Pre GE2025 Heche: CHADEMA haitashiriki Uchaguzi wowote kama Mazingira ya Siasa yatabaki kama yalivyo sasa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826

''Msimamo wetu bado ni huo, kutokana na mazingira tuliyopitia mwaka 2019 na mwaka 2020 yalitudhihirishia wazi kwamba hatutashiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka huu (2024) kutokana na yale yaliyotokea yanatupa hofu kwenda kushiriki Uchaguzi tena, lakini kama kuna mambo yatabadilika na Miswada ikiwemo vipengele vya Katiba vinavyokwaza uchaguzi kuwa huru sisi tutakuwa tayari kushiriki uchaguzi" -Heche

John Heche ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA amezungumza hayo wakati akifanya mahojiano maalumu na EATV kupitia Kipindi cha Ahadi Timilifu leo, Jumatatu Januari 15.2024
 
Msimamo sahihi katika wakati sahihi.
Shida ni kwamba ni ndani ya chadema kuna wengi sana wana uchu wa kuwa wabunge bila kujali lolote lile mfano ningependa kujua msimamo wa Sugu ,Lema !
Chadema imechelewa sana kuweka msimamo huu! Huu msimamo ulitakiwa kuwekwa bayana mbele hata ya Samia na ni mambo na vipengele vilitakiwa kuwepo kwenye maridhiano!
 
Hawana huo uwezo hata siku moja,
Wajaribu waone watavyofutika, ACT atapewa majimbo kibao na ndo itakuwa kifo cha CHADEMA
 
Sawa, but better late than never.
 
Heche umekosea sana!

"Chadema haitoshiriki uchaguzi wowote hadi katiba mpya yenye maoni ya wananchi kwenye rasimu ya warioba ipatikane"!!

Kauli hiyo ndio pekee dola ingeelewa!!!
 
kwani Chadema ndio chama pekee cha siasa Tanzania?
 
Hawana huo uwezo hata siku moja,
Wajaribu waone watavyofutika, ACT atapewa majimbo kibao na ndo itakuwa kifo cha CHADEMA
Sio rahisi kama unavyofikiria, nchi sio ya mtu mmoja au kikundi cha watu fulani wenye maamuzi tu yote kama wanavyojitahidi kuwaaminisha kuna sheria za ndani na za nje zinzozimulika za ndani kama tochi. Consequencies zake zina impact wengi na sio wachache.
 
Ni kweli, ule haukuwa uchaguzi bali UHUNI wa CCM.
 
hi sasa ishakuwa kawaida yenu kila zikaribiapo chaguzi mmekuwa mnatafuta sababu ya kukimbia chaguzi ili kuficha anguko lenu
 
Mimi nime muelewa kwani tangu mwanzo huo ndio msimamo wangu hata kama asingesema
 
Ndio vizuri kwani wanamkomoa nani labda?

Kwani bila Chadema hakuna Tanzania?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…