Hayati Magufuli huwezi kusahaulika kwa miaka mingi sana kwa Meli kubwa Ziwa Victoria

Huko usukumani Yes hawatamsahau kwa meli! Kila mtu atamkumbuka kivyake tusipangiane, kwani kabla hajazaliwa hakukua na meli Tanzania? Mv Liemba ilikuwepo kabla ya babu yako wala yake, so hamna jipya hapo labda kwako mtoto wa juzi!
 
Magufuli ni rais aliofanya mambo makubwa kwa muda mchache hadi dunia ikashangaa. pumzika kwa amani Baba kazi ulioifanya imeonekana na MUNGU akusamehe makosa yako yote upumzike mbiguni kwa furaha na amani.Amina
 
Ni sawa kabisa, hata wajerumani tunawakumbuka na kuwaenzi sana sisi kama waTanzania kwa kutujengea miundombinu ya reli, MV Liemba ya ziwa Tanganyika nk.
 
Marais wangapi wenye uthubutu wa aina hiyo?. Uzalendo wa hali ya juu.

Kumsahau ni swala lako binafsi.

Kwamba ndio rais wa kwanza kusimamia fedha za umma kujenga miundombinu kadhaa akiwa madarakani au?
 
Kwamba ndio rais wa kwanza kusimamia fedha za umma kujenga miundombinu kadhaa akiwa madarakani au?
Rais wa kwanza kuamua kufuta machozi ya wahanga wa ajali ya May 1996 kwa kufanya maamuzi magumu ya kutengeneza meli mpya yenya ubora mkubwa.

Marais wote hujenga vitu vingi kwa mujibu wa maelekezo ya ilani ya CCM.
 
Ni sawa kabisa, hata wajerumani tunawakumbuka na kuwaenzi sana sisi kama waTanzania kwa kutujengea miundombinu ya reli, MV Liemba ya ziwa Tanganyika nk.
Mjerumani alijenga huku akiiba mali zetu JPM amejenga kwa kutumia pesa zile zile zinazopangiwa matumizi mengi pengine akipuuzia malalamiko ya wa chini yake.
 
Kwa hiyo unajustify mauaji aliyoyafanya jpm kwa kusema hata mkapa alifanya au siyo!!
Hakuna rais wa TZ mwenye mikono misafi kabisa. Nyerere miaka ile alifanya unyama pia.

Pale wizara ya mambo ya ndani kule nyuma karibu na ukuta unaopakana na YMCA, kulikuwa na nyumba ya mabati yenye rangi nyekundu, uliza waliokuwepo miaka ile mle ndani palikuwa ni maalum kwa shughuli zipi.
 
Samia Hana mpango kabisa wa kuua .mtu ndo mana tunamuombe afie kwenye urais yaani atuongoze miaka mia ijayo
 
Wewe ndiye mwenye chuki dhidi ya viongozi wengine waliopita kama vile huyo unayemsifia alikuta nchi ni wonderland.
Kaacha meli ziwa victoria hapo sijaongelea masuala ya ndege zaidi ya kumi na mengi mengineyo.
 
Duh we utakuwa TISS. Asante
 
Hitler alikuwepo kabla hujazaliwa! Idi Amin, Stalin na Saddam Hussein wanakumbukwa kila iitwayo kesho, sembuse Lucifer Magufuli wa juzi?!
Swali la kujiuliza ni je Hitler na Stalin, sadam, idi Amin nk wanakumbukwa kwa lipi, wema au ubaya?!

Lucifer Magufuli atakumbukwa sana kwa muda mrefu ujao ili taifa lisije kurudia makosa kama hayo milele!
 
Rais wa kwanza kuamua kufuta machozi ya wahanga wa ajali ya May 1996 kwa kufanya maamuzi magumu ya kutengeneza meli mpya yenya ubora mkubwa.

Marais wote hujenga vitu vingi kwa mujibu wa maelekezo ya ilani ya CCM.

Hata kusingekuwa na ilani unadhani miundombinu isingejengwa?
 
Mjerumani alijenga huku akiiba mali zetu JPM amejenga kwa kutumia pesa zile zile zinazopangiwa matumizi mengi pengine akipuuzia malalamiko ya wa chini yake.

Zile pesa zilizopelekwa China kuna tofauti gani na hizo za hao wakoloni? Na hao wajerumani waliiba nini sana nchi hii, mbona wameondoka zaidi ya miaka 100 na bado nchi hii ni masikini na mali walizoacha? Au walituibia na akili?
 
Nchi hii ni maskini kwa sababu mimi na wewe tunapiga mdomo tu bila hata ya kujitoa kupambana na huo umaskini. Pesa ya China ni sehemu ndogo sana kulinganisha na inayotumika kumalizia treni ya SGR, ni sehemu ndogo sana kulinganisha na ujenzi wa hiyo meli ya Ziwani.

JPM anastahili heshima kwa uthubutu wake, mengineyo ni siasa nyepesi tu.
 
Weka tija ya hizo ndege hapa. Unaweza kuweka ni kiasi gani hadi sasa zimeingiza kama faida? Mbona ziko grounded muda mrefu?
Masuala ya muda kuwa grounded, ni mchakato mkuu kuziendesha, haziendeshwi kwa porojo za humu ndani JF.
 
Kwani wale tuliokuwa tunawatuhumu kabla ya Magufuli kuwa ni wezi, waliiba hela zote, na hakuna mradi wowote walifanya?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…