Hayati Magufuli kaacha legacy mbaya sana kwenye usalama wa nchi hii!

Hayati Magufuli kaacha legacy mbaya sana kwenye usalama wa nchi hii!

Tatizo nyie Chadema wanaowasikiliza na kuwaelewa ni wachache sana Tanzania ni watoto wenzenu wa mjini 20% ya nchi. 80% walimwelewa Magufuli sababu waliona tofauti kwenye maisha yao kama kupata maji, umeme, barabara, shule, hospitali, kusikilizwa na matatizo yao, kulinda haki zao za msingi kama ardhi, nyumba, biashara zao, maslahi ya maskini.
 
Hakuna chama hicho duniani kinaweza kufanya yote hayo. Palestina anapigana mwenyewe wakati Isreal kapewa silaha zote za dunia huku wao wanapambania ardhi na Allah atawapa ushindi na kuweka heshima ya nchi yao.

Sio chama, wananchi, vijana wenye uchungu na Taifa wanaweza kufanya hivyo. Kenya, Sri Lanka, Bangladeshi ni mifano. wamefanya hivyo. Baadaye wanaanzisha chama. Mwanzo itakuwa coalition ya wazalendo wote.
 
Hata samia kaanzia kuwika awamu yake ujue. Anyway ni kilianzia sio kiliansia punguza kutetemeka mkuu
Mbona mengine mnasema Kila kitu kiliansia kwake? Kwa nini kwenye kupanda mbegu za uovu mnataka kumsafisha 😂😂

Wengine wanasema Toka mtoto pendwa arudi kwenye maamuzi ,tumerudi tulikotoka.
 
Magufuli hayupo we Mbweha! Juzi kati hapa si mlisema nchi imeponywa!? Na si iliponywa na watu wazima kabisa?

Sasa Leo Magufuli anaingiaje hapo?

Kila mtu abebe mzigo wake mwenyewe. Magufuli mlimbebesha wa kwako na huyu abebe wa kwake!!

Walisema nchi imefunguliwa... Sijui kutoka wapi.
 
Sijasema wamerudishwa nimesema kaacha maana yake wapo kama alivyo waacha na kaacha mfano mbaya sana na unatuletea matatizo zaidi hata yaliyo kuwepo
Mkuu umeeleza jambo muhimu sana. Usiopoteze muda kubishana au kuelewesha kila mtu hapa. Wako wengi wasio na uwezo wa kuona mantiki ya mambo. Akili zao zimegota kwenye tribal politics na personality cult worship. Hata useme nini hawawezi kukuelewa. Hawajui kuwa legacy za watu kama Christopher Columbus na Julius Caesar zinachambuliwa hadi leo.

Nyerere mwenyewe alilalamika sana kuwa maRais waliomfuatia na wafuasi wao walichukua mambo mabaya ya utawala wake na kuacha mazuri. Na ndio kinachoendelea.

Yale mambo ya kikatili yanayohakikisha utawala wa CCM na makundi yake unabaki madarakani (by hooks and crooks) yanakumbatiwa sana hadi sasa. Ushabiki wa wananchi wa tribal politics na personality cult worship zinasaidia watawala kuendeleza maovu. Ndio msiba mkubwa wa Taifa hili (national tragedy) nyakati hizi. Hadi siku watu wengi watakapoamka kuelewa uhalisia wa mambo.
 
Hawa usalama na Polisi ni magufuli ndiyo alianzisha haya mambo ambayo tusipokuwa makini yatatuletea machafuko TZ. Kuwa aminisha Polisi waweze kuiba kura, kuaminisha usalama kusiliza simu za watu ovyo ovyo bila amri ya mahalama, TRA na usalama kufunga account za watu za bank bila kibali cha mahakama, usalama kuweka uchawa na kuteka na kuuwa watu bila kuwa na uchunguzi

Sasa tunaona matokeo yake. Hapa kuna ambao walikuwa wanaunga mkono kila kitu sasa ndiyo mnaona tuliyokuwa tunasema matatizo ya kuanzisha vitu vibaya vitaendelea hata kama haupo.

Huyu Mama anajaribu kuiga iga bila kujua yeye hana wasukuma na teknologia imebadilika sana. Nyakati hizi Watanzania huwezi kuwadanganya kirahisi na ndiyo maana wapinzani wanaeleweka maana uwazi umeongezeka sana.

Video mpaka vijijini siku hizi. Huwezi kudanganya watu tena kwamba wapinzani ni mabeberu kama wakati ule au Tanzania hakuna Corona!

Magufuli alifanya mazuri lakini kwenye mfumo wa serikali na demokrasia kafanya vibaya kuliko mtu mwingine yeyote!

Screenshot_2024-09-23-08-36-05-710_com.android.chrome.jpg
 
Back
Top Bottom