Hayati Mkapa ni aina ya wanaume wachache wenye misimamo migumu kwenye mahusiano

Hayati Mkapa ni aina ya wanaume wachache wenye misimamo migumu kwenye mahusiano

Paploman

JF-Expert Member
Joined
Apr 13, 2019
Posts
1,759
Reaction score
3,452
Kwa Kheri mzee wetu Mkapa, Mungu akurehemu huko uendako.

Nimevaa viatu vya mzee Mkapa kwenye mahusiano yake yenye moyo wa kipekee, havinitoshi kabisa na sio mimi tu karibia wanaume wengi wa karne hii hawawezi kuwa na ujasiri wa moyo kama aliokuwa nao huyu mzee wetu ni wa kipekee kabisa.

Hebu fikiria amemchukua Anna Kama mpenzi wake baada ya kumzidi kete Basil Pesambili Mramba akiwa tayari ana mtoto wa kiume wa Mramba, Hilo kwake mzee lilikuwa ni jambo dogo na kuona haikuwa na noma kabisa kwake akamfanya Mramba kuwa rafiki yake wa Karibu.

1995 Anagombea Urais, Alishawishi na kumpigia kampeni kabambe Mramba ili ashinde Ubunge Rombo na aliposhinda akamteua kuwa Waziri wa Fedha huku akiendelea kuwa mshikaji wake wa karibu Nje ya majukumu ya kikazi na hata kazini, Mkapa alikuwa anamuamini sana Mramba.

Katika hali ya kawaida wewe unaweza kufanya hivi kwa EX aliyezaa na mke wako? na ukawa unaenda nae kwako kama rafiki yako wa karibu sana? Mkapa bado anakuwa mwanaume wa kipekee sana sio tu kwenye siasa ukomavu wake wa kidiplomasia aliuhamishia hadi kwenye mahusiano

Pamoja na hayo Mtoto wa Mramba waliyezaa na Anna amekulia kwa Mkapa na Mzee alimpenda sana.

Ni wanaume wachache sana wanaoweza kufanya hivi. Hata mimi siwezi kufanya haya aliyofanya mzee wetu Mkapa

Upumzike kwa amani Mwamba.
 
Mkuu....
Wanaume wengi wenye misimamo isiyo yumbishwa mbele za watu, wanakuaga wadhaifu sana na wanyonge kwenye mahusiano yao.
Na hata alipo chapwa stuli na kuvunjika mguu, bado aliweza kuvumilia tu.
(Naomba nisimtaje jina)
 
Maisha ya huyo mzee hayaeleweki mkuu, labda angetusimulia mwenyewe, jana nimesoma stori anasimulia rafiki wake wa toka utotoni amesema yeye ndiye alimkutanisha Anna na mkapa na yeye ndiye alimpanga Anna hadi akakubali kuwa na Mkapa wakiwa bado vijana wanasoma, sasa unavosema Anna alikua na Mpenzi mwingine haieleweki
 
maisha ya huyo mzee hayaeleweki mkuu, labda angetusimulia mwenyewe, jana nimesoma stori anasimulia rafiki wake wa toka utotoni amesema yeye ndiye alimkutanisha Anna na mkapa na yeye ndiye alimpanga Anna hadi akakubali kuwa na Mkapa wakiwa bado vijana wanasoma, sasa unavosema Anna alikua na Mpenzi mwingine haieleweki
Samahani mkuu....
Hivi unaishi Tz ama De'Congo..??
Maana nisije nikajikuta nakukosea adabu kwa kukushangaa...[emoji69]
 
maisha ya huyo mzee hayaeleweki mkuu, labda angetusimulia mwenyewe, jana nimesoma stori anasimulia rafiki wake wa toka utotoni amesema yeye ndiye alimkutanisha Anna na mkapa na yeye ndiye alimpanga Anna hadi akakubali kuwa na Mkapa wakiwa bado vijana wanasoma, sasa unavosema Anna alikua na Mpenzi mwingine haieleweki
😛😛
Anna ana mtoto mkubwa kwa Mramba mkuu na tena alikuwa mkurugenzi wa Kampuni kubwa iliyoletaga utata kidogo
 
Mkuu....
Wanaume wengi wenye misimamo isiyo yumbishwa mbele za watu, wanakuaga wadhaifu sana na wanyonge kwenye mahusiano yao.
Na hata alipo chapwa stuli na kuvunjika mguu, bado aliweza kuvumilia tu.
(Naomba nisimtaje jina)
Mkuu misimamo mbele za watu ina mahusiano na udhaifu kwenye mahusiano?

Mbona mama Anna anaonekana mpole sana haha
 
😛😛
Ana ana mtoto mkubwa kwa Mramba mkuu na tena alikuwa mkurugenzi wa kubwa iliyoletaga utata kidogo
Ongea polepole chief, bado hata hatuja maliza kumhifadhi mzee...[emoji69][emoji69]
 
Pole yao sana wafiwa...

Hapo kosa siyo la marehemu... hapo kosa na la mwanamke kukubali...



Cc: mahondaw
 
Na wewe ndo walewale.
Kipindi yupo hai ulikuwa wapi kuyasema hayo.
Mtu akifa mnajifanya kumjua sana, mwacheni apumuzike maneno hayataondoa wala kubadili chochote.
Safari njema Mkapa
Kwani nimemsema vibaya mkuu?
 
Kukosa utu siyo sifa nzuri kuonesha jamii, ingekuwa busara kama ungeficha unyama wako ulionesha kwenye uzi huu. Haya yote uliyoandika ni ya uzushi na laana itakushukia.
 
Back
Top Bottom