, mifumo iliamka kufanya kazi

Hayati Magufuli aliweza kuwatisha waovu, mifumo iliamka kufanya kazi

Mimi kama raia mwema na mtumishi wa umma wa zama za mwendazake, hakika hakuna asiyekumbuka matukio ya huyo mtu hususani suala la kutopandisha madaraja, nyongeza ya mishahara, posho za kazi na vitisho visivyo na kifani kwa watumishi.

Ukija kwenye biashara ndo usiseme, taasisi binafsi nyingi zilikufa au kubadilishiwa matumizi.

Watu wengi hata watoto tulilazimika kuwapeleka shule za kata maana fedha ya kuwapeleka private ilikuwa changamoto na shule nyingi za private ukiondoa zile zinazomilikiwa na taasisi kama Kanisa la RC au Misikiti zilishindwa kujiendesha zikafungwa.

Kwangu mimi siipendi CCM ila huyu mama Mungu ampe miaka mitano mingine ana nafuu hata mitandaoni tunaandika mengi ya kukosoa Serikali na hatutishiwi kuwekwa kwenye viroba, pia kila mtu anaishi bila hofu, amani ipo, biashara zinafanyika na maofosini tunachapa kazi kwa furaha.

Heri utafune mhogo mkavu na maji kwa amani na uhuru kuliko nyama choma kwenye vita.

cc Rabbon

ChoiceVariable
Nyinyi ndo mlikuwa wezi sasa hivi mnamnanga.
 
Ni Kweli kabisa,

Kwa shetani na wezi wa Mali ya umma, Mimi ni HASARA kubwa,

Lakini Kwa Mungu, na wote wenye kiu ya HAKI, Mimi ni FAIDA kubwa sana.
Mbona hata yeye alikuwa anaiba mali ya umma? Au ndiyo nyie wenye macho makengeza, mnaona wizi wa watu wengine ila wa Magufuli hamuuoni. CAG Prof Mussa Assad kwenye ripoti ya 2016-18 alihoji matumizi ya Tsh 2.4 Trillion. Akaishia kufukuzwa kazi na Magufuli
 
Assad alisema hajui pesa zilipo,

Kutojua pesa zimeenda wapi, haimaanishi zimeibwa,

Magu alizikwapua na kwenda kujengea madaraka huko na huko bila kufuata Utaratibu wa kisheria,

Lakini Kwa kuwa KAZI alizofanya ni njema na zinaonekana,

Mtu huyo ni MWEMA.

Abarikiwe.
 
Wacha kujificha kwenye kichaka cha kazi nzuri eti "kujengea madaraja huko na huko". Kufanya manunuzi bila kufuata sheria ndiyo UFISADI wenyewe.

Angalia kuna Bombardier aliyonunua bila kufuata utaratibu, na nyinyi kila siku mnamsifia kununua ndege kumbe mwenzenu alikuwa anatengeneza mpunga wake.

Citizen ya 23 Desemba 2023 inasema hivi
Screenshot_20240317_124729_Chrome.jpg
 
Siku Inakuja,

Chain ya wizi iliyo ndani ya mfumo inayoshirikiana na mapandikizi yaliyoko upinzani kukwamisha wazalendo kunyoosha waovu,

Chain hiyo itakatwa tu.

Magufuli ametuachia Roho ya UZALENDO juu ya nchi yetu, na hayupo wa kutuzuia.

Mungu atubariki.
Wapinzani mnawasingizia, matawi ya mti hunawiri kulingana na kazi ya mizizi na shina. Tusizunguke jamani shida ipo ccm mahala serekali inapoundwa.
 
Wapinzani mnawasingizia, matawi ya mtu hunawiri kulingana na kazi ya mizizi na shina. Tusizunguke jamani shida ipo ccm mahala serekali inapoundwa.
CCM haitaki kurudi katika misingi ya HAKI na haitaki wanyoofu kupata vyeo vya juu,

Upinzani pia wanahusika, walipinga wazi ujenzi wa JNHP wazi wazi,

Lema alisema, tuachane na umeme wa maji, ni gharama kuliko umeme wa jua.

Motive behind ni nini juu ya kauli hizi?
 
Wacha kujificha kwenye kichaka cha kazi nzuri eti "kujengea madaraja huko na huko". Kufanya manunuzi bila kufuata sheria ndiyo UFISADI wenyewe.

