Huyu mnayemkumbuka ndiyo kasabababisha yote haya,Mama kakuta kikapu hakina kitu hali ya Uchumi ni Mbaya sasa ataongeza kutoka wapi?Hata hicho alichoongeza kwa hali aliyoikuta kajitahidi sana tusimvunje Moyo.
Waliokosea ni washauri wake wa Kisiasa kufanya siasa katika hili kwa kutangazatangaza bila kutoa Elimu au uelewa kwa Wafanyakazi,kilichotokea Wafanyakazi wakajenga Matumaini makubwa sasa hivi wamepigwa na kitu kizito wana hasira nao wanaweza kurudisha kitu kizito kitu ambacho kisiasa ni hatari.
Haya Majedwali ya Viwango vya nyongeza wanayohaha kuyasambaza sasa hivi wanakosea its too late,hii kazi ilitakiwa ifanyike kipindi hicho watu waelewe wanachopata wasijenge matumaini,huku ni kuvuta shuka wakati kumekucha.
Hapa inatakiwa akili kubwa ikae itafutwe Calculation nzuri ya kucounter attack hii reaction ya Watumishi.