Heche: Chadema Mwenyekiti wake ni Mbowe, akanusha kuwepo kambi ya Lissu na Mwenyekiti

Kama unautaka uenyeakiti wa CHADEMA, ukifika wakati wa uchaguzi, nenda ukajaze fomu. Lakini ufahamu uongozi kwenye vyama vya upinzani ni tiketi ya kwenda jela wakati wowote, kubambikiwa kesi, kufilisiwa, na wakati mwingine hata kuuawa.

Afadhali CHADEMA huwa wana uchaguzi wa kumchagua mwenyekiti, kuliko CCM ambako wanachama wamenyimwa haki ya kumchagua mwenyekiti, eti aliyetangazwa na tume kuwa Rais, ndiye automatically ni mwenyekiti wa CCM..
Ipo siku mwenekiti wa ccm atakuwa mpinzani kwa kupenda kwao kinga ya dola
 
Hawa viongozi wa siasa wamekuwa wakifikiri kwamba bado kuna watz ambao ni mazuzu wa kuendelea kuwadanganya na kuwahadaa kama miaka ile.

Mwaka 2015, wakati mh Lowassa alipokatwa makusudi na CCM tetesi zilianza kuvuma kuwa mheshimiwa huyo anajiandaa kukimbilia katika chama kimoja wapo cha upinzani kati ya ACT Wazalendo au Chadema.

Ghafla viongozi wa Chadema hivi hivi mfano wa Heche wakajitokeza na kuanza kupinga kwa kuwatoa hofu wanachama wao kuwa Chama hicho hakiwezi kufanya kosa hilo la karne la kumkaribisha fisadi Lowassa ndani ya chama chao, na kwamba kama akihamia upinzani basi ataenda ACT Wazalendo ambacho ni chama alichokianzisha mwenyewe ili akikatwa akimbilie huko.

Muda ni mwl mzuri, baada ya muda mheshimiwa akamwaga mkwanja kupitia mlango wa uwani wa mwenyekiti na genge lake.

After that kila mtu anakumbuka kilichotokea na wale wote waliopinga tetesi hawakujitokeza kukanusha tena walichokipinga 🤣🤣🤣🤣

Siasa za Tanzania bila unafiki kwa kweli haziendi maana wajinga na wadanganyika ni wengi mno kuliko wajanja.
Wewe ni mjumbe wa kamati yeyote kwenye hicho chama, au ni mwanachama. Vyama vyote vya siasa vinachukuliana watu, mfano ,Silinde, Waitara ,naibu Waziri wa afya, Gekulu hizo ndo siasa kama Kuna mtu anaweza kuwasaidia kupata jambo Fulani mnamchukua jambo lenu litimie. Siasa inahitaji mipango na mikakati Ili muweze kufikia malengo yenu. Katika siasa lengo la kwanza ni wanasiasa kunafaika mwisho ndo tunafuata sisi wafuasi/wananchi.
 
Hawa viongozi wa siasa wamekuwa wakifikiri kwamba bado kuna watz ambao ni mazuzu wa kuendelea kuwadanganya na kuwahadaa kama miaka ile.

Mwaka 2015, wakati mh Lowassa alipokatwa makusudi na CCM tetesi zilianza kuvuma kuwa mheshimiwa huyo anajiandaa kukimbilia katika chama kimoja wapo cha upinzani kati ya ACT Wazalendo au Chadema.

Ghafla viongozi wa Chadema hivi hivi mfano wa Heche wakajitokeza na kuanza kupinga kwa kuwatoa hofu wanachama wao kuwa Chama hicho hakiwezi kufanya kosa hilo la karne la kumkaribisha fisadi Lowassa ndani ya chama chao, na kwamba kama akihamia upinzani basi ataenda ACT Wazalendo ambacho ni chama alichokianzisha mwenyewe ili akikatwa akimbilie huko.