Angalia kuna Bombardier aliyonunua bila kufuata utaratibu, na nyinyi kila siku mnamsifia kununua ndege kumbe mwenzenu alikuwa anatengeneza mpunga wake.

Citizen ya 23 Desemba 2023 inasema hivi View attachment 2937046
Assad na Ripoti ya CAG halijatajwa humu,

Jikite kwenye mada, au anzisha Uzi wako uelezee Ripoti ya CAG.
 
CCM haitaki kurudi katika misingi ya HAKI na haitaki wanyoofu kupata vyeo vya juu,

Upinzani pia wanahusika, walipinga wazi ujenzi wa JNHP wazi wazi,

Lema alisema, tuachane na umeme wa maji, ni gharama kuliko umeme wa jua.

Motive behind ni nini juu ya kauli hizi?
Rabbon, Rabbon, Rabbon!... Nimekuita mara 3. Kwa Tz wapinzani are nothing, are negligible nikwambie sasa. Bwawa si linajengwa pamoja na hayo maneno?.
Kwa mwenye dola ndo pa kuelekeza focus.
 
Salaam, Shalom.

Ili pawe na Amani, huna budi kuwatisha waovu, KAZI hii ya kuhakikisha waovu hawachezei Sharubu za Serikali, Mungu alimsaidia Hayati Magufuli kuifanya kazi hiyo kwa ufasaha.

Maeneo yafuatayo, alidhibiti kwelikweli;

1. MTANDAO WA WIZI WA PESA ZA UMMA

Tumesikia Rais Samia analalamika Badala ya kuamrisha mifumo, asema kuwa umerudi mtandao wa kuiba pesa za umma, yaani pesa inatoka hazina kuja halmashauri, wanatokea watu, wanachepusha pesa hizo zinaingia katika account zao, na pesa hizo ni za mikopo tuliyokopa!

Miradi aliyeanzisha Magu, ilienda kwa kasi sababu ya ufuatiliaji wa karibu na wezi walidhibitiwa hasa.Usingeweza kukwiba pesa ya umma ukabaki salama.

2. UJAMBAZI WA KUTUMIA SILAHA.

Katika kipindi chake, majambazi walienda likizo, hilo litoshe kutupa kujua kazi kubwa aliyoifanya hasa katika kuifanya mifumo ya ulinzi na Usalama kutenda kazi Kwa viwango vya juu.

3. KUDHIBITI MTANDAO WA DAWA ZA KULEVYA

Kabla ya Magufuli kuingia madarakani, Nchi yetu ilikithiri kwa kutapakaa kwa dawa za kulevya, lakini baada ya miaka kadhaa, mateja wengi walijisalimisha katika sobber houses, sababu kuu ikiwa ni kuadimika Kwa dawa za kulevya mtaani. Hilo litoshe kutuonyesha jinsi ambavyo palifanyika kazi kubwa underground.

4. UTAKATISHAJI FEDHA

Pesa haramu, chafu zilizotokana na biashara ovu ya kuiba pesa za umma, uuzaji dawa za kulevya, biashara chafu za ukwepaji kodi, zilidhibitiwa kwa kiasi kikubwa, jambo hilo lilileta mtikisiko kwenye Uchumi kwa kuwa Kwa namna moja au ingine, pesa hizo zilisaidia kutengeneza ajira sekta binafsi.

5. MFUMO WA EFD ULIFANYA KAZI

Vituo vya mafuta kwa Mfano, vyenye kuingiza pesa nyingi, hazikuwa zikitoa EFD, na walipobanwa kutoa risiti, walitishia kugoma.

Ujasiri wa Magufuli, ulisaidia wafanyabiashara hao kurudi mezani na kukubali kutoa EFD bila masharti.

6. UFANISI KATIKA MIFUMO YA UTOAJI MIZIGO BANDARINI

Ni katika uongozi wa Hayati Magufuli, document za kutoa Mzigo bandarini zilipungua, mwanzoni palikuwa na utitiri wa karatasi na mizunguko iliyochelewesha ufaulishaji mizigo bandarini.

Scana ya ukaguzi wa vitu vinavyopita bandarini ULIFANYA KAZI utawala wa Magufuli, alipambana kweli kweli na ufanisi ulionekana.

HITIMISHO

Pamoja na mapungufu wa kibinadamu na makosa kadhaa aliyoifanya Hayati Magufuli, itoshe kusema, Mungu alimwezesha kukaa katika KITI cha maamuzi sawasawa na kuhakikisha mifumo inafanya KAZI. Magufuli hakulalamika, alichukua hatua.

