Hayati Magufuli anashambuliwa kila kona. Siyo kesi, ila mambo yaende; yasipoenda wananchi watawazomea kila kona

Hayati Magufuli anashambuliwa kila kona. Siyo kesi, ila mambo yaende; yasipoenda wananchi watawazomea kila kona

Wataongea mengi ila Magufuli was the best atleast katika kuhakikisha tuliyoamini hayawezekani yanafanyika
 
Nilikua Ddodma St Gemma Hosp huku mtaani kusema Magu mbaya hawakuelewi yaani wamama wale wanamsifia na wanasema kabisa bila Magu mwanangu asingesoma yaani huyu baba sijui yani km tutapata km yeye.Mama SAMIA ajipange sana akifanya masihhara atazomewa kweli
Achana na hao wamama wenye uelewa mdogo(ashakum si matusi),wewe msimamo wako ni upi juu ya uongozi wa the Late JPM?
 
Wapigaji wamerudi kwa kasi ili mambo yao yaende kazi ni moja kuua legacy yote ya mwendazake alafu waanze kupiga kama ilivyoada
 
Unless unajitoa ufahamu then go back to your memories and search ni nani hasa aliuzika muswada wa katiba wa Mzee Warioba!!
Nahisi unajitoa ufahamu pia. Wangapi waliufyata wakawa wanasema nyeusi ni nyeupe. Haukuwa msimu wa kusema ukweli, waliothubutu walijikuta bahati mbaya zikiwafuata. Kuna yule daktari aliye-challaenge zoezi la kujifukiza niambie nini kilifuata? Nani hapendi kitumbua chake kiwe salama? Au nasema uongo ndugu yangu..!!
 
Tulikuwa tukisema Magufuli anasifiwa na wananchi wasiojua lolote, ama wale waliokuwa wanafaidika na madaraka yake. Kwa wananchi wenye uelewa wa mambo tunajua ni kwa kiwango gani Magufuli ameiweka nchi hii kwenye wakati mgumu, kiuchumi, kisiasa na hata kijamii.

Namfananisha Magufuli na mwizi aliyejenga nyumba nyingi kwa fedha za wizi, ila baada ya kufariki madhambi yake yote kuwa hadharani na mali hizo kupotea.
Fanyeni vyote ila tunataka speed ya JPM,, hospital, barabara, masoko, umeme maji tuone vinaendelea
 
Nahisi unajitoa ufahamu pia. Wangapi waliufyata wakawa wanasema nyeusi ni nyeupe. Haukuwa msimu wa kusema ukweli, waliothubutu walijikuta bahati mbaya zikiwafuata. Kuna yule daktari aliye-challaenge zoezi la kujifukiza niambie nini kilifuata? Nani hapendi kitumbua chake kiwe salama? Au nasema uongo ndugu yangu..!!

Rudi kwenye msingi wa hoja yako Chief!

“Lawama ziende kwa aliezika mchakato wa Katiba Mpya!”

Hayo mengine hayanihusu!
 
Hivyo vyombo havifanyi kazi ya kumlinda Rais kama hisani ni lazima vimlinde vinatekeleza katiba kenge wewe hivi nyie wapumbavu wa magufuli mna akili gani mmfuate huko aliko.

Nimesema mahali hapa jukwaani waseme basi angalau chochote kulinda heshima yao na vyombo wanao viongoza. Heshima ya vyombo hivi imejengwa kwa miaka mingi kwa damu na jasho lao hivyo kukaa kimya si sawa na si haki. Kupotezea tuhuma hizi si afya kwa Taifa hili.

Dr Kigwangala kawa wa kupigiwa mfano wengine nao wa kabarofu basi.
 
Wapigaji wamerudi kwa kasi ili mambo yao yaende kazi ni moja kuua legacy yote ya mwendazake alafu waanze kupiga kama ilivyoada
Wapigaji waliwahi kuisha lini?
 
Mbona nae aliwashambulia wastaafu kwamba awajafanya kitu
 
Hajaacha deni tu acha uongo.kaacha vitu vilivyotumia hiyo pesa pia.Eti kaacha deni utafikiri hizo pesa alikopa akaenda kuweka pesa kwenye akaunti yake uswisi.

Lugha ya ki layman utafikiri mtu hata shule hukwenda. Hiyo miradi kila mkoa na wilaya huioni au ? Elimu bure huioni au ? umeme kila kijiji huuoni au? barabara kila kona huoni au? vituo vya afya kote nchini huoni au nk

Kipindi chake nchi ilikuwa inakopesheka na madeni yalikuwa yanalipika bila shida.Wakopeshaji walituamini

Twende sasa ni challenge kwa serikali iliyopo itamudu kukopesheka na kulipa madeni na kuendesha miradi nchi nzima kama Magufuli alivyomudu? muda ni mwalimu mzui.let us wait and see tuone matusi kwa Magufuli kama yana mantiki
Si mnadai CCM ni chuo cha uongozi na kwamba akitoka chuma kinaingia chuma? Au na ww una doubt uongozi wa CCM?

Uzuri ni kwamba mkifeli ni advantage kwa upinzani na mkifanikiwa pia ni advantage kwa upinzani ku seize opportunity ya kuua legacy ya JPM.

Hapa ni wakati wa Mbowe kucheza akili tu maana CCM wenyewe mnakiri hampo consistent kuongoza nchi.
 