Muda ni mwl mzuri, baada ya muda mheshimiwa akamwaga mkwanja kupitia mlango wa uwani wa mwenyekiti na genge lake.

After that kila mtu anakumbuka kilichotokea na wale wote waliopinga tetesi hawakujitokeza kukanusha tena walichokipinga 🤣🤣🤣🤣

Siasa za Tanzania bila unafiki kwa kweli haziendi maana wajinga na wadanganyika ni wengi mno kuliko wajanja.
Pilipili usizokula zakuwashia nini?
 
Akiondoka Mbowe, Chama kitakuwa kama CUF, serikali ya CCM imejaribu sana ikiwemo kumbambika kesi ya ugaidi imeshindwa, njia rahisi ni kuwachochea wanachama Wadai uenyekiti.
Umeona eh wanatafuta kila namna lakini CHADEMA NI IMARA.Walianzia kuengua majina ya wagombea uenyekiti 2019 wote wa Chadema kwa sababu mbalimbali,wakaja uchaguzi mkuu 2020,Wakapora wanawake 19 na kuwapa Viti maalum Ubunge,Wakamfunga Mbowe kwa kesi ya ugaidi pamoja na kuzuia mikutano ya vyama vya siasa.Mipango yote hiyo walishindwa kufanikiwa sasa wanachochea moto kwa Wanachadema ili Mbowe aondolewe Uenyekiti wa CHADEMA ili wakipasue chama lakini napo wameshindwa.Ngoja tuendelee kushuhudia tu kwa macho Kama Magufuri na ubabe wake wote alikufa akashindwa kuiua chadema basi tutaona mengi .
 
Samahani, nje ya mada kidogo, kwani chadema bado kipo?!!!!
 
Akiwa kwenye mjadala wasafi fm, John Heche amekanusha uvumi aliolizwa na mwandishi kuhusu kuwepo kambi mbili ndani ya Chadema huku yeye Heche akiwa kambi ya Tundu Lissu.

Heche amesema mara ya kwanza kuingia kikao cha kamati kuu ilikuwa 2011 na alikuta mjadala wa fedha unajadili, Heche anasema jinsi watu walivyokuwa wanavuta alijua ndio siku ya chama kupasuka ambapo Dk. Slaa alibananishwa na kina Mabere Marando na prof. Baregu.

Heche amesema hawawezi kuwa na uongozi ambao hauwezi kuhojiwa.

Kuhusu Mbowe kuwa mwenyekiti muda mrefu(miaka 19), amesema ni jambo zuri akiachia mtu mwingine lakini wanaoongea hivyo wachukue fomu, hawawezi kumuondoa mwenyekiti na chama kibaki bila mwenyekiti.
Awamu ya 5 iliwaaminisha kuwa chadema imekufa,sasa mataga yamekuja kivingine
 
Kwa chama kinachotumia maharamia kuzima Legacy ya Nyerere, sidhani kama wana uhalali wa kumtaja taja kuhalalisha uwepo wa Mbowe madarakani, yaani hayo ni matusi kwa Baba wa Taifa.

Nyerere aliongoza Nchi.

Mbowe anaongoza Chama tu!

CHADEMA, kumbeza Nyerere kwa kuua siasa zake wako maradufu sana halafu wanageuka na kumuenzi kutafuta kutumia nguvu yake kwa manufaa ya kibinafsi, hio sio sawa.

Nyerere alikuwa Mungu nini?
 
Hawa viongozi wa siasa wamekuwa wakifikiri kwamba bado kuna watz ambao ni mazuzu wa kuendelea kuwadanganya na kuwahadaa kama miaka ile.

Mwaka 2015, wakati mh Lowassa alipokatwa makusudi na CCM tetesi zilianza kuvuma kuwa mheshimiwa huyo anajiandaa kukimbilia katika chama kimoja wapo cha upinzani kati ya ACT Wazalendo au Chadema.

