Hayati Magufuli huwezi kusahaulika kwa miaka mingi sana kwa Meli kubwa Ziwa Victoria

Sukuma gang mna taabu sana, hakuna raisi atakayesahaulika ila huyo Jiwe atakumbukwa pia kwa ubishi wa kupingana na wataalam wa mambo ya afya huku aking'ang'ania malimao na vitunguu saumu kama tiba ya COVID-19 kitu kilichosababisha yeye kuwa raisi wa kwanza kufia madarakani tena kwa uzembe wake mwenyewe na pia atakumbukwa kwa ukatili uliokithiri.
Hiyo meli kama mengine yaliyofanywa na maraisi wengine hakuna hata raisi mmoja aliyetoa pesa zake za mfukoni bali ni pesa za kodi za wananchi, ni mara mia hata kuisifu kampuni iliyounda hiyo meli(japo nao hawakufanya bure,walilipwa kwa kazi hiyo), Jiwe alikuwa mwehu ila alifanikiwa ku-brainwash mazuzu ambao hadi leo wanamuona ni mungu mtu na hata madhila aliyowasababishia watu hatafuta namna ya kuya-justify.
 
Meli imejengwa kwa pesa za watanzania kazi akiifanya mama. Yeye hakuifikia hata 10% ya ujenzi acheni upoyoyo
Si Samia wala Jiwe waliojenga ile meli, meli imejengwa(imeundwa) na kampuni ya nje kwa malipo ya fedha za walipa kodi.
Mwandawazimu/Mwendakuzimu aliharibu sana mazuzu mpaka pesa za kodi za wananchi waliona ya kwamba ni fedha zake binafsi, yaani kwamba fedha zilizokuwa hazina ilikuwa kama ni personal account yake.
 
Hiyo si justification ya lile zimwi Jiwe kuwa katili kwa kiwango kile, bora lilikufa mapema otherwise lingesababisha madhara makubwa zaidi.
 
Weka tija ya hizo ndege hapa. Unaweza kuweka ni kiasi gani hadi sasa zimeingiza kama faida? Mbona ziko grounded muda mrefu?
Zinasubiri maonyesho ya ndege hizo
 
Jiwe alikuwa mpigaji haijawahi kutokea
 
Ni rahisi kuropoka maneno ukiwa nyuma ya keyboard mbali kabisa na shida za usafiri za watu wa kanda ya ziwa,

Unajua idadi kamili ya waliokufa siku ile pale ziwani wakati meli ilipozama?.
Heee!!sasa kufa kwa watu miaka 27 iliyopita inahusiana vipi na hii meli?kwani si kulikuwa na mv.serengeti na mv.victoria?ziwa victoria hakuna shida ya usafiri kiasi hicho na toka kumekuwa na usafiri wa mabus kwenda bk meli tena imekuwa sio kipaumbele!!kuna miaka kama 2 hakukuwa na usafiri wa meli kati ya mza na bk lakini wakati victoria inafanyiwa matengenezo makubwa na haikuleta athari kubwa!!nenda ziwa tanganyika huko ndio utaona shida ya usafiri.
 
Tatizo sio kutoa pesa zake mfukoni, tatizo ni kupambana mpaka miradi ikamilike. Tatizo ni uthubutu wake binafsi anapotaka jambo lake litimie. Uwezo wa kuamua kuwa Dodoma itakuwa ndio makao makuu na ikawa hivyo, uwezo wa kutatua matatizo ya kirasimu yanayochukua miaka na miaka pasipo kujali watanionaje.

Alikuwa binadamu na hakusita kutukumbusha juu ya ubinadamu wake kwamba yatupasa kunyenyekea muda wote.
 
Hebu tukumbushane na meli ya Bagamoyo. Ilinunuliwaje na inafanya kazi wapi kwa sasa
 
Hebu tukumbushane na meli ya Bagamoyo. Ilinunuliwaje na inafanya kazi wapi kwa sasa
Nenda katafute rekodi za kiserikali. Nimeleta huo uzi kwa heshima ya wengi walioteseka hapo ziwani kwa miaka mingi.

JPM na madhambi yake yote kwa kujenga hiyo meli ameliweka hai jina lake miongoni mwa watu wa kanda ya ziwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…