Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hakuna mashaka yoyote kuwa katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu, mchuano mkali sana wa kinyang'anyiro hicho utakuwa baina ya vyama viwili ambavyo ni CCM na CHADEMA.
Kwa maana hiyo ni lazima sisi wananchi tufuatilie kwa makini sana, kwa wagombea wa Urais wa vyama hivyo viwili vikuu, pale wanapomwaga sera zao kwa ajili ya uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi Oktoba mwaka huu.
Kwa bahati nzuri Mimi mwenyewe nilihudhuria na kushuhudia kampeni ya Urais aliyofanya mgombea wa CHADEMA Tundu Lissu hapo jana katika viwanja vya Tanganyika packers Kawe.
Miongoni ya yale aliyoahidi kupitia kwenye ilani ya chama chake cha CHADEMA ni kama haya yafuatayo:-
1.Wafanyakazi wote ambso hawajaongezewa mishahara yao kwa kipindi chote cha miaka 5, ambayo ni kwa mujibu wa sheria atawaongezea na kulipa malimbikizo yote ya miaka 5.
2. Fao la kujitoa kwa watumishi amesema atalirejesha na akasema wazi kuwa siyo sahihi kwa mfanyakazi anayeacha kazi kusubiria akiba yake aliyoweka kwenye mifuko ya kijamii hadi afike miaka 60.
3. Atawalipa wananchi wote walioathirika na ubomoaji wa nyumba zao, mathalani wakazi wa Kimara hadi Kibaha, kwa lengo la kupisha upanuzi wa barabara ya njia 8 na akaendelea kusema kuwa wananchi hao walifanyiwa huo wakati wananchi hao walilifikisha suala lao mahakamani na mahakama hiyo ikawa imetoa "stop order" lakini serikali haikujali zuio hilo la mahakama na ikaendekea na ubabe wake wa kuzibomoa nyumba hizo bila kulipa fidia yoyote.
4. Ameahidi kurejesha utawala wa sheria nchini, ambao kwa Maelezo yake ni kuwa utawala huu, wa seikali ya awamu ya 5 umeamua kuzikanyaga kanyaga.
6. Ameahidi pia iwapo chama chake kitapewa rifhaa na wananchi kwa kushinda uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi oktoba mwaka huu, nchi yetu itakuwa na Katiba mpya inayotokana na Rasimu ya Warioba ambayo wanaccm waliivuruga
7. Amesema kuwa atarekebisha mfumo wa kodi ambao anasema wafanyibiadhara wanatozwa kodi nyingi sana hadi kufikia kodi 16, na akaahidi kuwa atarekebisha mfumo huo wa kodi na kuwa rafiki kwa wafanyibiashara na kumfanya mfanyibiashara alipe kodi moja pekee.
8 Vile vile ameelezea kuwa atawapiga marufuku TRA kuwabambikia kodi kubwa kwa hila, wafanyibiashara wanaodaiwa kuwa wanawasaidia wapinzani, jambo ambalo limewafilisi wafanyibiadhara wengi hapa nchini.
9 Pia amesema atarejesha Uhuru wa wananchi kupata habari, badala ya mfumo uliopo kwenye utawala huu, kwa vyombo vya habari vingi kufungiwa na kupigwa faini, kutokana na sheria mpya kandamizi ya maudhui ya habari iliyopitishwa "fasta fasts" na Bunge letu kwa hati ya dharula
10. Kupunguza malipo ya Bodi ya mikopo kutoka asilimia 15 kutoka kwenye mishahara yao hivi sasa hafi asilimia 3
Hayo ni baadhi ya mambo yaliyo kwenye ilani ya Chadema, ambayo sera zake alizinadi kwenye viwanja vya Tanganyika Packers jana.
Hebu tutazame na ilani ya CCM kama alivyoinadi mgombea wake John Magufuli hapo jana, ambapi nilibahatika kuisikiliza hotuba yake kupitia kwenye "video clip" aliyoitoa kule Dodoma
1. Alisema atajenga uwanja mkubwa pale Dodoma katika awamu ijayo baada ya kuona uwanja wa Jamhuri hautoshi kutokana na watu kufutika Jana kuja kusikiliza ufunguzi wa kampeni za CCM.
