Uchaguzi 2020 Hebu tutafakari sera zinavyonadiwa na mgombea wa CCM John Magufuli na yule wa CHADEMA Tundu Lissu


Lissu hana uwezo wa kuongoza hata wilaya moja. Usimlinganishe na bulldozer. Magufuli ndo muarobaini wa maendeleo ya nchi, sio vibaraka.
 
Kwa JPM huna haja ya kutafakari. Kila mwenye macho na aone. Macho hayadanganyi.
 
Mystery ,

..Jpm katoa boko kwenye ufunguzi wa kampeni za ccm.

..vijana wa ccm wanasubiri mkutano ujao labda atarekebisha.
Hakika kila mwenye macho atakuwa ameona..................

Akilinganisha alivyojinadi Magufuli na avyojinadi Tundu Lissu, kura inabidi umpe Tundu Lissu
 
Hela ya ndege 5 na kujenga airport, Barbara ipo ya kutosha ila ya mishahara na maslahi ya watu itengezwe mbinguni! Mm naona tuache kupenda chama na Tujali maslahi ya watu kwanza.

Mm kuishi kwa kujichunga ninachosema kila waikato nimechoka , tunataka uhuru na maendeleo ya watu na taifa yaende sambamba mana ata tujenge viwanda na miundombinu vipi kama watu hawana hela nchi hii haitaendelea.
 
Halafu Baba Mwenye Ghorofa aliyewalisha nyasi anakufa anamanlizia nyasi.. anawaachia grorofa mnaendelaje kula kuku mpaka mnazeeka... No pain No Gain.. iko hivyo toka Beginning of times.

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
Hamna hela mnagombana tu mwisho mtauza ghorofa mpate hela!!!

Msipigie chama kura, angalieni sera ya mgombea na utendaji kazi wake mana mtakuja kuambiwa kwani nilisema ntaleta tetemeko tena!!!!

#nchi hii ni ya mwananchi sio ya viongoz wa CCM kuwa lazima wao washike dola.
#mabadiliko yanaanza na ww mwananchi.
#we can dictate who is who October 2020.
 
Kubomoa nyumba za Kimara/Mbezi bila fidia ilikuwa kukurupuka kwa kuwa stop order ilikuwa imeishatolewa na mahakama.
Pili ilikuwa kudharau muhimili mwingine ilitakiwa wahusika wapelekwe lupango.

Tatu nani wa kulaumiwa kati ya serikali na hao wananchi waliobomolewa nyumba?
Kuna wapuuzi wanadai kulikuwa na ushahidi wa beacon zilizochimbiwa ardhini?
Kwanini serikali haikuweka mabango katika maeneo haya kuwajulisha kuwa hiyo ni reserve ya barabara kama mataifa mengine yanavyofanya?

Kwani serikali miaka yote ilikuwa wapi wakati wizara za ardhi zilikuwa kilometer chache tu?
Endekezeni hizo roho mbaya za kufikiri unawakomoa wananchi kumbe serikali inajikomoa yenyewe kwani serikali ni watu.
 
Uhuru, Haki na Maendeleo ya wananchi.
VS
Ununuzi wa ndege.

Ipi sera nzuri hapo ya kumkwamua mwananchi kutoka kwenye lindi la umasikini unaomkabili?
Hapo kinachomkomboa mwananchi ni kumjengea miundombinu rafiki ambayo itamuwezesha kufanya shughuli zake za uzalishaji kirahisi na hiyo ni sera ya jpm ambayo hukuiandika umeoina ya ndege tu kwa sababu huna hela ya kupanda ndege ili watu waseme ndege hazisaidii mbona hukueleza yote?
 
Utaratibu wa kununua Ardhi nchini upo wazi kabisa, Jiridhishe serikalini.. na sheria ni msumeno.. kwa kipindi chote wanasiasa ndio waliokuwa wanakwepesha utekelezaji wake..

Hakuna anayefurahia chochote na Wala hakuna swala la roho mbaya.. imekuwa kawaida yetu watanzania kwenda kinyume na makubaliano(sheria) halafu baadae tunataka tuhalalishe makosa ..sheria haiko hivyo.. itakuja na kukutafuna Hata Kama miaka 40 imepita.

Wananchi tunahadaika kirahisi Sana na wanasiasa wa kupita kisa tunataka urahisi..kudekezwa.. kama umenunua Ardhi nchi popote pale inakutaka ufike kwenye mamlaka ya upangaji na Usimamizi (Halmashauri) wangapi watasema hawakuwahi huambiwa eneo Lile ni barabarani!?

Sheria sio za matajiri ..wala masikini pekee..sio za walalahoi wala wafanyakazi pekee.. sheria ni kwa ajili yetu sote.. haijalishi unacho au hauna... Sheria Ikianza kuchagua na kubagua basi imefail na tumefail Kama taifa..

Sheria is universal ndani ya nchi hii ukijenga barabarani utatoka. Uwe nani usiwe Nani na ukijenga bondeni utatoka, na tunakokwenda ukijenga bila kupanga au kupata kibali utakuwa punished. Shida sio kuoneana ni.kuwa na watu wenye utaratibu na taifa lenye utaratibu na linafuata misingi ya utawala wa kisheria.

Huwezi kuongoza kundi kwa kuangalia wachache wanataka nn.. ukienda hivyo Ni hao.wachache ambao hawajui picha ya sehemu kubwa ndio watakao ongoza hilo kundi. Utajenga mpasuko... be a man and take full responsibility.. Unataka watu wakosee halafu uwareward!? Seriously!?