OMBI: Wananchi tunaomba atokee kiongozi atakayefuta BETTING nchini, hivi sasa, vijana wa CCM+ CDM na wasio na vyama wametekwa na jinamizi hili, HAYATI Magu hakuliweza hili. Maisha hayajawahi kuwa Bahati nasibu.

Tunamshukuru Mungu kwa zawadi ya Rais Magufuli.

Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo Tanzania🇹🇿.

Amen.
Marehemu hakulalamika kwakua yy alikua final ni sawa na mzazi nyumbani ukikalamikia nyumba yako nani atarekebisha he was taking responsibility/action kwakua hakuna mwingine wakutoa hayo maamuzi zaidi ya yeye
 
Rabbon, Rabbon, Rabbon!... Nimekuita mara 3. Kwa Tz wapinzani are nothing, are negligible nikwambie sasa. Bwawa si linajengwa pamoja na hayo maneno?.
Kwa mwenye dola ndo pa kuelekeza focus.
No,

Vyama vya upinzani ni vyama mbadala, jawapasi kupinga Kila kitu,

Jambo lenye maslah ya umma lazima tuwe kitu kimoja,

Walipasa kukubali HOJA ya ujenzi wa HOJA ya BWAWA la JNHP, upinzani wao ungejikita katika kushauri Serikali kutafuta wakandarasi Bora na wenye Kutoa Bei nzuri chini ya wale Serikali iliyowaabgazia,

Huo ndio upinzani wenye TIJA,

Lakini huu upinzani wa kusema ndege hizo ni pangaboi, bazifai chochote,

Kesho yake tunamuona Lissu aliyepinga ununuzi wa ndege akiziita pangaboi, mtu huyo huyo anazipanda,

Upinzani wa aina hiyo Si mzuri.

Upinzani mzuri ujengwe katika Truth, Truth.

Waliendelea na upinzani wa aina hii, Si Rahisi kuaminika na kupewa Nchi.
 
Marehemu hakulalamika kwakua yy alikua final ni sawa na mzazi nyumbani ukikalamikia nyumba yako nani atarekebisha he was taking responsibility/action kwakua hakuna mwingine wakutoa hayo maamuzi zaidi ya yeye
Mbona sa100 anamlalamikia wizi wa watumishi wanachepusha pesa za miradi zinazotoka hazina Kisha wanahamishia Kwa AC zao? Kwann hachukui hatua?
 
Magu alikwama ktk kufuta mfumo wa Betting.

Hili ni janga la Taifa.
Sio kukwama, Magufuli hakuwa na shida na watu ambao genuinely ni walipa kodi wazuri. Sasa ukitazama yeye ndio alikazia kwamba lazma kampuni hizo zitozwe 18% ya mapato kama kodi. Nadhani katika utawala wake ndo sheria ilitungwa na ikaanza kufanya kazi so automatically existance ya makampuni ya betting na wakamaria ina faida kwa uchumi wa taifa. Hapo mi sioni tatizo kama ni uraibu wa kamari hata walevi pia wana uraibu wa pombe so ni uamuzi binafsi wa mtu kuwa hataki betting na aache.
 
Mbona sa100 anamlalamikia wizi wa watumishi wanachepusha pesa za miradi zinazotoka hazina Kisha wanahamishia Kwa AC zao? Kwann hachukui hatua?
Kwa sababu hana composure kama kiongozi wa taifa
 
Sio kukwama, Magufuli hakuwa na shida na watu ambao genuinely ni walipa kodi wazuri. Sasa ukitazama yeye ndio alikazia kwamba lazma kampuni hizo zitozwe 18% ya mapato kama kodi. Nadhani katika utawala wake ndo sheria ilitungwa na ikaanza kufanya kazi so automatically existance ya makampuni ya betting na wakamaria ina faida kwa uchumi wa taifa. Hapo mi sioni tatizo kama ni uraibu wa kamari hata walevi pia wana uraibu wa pombe so ni uamuzi binafsi wa mtu kuwa hataki betting na aache.
Ungejuwa ni kesi ngapi ziko ICSID na ngapi tumekwisha garagazwa na tunalipa billions of dollars kwa sababu ya maamuzi yake ya HOVYO, usingeandika huo utumbo
 
Back
Top Bottom