2 Vile vile aliahidi kuongeza kununua ndege nyingine 5 za abiria katika awamu ijayo kwa madai kuwa ndege zilizopo hivi sasa hazitoshi na nchi yetu ni tajiri kwa hiyo tunao uwezo wa kufanya manunuzi hayo kwa pesa "cash"
3. Aliahidi pia katika awamu ijayo atajenga uwanja wa ndege wa kimataifa hapo msalato kwa kile alichodai kuwa hiyo Dodoma ishakuwa ni mji mkuu, kwa hiyo kunahotajika ndege kubwa za kutua kwenye mji huo
4 Kama kawaida yake pia aliahidi pia ataendelea kujenga miundo mbinu ya barabara za lami zitakazoenea nchi nzima.
Hebu sisi wananchi tutafakari kwa makini ni yupi hapo tumpe kura zetu na aingie Ikulu.
Kila la kheri wananchi na mtumie vyema kura zenu kwa manufaa yenu na vizazi vijavyo
miaka 60 kwa ccm inatosha, tujaribu sera mbadala.
Hela ya ndege 5 na kujenga airport, Barbara ipo ya kutosha ila ya mishahara na maslahi ya watu itengezwe mbinguni! Mm naona tuache kupenda chama na Tujali maslahi ya watu kwanza.Kiongozi umeisoma ilani ya Chama Cha Mapinduzi!? Kwanza!?
Pili Hakuna Haki Bila Wajibu... Na Serikali haitengenezi fedha toka Mbinguni.. Ni Kama kuendesha duka tu..lazima unapoanza ujitoe kweli kweli uwekeze upunguze matumizi.
Ukishafanikiwa unaweza Hata kukaa nyumbani na bado ukala. Wakayi issue ya ubungo kimara ilitolewa ufafanuzi kwa mujibu wa mpango kabambe wa jiji wa mwaka 1979..imekwisha prescribe upana ROW ya Barabara hiyo.
Utaratibu wa watu kuvamia na wanasiasa kuwa pressure watumishi kuwamilikisha kwa ajili ya kupata kura ndicho kilichotufikisha hapa. Lakini Kama mpango upo lazima ufuatwe huo ndio utawala wa haki na sheria.
Lissu anatuambia atalipa malimbikizo na fidia kwa watu waliovamia mbona tutakuwa masikini siku tatu, Sio kitu kibaya kupandisha mishahara na kulipa malimbikiz, ila kwa Sasa Ni kwa fedha ipi!?
Kwann tusitengeneze Kwanza hiyo nyingi kwakuwekeza Kama kweli tunataka longevity kwenye hayo mafao!? Au tulipane ikiisha tukae tuangaliane!?
Kwa kipindi hiki nakushauri soma ilani ..achana na maneno ya jukwaani.. kila mtu anataka kuonekana mwema atasema chochote kuvutia.. despite the facts saying otherwise.
Issue ya Ndege Tano iko kwenye mpango wa upanuzi wa Shirika.. nne za abiria na Freight Jet Moja. Kwa ajili ya kusaidia katika usafirishaji wa mizigo.
Uwanja mkubwa Dodoma ni pamoja na kwa matumizi ya dhifa za kitaifa now we have moved Government operations to Dodoma.
Ila sema ni uchaguzi time anything can be said anyhow.!
Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
Hamna hela mnagombana tu mwisho mtauza ghorofa mpate hela!!!Halafu Baba Mwenye Ghorofa aliyewalisha nyasi anakufa anamanlizia nyasi.. anawaachia grorofa mnaendelaje kula kuku mpaka mnazeeka... No pain No Gain.. iko hivyo toka Beginning of times.
Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
Kubomoa nyumba za Kimara/Mbezi bila fidia ilikuwa kukurupuka kwa kuwa stop order ilikuwa imeishatolewa na mahakama.Kiongozi umeisoma ilani ya Chama Cha Mapinduzi!? Kwanza!?
Pili Hakuna Haki Bila Wajibu... Na Serikali haitengenezi fedha toka Mbinguni.. Ni Kama kuendesha duka tu..lazima unapoanza ujitoe kweli kweli uwekeze upunguze matumizi.
Ukishafanikiwa unaweza Hata kukaa nyumbani na bado ukala. Wakayi issue ya ubungo kimara ilitolewa ufafanuzi kwa mujibu wa mpango kabambe wa jiji wa mwaka 1979..imekwisha prescribe upana ROW ya Barabara hiyo.
