Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, John Heche Juni 25, 2026 kwenye mahojiano na kituo cha Redio, cha VOS amesema kuwa chama hicho hakiko tayari kuingia kwenye maridhiano yoyote na Chama Cha Mapinduzi (CCM) bila uwepo wa mpatanishi wa kimataifa (mediator) asiyekuwa na upande, akitolea mfano wa mifumo ya usuluhishi iliyowahi kutumika nchini Kenya na kwingineko duniani.
Heche amesisitiza kuwa ili maridhiano hayo yawe ya kweli na yenye tija, lazima mpatanishi huyo atoke katika taasisi kubwa kama vile Jumuia ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC), Umoja wa Afrika (AU), au Umoja wa Ulaya (EU). Amesema nchi ya Tanzania ni sehemu ya dunia, hivyo kuwepo kwa mpatanishi wa nje si jambo la kigeni, na amekosoa vikali mtazamo wa viongozi wanaodai kuwa kuwashirikisha wadau wa kimataifa ni "kupeleka mambo ya ndani nje ya nchi."
Soma: