Hayati Magufuli kwanini alificha jalada la ununuzi wa ndege?

Hayati Magufuli kwanini alificha jalada la ununuzi wa ndege?

Sifa kubwa ya madikteta ni usiri na kuficha mambo ya umma kama masuala binafsi.

Ndivyo ilivyokuwa kwa Mwendazake wakati anafanya mpango wa kununua ndege...

Why unatuuliza sisi?

Makamu wa rais wa awamu ya tano humjui? Waziri mkuu wa awamu ya tano humjui?

Why usiende kuwauliza wao?

Mnatengeneza mazingira ya kuonekana magu alikuwa ni one man show me siamini

Kama magu alifanya makosa basi yalikuwa ya wote serikali mzima

Na kama magu alikuwa dicteta then ni serikali ya awamu ya tano wote
 
Sifa kubwa ya madikteta ni usiri na kuficha mambo ya umma kama masuala binafsi.

Ndivyo ilivyokuwa kwa Mwendazake wakati anafanya mpango wa kununua ndege...
Kwenye hii Habari ambayo ni muhimu sana hata sehemu moja hujataja source halisi ya Habari, wala hata hujaleta evidence yoyote ile, umefikiria tu na kuandika.

Huyo Rais mwenye kuficha mafaili ataficha mafaili mangapi? Kwapani? Kabatini, hana hata secretary?

Tujifunze evidence, evidence ---- na tuogope kusema uongo, kuna 10 commandments (amri kuu za Mungu) mojawapo usiseme uongo!
 
Narudia tena aliyeweka hilo takes hakua mjinga. Teteeni panapofaa. Penye walakini nyoosheni mikono mkemee. Halafu kwa upumbavu unafikiri biashara ya kimataifa unafanya kwa sport money...
Ona sasa huyu.

Ulitaka anunue kwa mkopo huku keshi anayo?

Kichwa chako kishaanza kumezwa na wadwanzi bila wewe kujua. Ukabila unaujua wewe?. Wasukuma wangapi walikuwa pale ikulu?. Mko sensitive na mambo ya kijinga sana mmaacha ya maana.
 
Ona sasa huyu.
Ulitaka anunue kwa mkopo huku keshi anayo?

Kichwa chako kishaanza kumezwa na wadwanzi bila wewe kujua. Ukabila unaujua wewe?. Wasukuma wangapi walikuwa pale ikulu?. Mko sensitive na mambo ya kijinga sana mmaacha ya maana.
Siku ukisoma international finance ndo utanielewa. Ukiwa mbumbumbu wa vitu usidakie dakie tu. Sijasema mkopo nimesema huwezi kulipa cash upfront. Huo ni ujinga. Unalia on delivery. Not siku ya kuorder.
 
Siku ukisoma international finance ndo utanielewa. Ukiwa mbumbumbu wa vitu usidakie dakie tu. Sijasema mkopo nimesema huwezi kulipa cash upfront. Huo ni ujinga. Unalia on delivery. Not siku ya kuorder.
Ona sasa unavyojichanganya?. Unalia hukupewa mkataba. Hayo ya kulipa umeyajuaje?
 
Same old story everyday, hebu tutajie mkataba mmoja tu uliowahi kuwekwa wazi na serikali ya CCM tukauona?

Ukishindwa kufanya hivyo, tujibu; kwanini tusiamini nyie wapinzani maslahi mnatumiwa na walamba asali ili kufanikisha malengo yao?
CAG has unrestricted access to all contracts entered by the government. If some are hidden, it raises questions
 
Zile ndege ilikuwa wizi mtupu bin ujambazi bin ufisadi bin ujangili!

Anyway, Mola alishamaliza kesi yetu ila tuzidi kumlaani milele!
 
Kwenye hii Habari ambayo ni muhimu sana hata sehemu moja hujataja source halisi ya Habari, wala hata hujaleta evidence yoyote ile, umefikiria tu na kuandika...
Braza vote(kasma) ya ikulu ulishawahi kuona ukaguzi wake? Ukitaka kuficha kitu Tanzania hii kipeleke ikulu. Ukaguzi wa vote ya ikulu hata ukifanyika hauwekwi hadharani.

Je ndege Zina umuhimu Gani huo mpaka ziwekwe kwenye kasma inayokaguliwa bila kutolewa taarifa hadharani?
 
Jamani Mtamuuwa Mara Ya Pili Mzilankende Mnyago
 
Sifa kubwa ya madikteta ni usiri na kuficha mambo ya umma kama masuala binafsi.

Ndivyo ilivyokuwa kwa Mwendazake wakati anafanya mpango wa kununua ndege...
Hizi ndege ni janga kubwa kitaifa, mengi mtayajua baadaye.
 
Braza vote(kasma) ya ikulu ulishawahi kuona ukaguzi wake? Ukitaka kuficha kitu Tanzania hii kipeleke ikulu. Ukaguzi wa vote ya ikulu hata ukifanyika hauwekwi hadharani. Je ndege Zina umuhimu Gani huo mpaka ziwekwe kwenye kasma inayokaguliwa bila kutolewa taarifa hadharani?
Suala sio ndege kupelekwa ikulu swala ni Ndege kua chini ya Tanzania Government Flight Agency (TGFA) shirika ambalo lipo chini ya Ikulu na ambalo linasimamia ndege zote za serikali, na kwa mfumo uliopo sasa ndege zote zinazonunuliwa na serikali zipo chini ya TGFA then zinakua leased kwa ATCL hii iliwekwa makusudi kuzuia makosa yaliyofanyika kati ya ATC na SA airline yasijirudie, km mnataka zisiwe chini ya ikulu lipelekeni hilo shirika likawe chini ya wizara ili watu wakibinafsisha tena ATCL ndege zipotee tena km za ATC.

come to issue ya pili, 2yrs now jamaa hayupo si muweke mafaili hadharani au mlimzika jamaa na mafaili yake?
And vp kuhusu ndege hizi mpya 5 mafaili yake CAG ameshapewa au mama anatembea nayo?

Kuna double standard moja ya kijinga sana inafanyika now dys tena on purpose, hebu muwapimie hawa maraisi vipimo sawa mnapo wa critisize, sio mmoja akifanya inakua kesi mweingine akifanya its okay kisa tu mna chuki binafsi.
 
Swala sio ndege kupelekwa ikulu swala ni Ndege kua chini ya Tanzania Government Flight Agency (TGFA) shirika ambalo lipo chini ya Ikulu na ambalo linasimamia ndege zote za serikali...
Kama suala ni umiliki wa GFA hata sasa tuna ndege imeshikiliwa uwanja wa ndege uholanzi. Hata ukiweka chini ya ikulu lazima tu zishikwe maana inayoshitakiwa ni Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kwenye suala la kufungua account hata tukifungua Leo mtasema tunamuonea maana hayupo hai.

Pia kitengo hicho kilikua wizara ya uchukuzi kabla ya 2018. Nini kilimpelekea kukipeleka ikulu?
 
Back
Top Bottom