Utaratibu wa watu kuvamia na wanasiasa kuwa pressure watumishi kuwamilikisha kwa ajili ya kupata kura ndicho kilichotufikisha hapa. Lakini Kama mpango upo lazima ufuatwe huo ndio utawala wa haki na sheria.
Lissu anatuambia atalipa malimbikizo na fidia kwa watu waliovamia mbona tutakuwa masikini siku tatu, Sio kitu kibaya kupandisha mishahara na kulipa malimbikiz, ila kwa Sasa Ni kwa fedha ipi!?
Kwann tusitengeneze Kwanza hiyo nyingi kwakuwekeza Kama kweli tunataka longevity kwenye hayo mafao!? Au tulipane ikiisha tukae tuangaliane!?
Kwa kipindi hiki nakushauri soma ilani ..achana na maneno ya jukwaani.. kila mtu anataka kuonekana mwema atasema chochote kuvutia.. despite the facts saying otherwise.
Issue ya Ndege Tano iko kwenye mpango wa upanuzi wa Shirika.. nne za abiria na Freight Jet Moja. Kwa ajili ya kusaidia katika usafirishaji wa mizigo.
Uwanja mkubwa Dodoma ni pamoja na kwa matumizi ya dhifa za kitaifa now we have moved Government operations to Dodoma.
Ila sema ni uchaguzi time anything can be said anyhow.!
Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
Hapo kinachomkomboa mwananchi ni kumjengea miundombinu rafiki ambayo itamuwezesha kufanya shughuli zake za uzalishaji kirahisi na hiyo ni sera ya jpm ambayo hukuiandika umeoina ya ndege tu kwa sababu huna hela ya kupanda ndege ili watu waseme ndege hazisaidii mbona hukueleza yote?Uhuru, Haki na Maendeleo ya wananchi.
VS
Ununuzi wa ndege.
Ipi sera nzuri hapo ya kumkwamua mwananchi kutoka kwenye lindi la umasikini unaomkabili?
Utaratibu wa kununua Ardhi nchini upo wazi kabisa, Jiridhishe serikalini.. na sheria ni msumeno.. kwa kipindi chote wanasiasa ndio waliokuwa wanakwepesha utekelezaji wake..Kubomoa nyumba za Kimara/Mbezi bila fidia ilikuwa kukurupuka kwa kuwa stop order ilikuwa imeishatolewa na mahakama.
Pili ilikuwa kudharau muhimili mwingine ilitakiwa wahusika wapelekwe lupango.
Tatu nani wa kulaumiwa kati ya serikali na hao wananchi waliobomolewa nyumba?
Kuna wapuuzi wanadai kulikuwa na ushahidi wa beacon zilizochimbiwa ardhini?
Kwanini serikali haikuweka mabango katika maeneo haya kuwajulisha kuwa hiyo ni reserve ya barabara kama mataifa mengine yanavyofanya?
Kwani serikali miaka yote ilikuwa wapi wakati wizara za ardhi zilikuwa kilometer chache tu?
Endekezeni hizo roho mbaya za kufikiri unawakomoa wananchi kumbe serikali inajikomoa yenyewe kwani serikali ni watu.
Wewe huli ubwabwa ? Sera zinalenga kutatua matatizo ya wananchi, wananchi wengi tunapambana na njaa, kupata chakula cha siku ni shida.Huyo Rungwe naye anataka tu kupata "airtime"
Hivi tangu lini kula ubwabwa ikawa ndiyo Sera kuu ya chama cha siasa?
Wewe hutetei sheria bali unatetea nguvu bila sheria.Utaratibu wa kununua Ardhi nchini upo wazi kabisa, Jiridhishe serikalini.. na sheria ni msumeno.. kwa kipindi chote wanasiasa ndio waliokuwa wanakwepesha utekelezaji wake..
Hakuna anayefurahia chochote na Wala hakuna swala la roho mbaya.. imekuwa kawaida yetu watanzania kwenda kinyume na makubaliano(sheria) halafu baadae tunataka tuhalalishe makosa ..sheria haiko hivyo.. itakuja na kukutafuna Hata Kama miaka 40 imepita.
Wananchi tunahadaika kirahisi Sana na wanasiasa wa kupita kisa tunataka urahisi..kudekezwa.. kama umenunua Ardhi nchi popote pale inakutaka ufike kwenye mamlaka ya upangaji na Usimamizi (Halmashauri) wangapi watasema hawakuwahi huambiwa eneo Lile ni barabarani!?
