Hebu piga picha kama Tundu Lissu asingerudi

Hebu piga picha kama Tundu Lissu asingerudi

Bila Lissu manyanyaso kwa wapinzani yangekuwa ya kutisha zaidi ya tunavyoshuhudia kwa sasa.
Kampeni pia zingekuwa zimepoa Sana.
Bila Lissu waliobaki wote ni mawakala wa Chama Tawala, hakuna ambaye angeguswa kama ilivyo sasa. Unaona wanaguswa ? Labda ACT - Wazalendo kidogooo.
 
Shida ya Tanzania, akili maiti ni nyingi mno...hata akina kalamaganda, pamoja na upolofesa wake, ni akili maiti tu.
Mpaka wana ccm wenyewe hawakuwa na amani na Magufuli kiasi cha kuishi kwa tabu sana kwenye shughuli zao za kila siku.
 
Si kurudi Tanzania tu, mi nafikiri mbali zaidi na kusema je kama Lissu angekufa baada ya lile shambulio..

Yaani hali ingekuwa ni mbaya ziadi ya kile kipindi cha ukoloni.
Kwa akili yako, amesaidia nini? Ana nini kutusaidia watanzania?
 
Napiga picha.. nawona hasingepata pesa za beberuz.. na picha zaidi anafurahia pesa.. zaidi ya cheo.. anachojuwa hatakipata..
 
Aliyetaka kumuua Lisu Ni mtu ambaye alishatabiri haya na kwamba dawa yoyote isingefanya kitu Bila kumpoteza.Mungu Ni mkubwa Sana ,hata shetani haruhusiwi kuua Ni laana mbaya Sana hasa kwa mtu asiye na hatia.ona sasa kinachofanyika sioni hata picha moja ya Lisu mitaani likini huwezi amini.ama kweli binadamu hupanga Bali mwamuzi Ni MUNGU.AMINA
 
Na ndio maana wakamuacha arudi wangeweza kumzia kutokurudi ila walijua uchaguzi ungepoa mno.
 
Na ndio maana wakamuacha arudi wangeweza kumzia kutokurudi ila walijua uchaguzi ungepoa mno.
Walikubali arudi kwa hiari yao? Acha upuuzi Mkuu, kurudi kwa Lissu ni SHINIKIZO kutoka huko duniani.
 
Kwa kweli Tz ingekua nchi moja ya kifala sn bila uwepo wa Tundu Lissu
 
Mimi na wengine wengi tulishaamua kwamba hatutakwenda vituoni kupiga kura. Nikifikiria zile chaguzi ndogo za marudio na ule uchaguzi wa serekali za mitaa, ukisikia ba kauli za hovyo toka kwa kiba Ndugai na kina kibajaji na Msukuma, unakatishwa tamaa kwa kiwango kikubwa kabisa.
Ila sasa, tumeamua kwenda kupiga kura, tutapiga kura na kuzilinda. Tunahitaji viongozi jasiri wa aina ya lissu. Nakuhakikishieni huku nilipo kura za lissu ni za kumwaga. Shida nayoiona ni kule tume. Watamtangaza?
 
Shida ya Tanzania, akili maiti ni nyingi mno...hata akina kalamaganda, pamoja na upolofesa wake, ni akili maiti tu.
Ukweli mchungu wasomi wetu wengi ni waoga na wanafki . Wengi ni kujikomba kwa ajili ya vyeo na madaraka.
 
Mungu ni MKUU na akiamua kitu basi no body can do or say anything, Huwa najaribu kufikiri kua zile risasi 16 zilizomwingia na hakufa bado wakati kuna watu wanapigwa ka risasi kamoja tu wanakata moto on the spot, Nakosaga majibu ya kidunia na nabaki kumwamini Mungu ndio alitenda hii miujiza...

Mpaka muda huu sijapataga kujua hawa watu wasiojulikana ni kina nani? Au TZ siku hizi tunaishi na Aliens.? Naamini hata hao aliens tunaowaskiaga, hawawezi kutenda unyama ka ule dhidi ya binadamu...

Kumepoa sana asaiv bila kusikia kampeni za Lissu, Nilikua nimezoea kumskiza jamaa, sema tar 9 keshokutwa tu...
 
Back
Top Bottom