Hayati Magufuli: Ni mara kumi nikachunge kule kijijini kuliko kuwa Rais na kuliuza Taifa

Hayati Magufuli: Ni mara kumi nikachunge kule kijijini kuliko kuwa Rais na kuliuza Taifa

Kati ya hasara Taifa la Tanzania lilipata ni kumpoteza Mzalendo Hayati John Pombe Joseph Magufuli hapo March, 2021.

Itatuchukua muda mrefu sana kukaa sawa.
 
Tulishatoka utumwani kwa lile shetani lenu la Chato.
Twamuomba sana Mungu asitupe tena jaribu la kutuletea jitu hatari kama lile
Tusiwaone hapa mnaleta mjadala wa bandari tulieni mnyooshwe na bi mkora!
 
C kila mwenye ubongo ana akili!! Rudi kusoma context yang tena!! Hakuna sehem nimesema bora kuuza Nchi.
Binadamu hawezi kuwa na pande mbili ama atakuwa na front and hind.

Ama Magufuli hafai au anafaa.

Ukikifikiria kitu kwa makini ama utakikataa au kuunga mkono.

Ila bakaa ya maneno: ukiwa umembaini adui ukitaka kumtumia akili nyingi utamsamehe. Maoni sahihi: Ama Magufuli alikuwa sahihi ama laa.

Wanao uza nchi wapo sawa kabisa. Watu wazuri walipata muda wao wa kuitetea nchi. Waliofikiri wana maarifa makubwa wakakataa kwa kufiri Kuna njia mbadala na ambayo ni hii.
 
"Unapoona Wananchi wanashangaa shangaa sana, hawakuzoea ninayoyafanya, walijua nitakuwa sehemu ya wezi, NEVER, sio Mimi. Ni mara kumi nikachunge kule kijijini kuliko kuwa Rais na kuliuza Taifa, ninasema hapana"

Hayati Rais John Pombe Magufuli.

View attachment 2689631
Hizi ni mbinu chafu za wapinzani wa DPW kujifanya wanamkumbuka sana JPM, huyu hayati Magufuli ndiye aliyejenga reli ya SGR kwenda Kigali na imekula trilioni 17 mpaka muda huu inapokaribia kumalizika.

Angekuwa yupo hai muda mrefu sana wangeshasaini mikataba pale ikulu na muda huu zingekuwa zinaendelea nyimbo za mapambio ya hicho kilichosainiwa. Hawezi kujitetea maskini ya Mungu kwani ameshaondoka.

Hawezi kuidhinisha ujenzi wa reli hiyo ya matrilioni tena akivumilia matusi ya hawa hawa wanaojifanya kumsifu leo kinafiki tu, halafu aone eti kuleta mwekezaji bandarini ni kuuza nchi, that is bull shit.

JPM alikuwa na akili ya kimaendeleo kuliko wengi wetu hapa Tanzania, alitaka sana kuimarisha ushoroba wa kati akifahamu ushindani wa kina Angola na bandari zingine afrika.
 
Bandari day 22 July
 

Attachments

  • IMG-20230716-WA0843.jpg
    IMG-20230716-WA0843.jpg
    247.4 KB · Views: 7
Back
Top Bottom