Kijana shirikisha ubongo na akili kwa pamoja kwenye ku reason mada zako. Hakuna mtu anamu attack Marehemu Magufuli. Ni vitu vinajitokeza au vinatokelezwa na sasa vinaonekana. Bahati mbaya wakati wa utawala wake hakuruhusu hii.
Nikuulize kitu kirahisi kabisa, hivi unajua huyu CAG yeye Marehemu ndio alimleta baada ya kumtoa wa mwanzo? Sasa unahisi huyu CAG anamzunguka Marehemu?
Kwa uelewa wako, Marehemu alisema ATCL imepata faida ya bilioni 28 na huyu mtaalam wa ukaguzi anasema tumekula hasara ya mabilioni hapa unapendekeza tumuamini nani?
Unaamini Marehemu alikuwa ni binadamu wa kawaida na hence sio perfect au unawaza alikuwa Mungu ambae hakosei? Kama ni binadamu wa kawaida kwann unasumbuka kusikia anakosolewa?
Nikushauri kitu, kila uongozi una namna yake ya kutawala, utawala wa Magufuli ulishapita jifunze ndani ya moyo wako kuamini kuwa Magufuli amekuja na ameondoka sasa ni mama Samia. Nae atakuwa na mazuri yake na mapungufu yake na hazimiki kufuatisha mtindo wa utawala wa Magufuli. Yeye ni Rais kamili na ana uhuru kupanga serekali yake anavyoona yeye inamfaa