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Huyo Rungwe naye anataka tu kupata "airtime"

Hivi tangu lini kula ubwabwa ikawa ndiyo Sera kuu ya chama cha siasa?
Wewe huli ubwabwa ? Sera zinalenga kutatua matatizo ya wananchi, wananchi wengi tunapambana na njaa, kupata chakula cha siku ni shida.
 
Wewe hutetei sheria bali unatetea nguvu bila sheria.

Stop order ilitolewa na mahakama lakini ikatumika misuri bila sheria nyumba zikavunjwa.

Sasa kama unaheshimu sheria kama unavyodai kwanini hukusubiri mahakama yenye mamlaka ya kutafsiri hoja kisheria ikafanya kazi yake?

Nani alikupa mamlaka ya mahakama kama si kuingilia muhimili mwingine?

Tuache kujidanganya kwa kukumbatia jaziba visasi na unafiki,nakuhakikisha ubomoaji wa Kimara ipo siku haki itatendeka iwe kesho hata baada ya miaka 50.
 
1979 hakukuwa na watu mule. Watumishi wa serikali na wanasiasa wamekosea.. wakawahadaa wananchi... Sasa tunataka Barabara yetu.. unatushauri tuwawajibishe Wanasiasa na wataalamu wataweza kuilipa hiyo fidia!?

Hebu ngoja nikuelewe...Sie tuko Mlele huku tunataka shule ya sekondari na kituo cha sfya.. halafu Ninyi mko daslama mnavamia maeneo ya barabara yaliyotengwa tayari... Halafu serikali hiii hii tunayoilipa kodi mimi na wewe ikulipeni ninyi kwa makosa yenu ...wakati huo sisi tusiokosea tuendelee kusubiri huduma?

Acha mzaha bwana. Huo ni wizi na sio wa kuentertain kabisa. Yaani ukosee tuchukue kodi tukugawie kwa makosa yako!?

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Wewe unazuga ,unakwepa hoja ya msingi.
Umeshindwa kuheshimu katiba tuliotunga sisi wenyewe.Umedharau mahakama,umejitwisha kazi ya mahakama isio yako.Kwa ufupi umevunja sheria.
 
CCM ni vibaka hawana sera .....kwanza mgombea wao aliapa kuilinda katiba lakini kwa muda wake wote amekuwa anavunja katiba alioapa kuilinda!Wananchi tumenyang'anywa haki zetu z msingi kama kupata habari,kumiliki biashara halali,kupata matibabu,CCM wanaendekeza ukabila,wizi,upendeleo na rushwa ya ngono.(Kisarawe mpo)???na CCM inawadhalilisha akina mama.
 
Ilani ya ccm ya 2015 imetekelezwa chini ya 50% na baadhi ya sekta hali ni mbaya zaidi,mfano kituo cha afya kila kata,wamejenga na kukarabati 500 kati ya zaidi 3000 vinavyohitajika,zahanati kila kijiji haijatekelezwa.

Kuunganisha mikoa yote kwa barabara za lami hadi leo hii bado,,Tabora-Kigoma,Kigoma-Katavi,Rukwa-katavi,Rukwa-Tabora,,Mbeya-Tabora,Mbeya-Singida,Njombe-Morogoro,Ruvuma-Morogoro,Mara-Arusha,Simiyu-Singida/Arusha,Kagera-Kigoma kote huko ni mavumbi na kwingine kazi haziishagi toka enzi za JK.

Sekta ya kilimo ndio kabisaa hata bajeti ilipunguzwa sana ikilinganishwa na ile ya 2015..Chadema hizi ndio mambo za ku capitalize na kuchambua kuwaeleza watu kushindwa kwa ccm na uongo bila kusahau kutekeleza miradi isiyo na maana kama reli ,viwanja vya ndege,mastendi uchwara nk nk
 
Wewe unazuga ,unakwepa hoja ya msingi.
Umeshindwa kuheshimu katiba tuliotunga sisi wenyewe.Umedharau mahakama,umejitwisha kazi ya mahakama isio yako.Kwa ufupi umevunja sheria.
Katiba hiyo hiyo ndiyo inayoestablish sheria za Ardhi.. kwa mujibu wa sheria ya Ardhi "makazi asilia" tu ndio yanapaswa kuheshimiwa na mipango mipya.. na Kama mwananchi alifanya Maendelezo (of which wengi waendeleza baada ya sheria kutungwa) anapaswa kufuata taratibu kama zilivyokua prescribed.

Huwezi kuniambia few unlawful officers wakimlikisha mtu eneo la ikulu.. halafu tukamyanganya..akienda mahakamani watakataa kumsikiliza!?

Nope watamsikiliza ... maana anazo nyaraka za serikali zinazotosha kufungua kesi.. Sasa mchakato wa kuwatambua culprits na kuwawajibisha kisheria unaweza kuchukua muda ila kamwe hatashinda hiyo kesi Ili alipwe au apewe ebeo...never! anachoweza ni kupata ushahidi alitapeliwa. Na hicho ndicho wakazi wa Kimara wanachoweza kupata. Basi.

Hata hivyo huyu anayekwenda kuanza Ujenzi kwenye eneo bila kufuata taratibu (squatting) naye anavunja chungu au!? Maana it's like katiba ni kwa ajili ya kundi hilli ila si kwa kundi lile. Hiyo double standard ni mbaya sana kwa ustawi wa jamii yetu. Believe me.



Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Kura yangu itaenda kwa aliyeahidi maendeleo ya watanzania ambayo ndiyo chachu ya maendeleo ya Tanzania yenyewe. Hata principle ya kiuchumi inasema kwanza maendeleo ya watu then vitu (Economic growth -> economic develipment)
 
CCM hawana jipya. Ni Yale Yale ya 2015. Zitto kawachambua ahadi zao na utekelezaji.... Ni 31 % tu ndiyo wametekeleza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…