Ghafla viongozi wa Chadema hivi hivi mfano wa Heche wakajitokeza na kuanza kupinga kwa kuwatoa hofu wanachama wao kuwa Chama hicho hakiwezi kufanya kosa hilo la karne la kumkaribisha fisadi Lowassa ndani ya chama chao, na kwamba kama akihamia upinzani basi ataenda ACT Wazalendo ambacho ni chama alichokianzisha mwenyewe ili akikatwa akimbilie huko.

Muda ni mwl mzuri, baada ya muda mheshimiwa akamwaga mkwanja kupitia mlango wa uwani wa mwenyekiti na genge lake.

After that kila mtu anakumbuka kilichotokea na wale wote waliopinga tetesi hawakujitokeza kukanusha tena walichokipinga 🤣🤣🤣🤣

Siasa za Tanzania bila unafiki kwa kweli haziendi maana wajinga na wadanganyika ni wengi mno kuliko wajanja.
Huu wimbo wa ccm kwamba lowasa alitoa pesaili kuingia Chadema mbona umeshafubaa? Alitoa sh. ngapi? Nani alipokea? Je! alipotoka Chadema kwenda ccm alilipa sh. ngapi?
Kuhusu uenyekiti wa Chadema:- Inakuwaje wanachadema hawana tatizo na m/kiti wao, ila ccm ndio wenye shida? Ccm badala ya kuhangaika na umasikini wa taifa hili, wanahangaika na uenyekiti wa Chadema. Kachukueni basi form mgombee.
Mbowe ataendelea kuwa mwenyekiti wa Chadema hatamiaka 100. Mliharibu bustani yake, mkavunja bilicanas, mkamsingizia ugaidi yote yameshindikana. Mwenyewe anasema hata mkavunja ile nyumba anayoishi; no surrender no retreat.
 
Nyerere alikuwa Mungu nini?
Hayo ni yako. Awe asiwe mbona mnamtumia as a source of authority mnapotaka kusema kitu?
Halafu mnazodoa na kukandamiza filosofia zake nyakati zingine zote?
 
Heche anajua bila ya Mbowe kuendelea kuwa Chairman basi maridhiano yatakufa kifo cha Mende

Maridhiano yakifa basi na yale Majimbo maalum ya maridhiano ikiweno kwa Heche na Sugu pia yatapotea

Mbowe kuendelea kuwa Chairman hadi 2025 itasaidia yeye Mbunge
 
Kama unautaka uenyeakiti wa CHADEMA, ukifika wakati wa uchaguzi, nenda ukajaze fomu.
Kwani Lema hafai?
Lakini ufahamu uongozi kwenye vyama vya upinzani ni tiketi ya kwenda jela wakati wowote, kubambikiwa kesi, kufilisiwa, na wakati mwingine hata kuuawa.
Si mungu yupo? au
Afadhali CHADEMA huwa wana uchaguzi wa kumchagua mwenyekiti, kuliko CCM ambako wanachama wamenyimwa haki ya kumchagua mwenyekiti, eti aliyetangazwa na tume kuwa Rais, ndiye automatically ni mwenyekiti wa CCM..
Tofauti imekuwa CCM wamesha badilisha angalau Wenyeviti watatu Mbowe bado yupo....ati Demokrasia!
Tena tunajua Vyama hivi vyote vina Katiba zao...angalau ya CCM inafuatiliwa na Inaheshimiwa, yaani inaonyesha Demokrasia, lakini CHADEMA mwenyekiti ni maisha! Halafu ndio muachiwe Dola na kufanya maamuzi ya Katiba ya Jamhuri....mkituwekea kipengele chenu kinachomruhusu Mbowe awe Dikteta je?
 
Honestly huwa sielewi unaongeaga utoto gani. Inaonekana ww ni wale mliochelewa kujua kusoma na kuandika.
 
Chadema ni mbowe na mbowe ni Chadema mtalia Lia sana ma CCM mpaka mkome.
 
Back
Top Bottom