Sheria sio za matajiri ..wala masikini pekee..sio za walalahoi wala wafanyakazi pekee.. sheria ni kwa ajili yetu sote.. haijalishi unacho au hauna... Sheria Ikianza kuchagua na kubagua basi imefail na tumefail Kama taifa..
Sheria is universal ndani ya nchi hii ukijenga barabarani utatoka. Uwe nani usiwe Nani na ukijenga bondeni utatoka, na tunakokwenda ukijenga bila kupanga au kupata kibali utakuwa punished. Shida sio kuoneana ni.kuwa na watu wenye utaratibu na taifa lenye utaratibu na linafuata misingi ya utawala wa kisheria.
Huwezi kuongoza kundi kwa kuangalia wachache wanataka nn.. ukienda hivyo Ni hao.wachache ambao hawajui picha ya sehemu kubwa ndio watakao ongoza hilo kundi. Utajenga mpasuko... be a man and take full responsibility.. Unataka watu wakosee halafu uwareward!? Seriously!?
Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
1979 hakukuwa na watu mule. Watumishi wa serikali na wanasiasa wamekosea.. wakawahadaa wananchi... Sasa tunataka Barabara yetu.. unatushauri tuwawajibishe Wanasiasa na wataalamu wataweza kuilipa hiyo fidia!?Wewe hutetei sheria bali unatetea nguvu bila sheria.
Stop order ilitolewa na mahakama lakini ikatumika misuri bila sheria nyumba zikavunjwa.
Sasa kama unaheshimu sheria kama unavyodai kwanini hukusubiri mahakama yenye mamlaka ya kutafsiri hoja kisheria ikafanya kazi yake?
Nani alikupa mamlaka ya mahakama kama si kuingilia muhimili mwingine?
Tuache kujidanganya kwa kukumbatia jaziba visasi na unafiki,nakuhakikisha ubomoaji wa Kimara ipo siku haki itatendeka iwe kesho hata baada ya miaka 50.
Wewe unazuga ,unakwepa hoja ya msingi.1979 hakukuwa na watu mule. Watumishi wa serikali na wanasiasa wamekosea.. wakawahadaa wananchi... Sasa tunataka Barabara yetu.. unatushauri tuwawajibishe Wanasiasa na wataalamu wataweza kuilipa hiyo fidia!?
Hebu ngoja nikuelewe...Sie tuko Mlele huku tunataka shule ya sekondari na kituo cha sfya.. halafu Ninyu mko daslama mnavamia maeneo ya barabara yaliyotengwa tayari... Halafu serikali hiii hii tunayoilipa kodi mimi na wewe ikulipeni ninyi kwa makosa yenu ...wakati huo sisi tusiokosea tuendelee kusubiri huduma zetu?
Acha mzaha bwana. Huo ni wizi na sio wa kuentertain kabisa. Yaani ukosee tuchukue kodi tukugawia kwa makosa yako!?
Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
Katiba hiyo hiyo ndiyo inayoestablish sheria za Ardhi.. kwa mujibu wa sheria ya Ardhi "makazi asilia" tu ndio yanapaswa kuheshimiwa na mipango mipya.. na Kama mwananchi alifanya Maendelezo (of which wengi waendeleza baada ya sheria kutungwa) anapaswa kufuata taratibu kama zilivyokua prescribed.Wewe unazuga ,unakwepa hoja ya msingi.
Umeshindwa kuheshimu katiba tuliotunga sisi wenyewe.Umedharau mahakama,umejitwisha kazi ya mahakama isio yako.Kwa ufupi umevunja sheria.
Kura yangu itaenda kwa aliyeahidi maendeleo ya watanzania ambayo ndiyo chachu ya maendeleo ya Tanzania yenyewe. Hata principle ya kiuchumi inasema kwanza maendeleo ya watu then vitu (Economic growth -> economic develipment)Hakuna mashaka yoyote kuwa katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu, mchuano mkali sana wa kinyang'anyiro hicho cha urais utakuwa baina ya vyama viwili ambavyo ni CCM na CHADEMA.
Kwa maana hiyo ni lazima sisi wananchi tufuatilie kwa makini sana, kwa wagombea wa Urais wa vyama hivyo viwili vikuu, pale wanapomwaga sera zao kwa ajili ya uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi Oktoba mwaka huu.
