Hayati Magufuli: Ningeweza kusema ninawaongeza mshahara halafu nikaongeza elfu tano tano

Hayati Magufuli: Ningeweza kusema ninawaongeza mshahara halafu nikaongeza elfu tano tano

Alichokifanya Samia ni sawa kabisa, mwenye mshahara mdogo kapata ongozeko la 23%, hivi mtu wa chini aliyepanga chumba cha 50,000 leo kaongezewa 80,000 kwenye mshahara hajapata uwezo wa kupanga vyumba viwili?
Sisi wachini tunamshukuru sana rais Samia
 
Huyu mnayemkumbuka ndiyo kasabababisha yote haya,Mama kakuta kikapu hakina kitu hali ya Uchumi ni Mbaya sasa ataongeza kutoka wapi?Hata hicho alichoongeza kwa hali aliyoikuta kajitahidi sana tusimvunje Moyo.

Waliokosea ni washauri wake wa Kisiasa kufanya siasa katika hili kwa kutangazatangaza bila kutoa Elimu au uelewa kwa Wafanyakazi,kilichotokea Wafanyakazi wakajenga Matumaini makubwa sasa hivi wamepigwa na kitu kizito wana hasira nao wanaweza kurudisha kitu kizito kitu ambacho kisiasa ni hatari.

Haya Majedwali ya Viwango vya nyongeza wanayohaha kuyasambaza sasa hivi wanakosea its too late,hii kazi ilitakiwa ifanyike kipindi hicho watu waelewe wanachopata wasijenge matumaini,huku ni kuvuta shuka wakati kumekucha.

Hapa inatakiwa akili kubwa ikae itafutwe Calculation nzuri ya kucounter attack hii reaction ya Watumishi.
Kwani yeye alipoingia 2015 alikuta kuna mzigo kiasi gani? Halafu Yeye alifariki ghafla huko ndani kulikuwa na kitu
 
Alichokifanya Samia ni sawa kabisa, mwenye mshahara mdogo kapata ongozeko la 23%, hivi mtu wa chini aliyepanga chumba cha 50,000 leo kaongezewa 80,000 kwenye mshahara hajapata uwezo wa kupanga vyumba viwili?
Sisi wachini tunamshukuru sana rais Samia

hivi kima cha chini ni watumishi wa idara gani???

maana wanaopokea mishahara ya kwapa ni polisi na waalimu,wameongezewa 60 elfu.
 
Back
Top Bottom