Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,843
- 31,057
Hakuna mashaka yoyote kuwa katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu, mchuano mkali sana wa kinyang'anyiro hicho cha urais utakuwa baina ya vyama viwili ambavyo ni CCM na CHADEMA.
Kwa maana hiyo ni lazima sisi wananchi tufuatilie kwa makini sana, kwa wagombea wa Urais wa vyama hivyo viwili vikuu, pale wanapomwaga sera zao kwa ajili ya uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi Oktoba mwaka huu.
Kwa bahati nzuri Mimi mwenyewe nilihudhuria na kushuhudia kampeni ya Urais aliyofanya mgombea wa CHADEMA Tundu Lissu hapo jana katika viwanja vya Tanganyika packers Kawe.
Miongoni ya yale aliyoahidi kupitia kwenye ilani ya chama chake cha CHADEMA ni kama haya yafuatayo:-
1.Wafanyakazi wote ambso hawajaongezewa mishahara yao kwa kipindi chote cha miaka 5, ambayo ni kwa mujibu wa sheria atawaongezea na kulipa malimbikizo yote ya miaka 5.
2. Fao la kujitoa kwa watumishi amesema atalirejesha na akasema wazi kuwa siyo sahihi kwa mfanyakazi anayeacha kazi kusubiria akiba yake aliyoweka kwenye mifuko ya kijamii hadi afike miaka 60.
3. Atawalipa wananchi wote walioathirika na ubomoaji wa nyumba zao, mathalani wakazi wa Kimara hadi Kibaha, kwa lengo la kupisha upanuzi wa barabara ya njia 8 na akaendelea kusema kuwa wananchi hao walifanyiwa huo wakati wananchi hao walilifikisha suala lao mahakamani na mahakama hiyo ikawa imetoa "stop order" lakini serikali haikujali zuio hilo la mahakama na ikaendekea na ubabe wake wa kuzibomoa nyumba hizo bila kulipa fidia yoyote.
4. Ameahidi kurejesha utawala wa sheria nchini, ambao kwa Maelezo yake ni kuwa utawala huu, wa serikali ya awamu ya 5 umeamua kuzikanyaga kanyaga.
6. Ameahidi pia iwapo chama chake kitapewa ridhaa na wananchi kwa kushinda uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi oktoba mwaka huu, nchi yetu itakuwa na Katiba mpya inayotokana na Rasimu ya Warioba ambayo wanaccm waliivuruga
7. Amesema kuwa atarekebisha mfumo wa kodi ambao anasema wafanyibiadhara wanatozwa kodi nyingi sana hadi kufikia kodi 16, na akaahidi kuwa atarekebisha mfumo huo wa kodi na kuwa rafiki kwa wafanyibiashara na kumfanya mfanyibiashara alipe kodi moja pekee.
8 Vile vile ameelezea kuwa atawapiga marufuku TRA kuwabambikia kodi kubwa kwa hila, wafanyibiashara wanaodaiwa kuwa wanawasaidia wapinzani, jambo ambalo limewafilisi wafanyibiathara wengi hapa nchini.
9 Pia amesema atarejesha Uhuru wa wananchi kupata habari, badala ya mfumo uliopo kwenye utawala huu, kwa vyombo vya habari vingi kufungiwa na kupigwa faini, kutokana na sheria mpya kandamizi ya maudhui ya habari iliyopitishwa "fasta fasta" na Bunge letu kwa hati ya dharula
10. Kupunguza malipo ya Bodi ya mikopo kwa wanafunzi waliomaliza vyuo vyao, kutoka asilimia 15 kutoka katika mishahara yao hivi sasa hadi asilimia 3
Hayo ni baadhi ya mambo yaliyo kwenye ilani ya Chadema, ambayo sera zake alizinadi kwenye viwanja vya Tanganyika Packers jana.
Hebu tutazame na ilani ya CCM kama alivyoinadi mgombea wake John Magufuli hapo jana, ambapo nilibahatika kuisikiliza hotuba yake kupitia kwenye "video clip" aliyoitoa kule Dodoma
1. Alisema atajenga uwanja mkubwa pale Dodoma katika awamu ijayo baada ya kuona uwanja wa Jamhuri hautoshi kutokana na watu kufulika Jana kuja kusikiliza ufunguzi wa kampeni za CCM.
2 Vile vile aliahidi kuongeza kununua ndege nyingine 5 za abiria katika awamu ijayo kwa madai kuwa ndege zilizopo hivi sasa hazitoshi na nchi yetu ni tajiri kwa hiyo tunao uwezo wa kufanya manunuzi hayo kwa pesa "cash"
3. Aliahidi pia katika awamu ijayo atajenga uwanja wa ndege wa kimataifa hapo msalato kwa kile alichodai kuwa hiyo Dodoma ishakuwa ni mji mkuu, kwa hiyo kunahitajika ndege kubwa za kutua kwenye mji huo
4 Kama kawaida yake pia aliahidi pia ataendelea kujenga miundo mbinu ya barabara za lami zitakazoenea nchi nzima.
Hebu sisi wananchi tutafakari kwa makini ni yupi hapo tumpe kura zetu na aingie Ikulu.
Kila la kheri wananchi na mtumie vyema kura zenu kwa manufaa yenu na vizazi vijavyo.