Hayati Magufuli kaacha legacy mbaya sana kwenye usalama wa nchi hii!

Umetoa hoja yenye uhalisia kabisa, japo wasiowaza wanaweza kupata shida kukuelewa. Mara nyingi namna ya kutawala ni usimikaji unaoenda kudumu kwa miaka kadhaa.

Kwa sababu utawala ni mfumo na uongozi ni team, kwa maana ya kwamba namna ya kutawala huwa inaanzia juu na kushuka chini hadi mitaani na kujikita.

Mifano iko DRC, Liberia, Uganda, na hata Rwanda itaendelea kuwa hivyo kwa miaka mingi zaidi. Namna hiyo ya utawala haiwezi kuja na kutoka tu kama chakula tumboni.

Hivyo, mwendazake kwa kukaa miaka 6 pale kwenye kiti, ilitosha kusimika namna hii ya ajabu ya kuongoza nchi na itadumu kwa muda mrefu kila ikihitajika suluhisho dhidi ya wapinzani wa kisiasa wa mtawala.

Athari ni kubwa, na zitachukua muda mrefu kuondoka, ama zitadumu milele.

Ova
 
Inawezekana una tatizo binafsi na hayati JPM sio bure.

JPM hayupo miaka mitatu na ushee sasa aliowaacha kwenye nafasi zao wote walitolewa na huyo mama yenu wakawekwa hao mliompendekezea wawekwe sasa kuanza kutupa lawama kwa JPM asiyekuwepo na unamwacha aliyekalia kiti tena juzi kasimama hadharani mbele ya vyombo vya dola na kuonesha rangi yake halisi leo unaleta ujinga wako hapa?!

Wakati wa JPM hayakuwepo mambo ya kijinga kama yaliyopo , yeye alikuwa anashughulikia viashiria vya matukio hatarishi kweli sio ya kujitengezea.

Wimbi la kupotea watu zamu hii ni kubwa sana tena kwenye mambo mengine ya kitoto.
You must be kidding to switch your blame to someone already exterminated by yourself.

There shall be nobody to stain JPM's legacy for the next fifty years to come----period
 
Muache Jiwe apumzike kwa amani. Pambana na hao mlio nao kwa sasa. Siyo sikila kitu umtwishe Magu. Yeye hajawachagulia huyo miliye naye na wala hiyo Katiba hakuitunga yeye. Lawama kama zinapaswa kubebwa basi ni kwa Watanzania wote kwa kuruhusu kuendelea kuwa na Katiba hiyo mbovu ambayo inawapa mamlaka na nguvu za kuptiliza kwa hao viongozi wabaya
 
Gen Z Kenya waliingia mtaani pamoja na mikwara ya askari, na baadhi yao waliuawa na wengine kwa mamia kukamatwa.

Lawama kwa Magufuli kwa uovu mnaofanyiwa leo wakati Magufuli hayupo ni mkakati usioweza kuwasaidia.
Mpaka hapo Chadema na wafuasi wake, hatakuja kusamehewa na kuelweka kwa Watanzania , mpaka hapo watakapokuwa wameacha kuelekeza lawama za matatizo yao yote kwa hayati JPM. Kiukweli ni kwamba the more they direct everything evel to JPM, the more they become less appealing to the citizens. Huu mzumu wa JPM utaendelea kuwasumbua na kuteka mawazo yao yote to the extent ya kupoteze focus to the current issues and challenges of today that they are expected to address.
 
Chadema haitawashi kusameheka kwa watanzania kwa namna walivyokebehi na kusherehekea Kifo cha Shujaa. Acha simba jike awakomeshe mlimuona kama tumanini jipya kwenu na kuungana katika kumlaumu Jiwe on everything . Tumaini lenu liko wapi sasa?
Magufuli hayupo we Mbweha! Juzi kati hapa si mlisema nchi imeponywa!? Na si iliponywa na watu wazima kabisa?

Sasa Leo Magufuli anaingiaje hapo?

Kila mtu abebe mzigo wake mwenyewe. Magufuli mlimbebesha wa kwako na huyu abebe wa kwake!!
 
Sio chama, wananchi, vijana wenye uchungu na Taifa wanaweza kufanya hivyo. Kenya, Sri Lanka, Bangladeshi ni mifano. wamefanya hivyo. Baadaye wanaanzisha chama. Mwanzo itakuwa coalition ya wazalendo wote.
Hiyo ndiyo njia pekee kulikomboa taifa.
 
Unategemea nini kama Bashite,Musiba,Sabaya,Ali Hapi wote wamerudi...Hao jamaa wamefanya umafia sana kipindi cha JIWE kwa kujilimbikizia mali kwa mgongo wa KIKOSI KAZI -TASK FORCE.
Tokea bashite karudishwa na hapi tunashuhudia utekaji na mauaji ya raia wa upand e wa pili
 

Ukweli mtupu
 

Sasa kuengua wapinzani ndiyo utamaduni mpya🤦🏾‍♂️
 
Ahsante muanzisha Uzi kwa kuliona Hilo. Sasa hivi hata yule asiye kichaa kama alivyokuwa Magufuli, akishika Madaraka atakanyaga mule mule alimopita Magufuli.
 
Inaonekana hujui mambo mengi sana bwana mdogo. Sheria ya TRA ya kufunga akaunti ya Benki ya mteja anayedaiwa kodi ipo miaka mingi sana kabla ya JPM hajawa Rais, pia simu kusikilizwa haijaanzishwa na JPM ipo miaka mingi tangu mawasiliano yaanzishwe duniani ila wewe uelewa wako ni mdogo tu ndio maana unasema hivyo. Kusikilizwa maongezi search Snowden wa USA kwenye Google utajua hata mabeberu ya USA yanafanya sana tu. Hata kwenye mitandao unaangaliwa kila wakati usifikiri uko free kiasi hicho pia kasome kanuni za ITU utajua jinsi Dola inavyoweza ingilia mawasiliano yako. Unafikiri Interceptor zilitengenezwa kwa ajili gani? Endelea kulala usingizi wa pono mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…