Alianza kwa kufunua madudu ya wenzie nae yake yafunuliwe tuone uadilifu wake
 
Tulikuwa tukisema Magufuli anasifiwa na wananchi wasiojua lolote, ama wale waliokuwa wanafaidika na madaraka yake. Kwa wananchi wenye uelewa wa mambo tunajua ni kwa kiwango gani Magufuli ameiweka nchi hii kwenye wakati mgumu, kiuchumi, kisiasa na hata kijamii.

Namfananisha Magufuli na mwizi aliyejenga nyumba nyingi kwa fedha za wizi, ila baada ya kufariki madhambi yake yote kuwa hadharani na mali hizo kupotea.
Aliwateka akili kundi kubwa la wananchi ambao asilimia kubwa ni illiterate(wanyonge )na kuwadanganya et yeye ndo mkombozi wao na ndo wakawa na kazi ya kuimba shujaa wa Africa, go to hell Magufuli
 
Na hao ndio population kubwa ya Tanzania zaidi ya asilimia 80 na ndio wanyonge wenyewe waliompigia kura na ndio alijitahidi kuwapelekea miradi mingi na elimu bure nk

Ndio aliosimama nao.Lisu alisimama na wanaoielewa akaambulia kura milioni moja

Magufuli akasimama na wasiojielewa wenye elimu duni na uelewa duni na machinga na ma ntilie nk.

Nakubaliana na wewe alisimama na wengi wa chini hakusimama na wachaje wa juu au middle class
Kwa hiyo un informed decisions ndio right decision? Kama unakiri hawajitambui sasa unadhani yakiburuzwa na mama kwa propaganda ndio hawatamuunga mkono pia?

If u agree hawawezi kureason then kubali pia hawatareason hta kma utawala huu ukifel
 
Magufuki kama alikuwa fisadi papa na mwizi na akafanya hayo makubwa ya miradi ya maendeleo kila mkoa wilaya mitaa na vijiji tunatarajia serikali iliyopo itafanya makubwa kwenye miradi maendeleo na ya jamii kuliko fisadi Papa Magufuli ambaye wengi wanyonge walimfurahia na ufisadi wake ulioripotiwa na CAG

Angekuwa hai wanyonge wangemtaka f Magufuli aongezewe kipindi cha kutawala
 
Aliwateka akili kundi kubwa la wananchi ambao asilimia kubwa ni illiterate(wanyonge )na kuwadanganya et yeye ndo mkombozi wao na ndo wakawa na kazi ya kuimba shujaa wa Africa, go to hell Magufuli
umeme kila kijiji zilikuwa nyimbo? Barabara bora za lami.uswahilini na vijijini zilikuwa nyimbo?

Vituo vya afya kila eneo zilikuwa nyimbo?Miradi ya maji kila kona zilikuwa nyimbo?
Adabu sekta ya umma kuhudumia wanyonge zilikuwa nyimbo?

U salute you Magufuli wherever you are .Ume set record ambayo itachukua miaka mingi kuivunja kwa yeyote atakayeshika serikali
 
Muosha uoshwa ye alipokuwa akiwatuma kina veronica france musiba mulaga kuwananga wastaafu.Ukupiga kelele mbona?
Kwetu ni furaha tu huzuni yenu sio huzuni yetu.
Tunasubiria tu msimu wa korosho this time hakuna kizingiti lzm wanywee bia mbuzi.Tupo salama na mama akimaliza mitano tunamuongeza mitano tena.
Utakuja kurudi hapa siku moja ukiwa na huzuni na huamini kinachoendelea kwenye siasa unapewa furaha ya muda mfupi alafu maumivu ya muda mrefu haka kamchezo huwa kapo kwa kila anaeanza.kasoro Mwendazake hakua mnafiki alikua ananyooka penye ukweli anasema ,hataki anasema ndo maana alichukiwa na wengi binadamu tunapenda kudanganywa
 
Mtu mnyonge wa chini haangalii Makaburasha ya CAG wala hata hamjui CAG ndio nani na hahitaji kumjua .Yeye anaangalia mwanawe anaenda shule bure msingi hadi sekondari ? Vituo vya afya vipo? barabara zipo? Maji yapo? Machinga na mama Ntilie mazingira yako mazuri yapo? Hayo Magufuli alihangaika nayo na wanyonge wakamkubali hayo ya CAG mbaki nayo nyie msio wanyonge
Lakini CAG si mteuliwa wa jiwe? We ulitaka aseme uongo?
 
Magufuki kama alikuwa fisadi papa na mwizi na akafanya hayo makubwa ya miradi ya maendeleo kila mkoa wilaya mitaa na vijiji tunatarajia serikali iliyopo itafanya makubwa kwenye miradi maendeleo na ya jamii kuliko fisadi Papa Magufuli ambaye wengi wanyonge walimfurahia na ufisadi wake ulioripotiwa na CAG

Angekuwa hai wanyonge wangemtaka f Magufuli aongezewe kipindi cha kutawala
Kama na wao watakopa 20t why not? Hakuna mnyonge yoyote aliye kombolewa na Magufuli, sana sana ameruhusu biashara wa wamachinga wa mjini ambao wako vocal. Lakini wanyonge kwa maana ya wanyonge, hao huwa wanaburuzwa tu na kuwekewa maneno mdomoni na matapeli wa kisiasa.
 
Back
Top Bottom