Kwa bahati nzuri Mimi mwenyewe nilihudhuria na kushuhudia kampeni ya Urais aliyofanya mgombea wa CHADEMA Tundu Lissu hapo jana katika viwanja vya Tanganyika packers Kawe.
Miongoni ya yale aliyoahidi kupitia kwenye ilani ya chama chake cha CHADEMA ni kama haya yafuatayo:-
1.Wafanyakazi wote ambso hawajaongezewa mishahara yao kwa kipindi chote cha miaka 5, ambayo ni kwa mujibu wa sheria atawaongezea na kulipa malimbikizo yote ya miaka 5.
2. Fao la kujitoa kwa watumishi amesema atalirejesha na akasema wazi kuwa siyo sahihi kwa mfanyakazi anayeacha kazi kusubiria akiba yake aliyoweka kwenye mifuko ya kijamii hadi afike miaka 60.
3. Atawalipa wananchi wote walioathirika na ubomoaji wa nyumba zao, mathalani wakazi wa Kimara hadi Kibaha, kwa lengo la kupisha upanuzi wa barabara ya njia 8 na akaendelea kusema kuwa wananchi hao walifanyiwa huo wakati wananchi hao walilifikisha suala lao mahakamani na mahakama hiyo ikawa imetoa "stop order" lakini serikali haikujali zuio hilo la mahakama na ikaendekea na ubabe wake wa kuzibomoa nyumba hizo bila kulipa fidia yoyote.
4. Ameahidi kurejesha utawala wa sheria nchini, ambao kwa Maelezo yake ni kuwa utawala huu, wa serikali ya awamu ya 5 umeamua kuzikanyaga kanyaga.
6. Ameahidi pia iwapo chama chake kitapewa ridhaa na wananchi kwa kushinda uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi oktoba mwaka huu, nchi yetu itakuwa na Katiba mpya inayotokana na Rasimu ya Warioba ambayo wanaccm waliivuruga
7. Amesema kuwa atarekebisha mfumo wa kodi ambao anasema wafanyibiadhara wanatozwa kodi nyingi sana hadi kufikia kodi 16, na akaahidi kuwa atarekebisha mfumo huo wa kodi na kuwa rafiki kwa wafanyibiashara na kumfanya mfanyibiashara alipe kodi moja pekee.
8 Vile vile ameelezea kuwa atawapiga marufuku TRA kuwabambikia kodi kubwa kwa hila, wafanyibiashara wanaodaiwa kuwa wanawasaidia wapinzani, jambo ambalo limewafilisi wafanyibiathara wengi hapa nchini.
9 Pia amesema atarejesha Uhuru wa wananchi kupata habari, badala ya mfumo uliopo kwenye utawala huu, kwa vyombo vya habari vingi kufungiwa na kupigwa faini, kutokana na sheria mpya kandamizi ya maudhui ya habari iliyopitishwa "fasta fasta" na Bunge letu kwa hati ya dharula
10. Kupunguza malipo ya Bodi ya mikopo kwa wanafunzi waliomaliza vyuo vyao, kutoka asilimia 15 kutoka katika mishahara yao hivi sasa hadi asilimia 3
Hayo ni baadhi ya mambo yaliyo kwenye ilani ya Chadema, ambayo sera zake alizinadi kwenye viwanja vya Tanganyika Packers jana.
Hebu tutazame na ilani ya CCM kama alivyoinadi mgombea wake John Magufuli hapo jana, ambapo nilibahatika kuisikiliza hotuba yake kupitia kwenye "video clip" aliyoitoa kule Dodoma
1. Alisema atajenga uwanja mkubwa pale Dodoma katika awamu ijayo baada ya kuona uwanja wa Jamhuri hautoshi kutokana na watu kufulika Jana kuja kusikiliza ufunguzi wa kampeni za CCM.
2 Vile vile aliahidi kuongeza kununua ndege nyingine 5 za abiria katika awamu ijayo kwa madai kuwa ndege zilizopo hivi sasa hazitoshi na nchi yetu ni tajiri kwa hiyo tunao uwezo wa kufanya manunuzi hayo kwa pesa "cash"
3. Aliahidi pia katika awamu ijayo atajenga uwanja wa ndege wa kimataifa hapo msalato kwa kile alichodai kuwa hiyo Dodoma ishakuwa ni mji mkuu, kwa hiyo kunahitajika ndege kubwa za kutua kwenye mji huo