Pre GE2025 Heche: Huyu mama hawezi kushinda uchaguzi Lissu akiwa mgombea na sisi tukiongoza chama sababu ni mwanamke, Mzanzibar na hana hoja

Pre GE2025 Heche: Huyu mama hawezi kushinda uchaguzi Lissu akiwa mgombea na sisi tukiongoza chama sababu ni mwanamke, Mzanzibar na hana hoja

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Kuna kitu umekiongea vibaya kwenye hoja yako.
Heche kama ni Heche kweli anaongelea strengths na weaknesses za Samia.

Nani asiyejua kwa Tanzania ya leo mgombea mwanamke ana nafasi Ndogo kushinda kuliko mwanaume kama mambo mengine yote wanafanana?

Hivyo hivyo Samia kuwa Mzanzibar ni weakness kwenye uraias wa Tanzania. Ni sawa na mtu aseme Mbowe kuwa mchaga ni tatizo kwenye Urais.

Misogyny ni kitu tofauti kabisa. Hedge anaongelea facts zilizopo na hata wewe Unajua.
Ubaguzi unaweza kukusaidia kushinda ila bado ni UBAGUZI TU
 
Tulipaswa kuambiwa na hasa kuambiwa kuwa huo wasifu unamfanya asiwa na sifa ya kuchaguliwa?

..anaweza asichaguliwe na watu wanaoamini katika mfumo dume, au wanaoamini Raisi wa muungano anapaswa kuwa Mtanganyika kwasababuWazanzibari wana Raisi na serikali yao.

..pia anaweza kuchaguliwa na wale wanaoamini wanawake nao wanastahili kuongoza sawa na wanaume, au wanaoamini Tanzania ni nchi moja hivyo haijalishi Raisi wa muungano anatoka Tanganyika, au Zanzibar.
 
Huyu aliyeanzisha huu uzi hata hajui nini ni fact na kitu gani ni ubaguzi.

Kweli kusema mgombea Mzanzibari ni tatizo unahitaji hata degree kujua hilo?

Hata unaweza kusema mgombea kutoka kabila kubwa kama wahaya ni tatizo. Hiyo ni fact sio ubaguzi.

Watanganyika wapo wengi na wengi wangetaka Rais wa Jamhuri awe Mtanganyika. Hiyo ni fact. Mtu kusema hayo hata si ubaguzi.
 
..anaweza asichaguliwe na watu wanaoamini katika mfumo dume, au wanaoamini Raisi wa muungano anapaswa kuwa Mtanganyika kwasababuWazanzibari wana Raisi na serikali yao.

..pia anaweza kuchaguliwa na wale wanaoamini wanawake nao wanastahili kuongoza sawa na wanaume, au wanaoamini Tanzania ni nchi moja hivyo haijalishi Raisi wa muungano anatoka Tanganyika, au Zanzibar.
Kwa hii katiba ilivyo rais atatoka CCM tu haijalishi ni nani hata kama litasimamishwa Jiwe kugonbea dhidi ya binadamu wa upinzani na huo ndo ukweli mchungu.....Heche na Lissu wamekutana pipa na mfuniko....siasa wanazoenda nazo hazitowafikisha popote kutokana na aina ya watu watakaowaongoza....hawahawa wanaomkimbia Mbowe kwny maandamano ndo hao hao watakaowakimbia wao wakiitisha maandamano.....na anaposema Mama hatoshinda wao wakiwa viongozi wa Chama watatumia mbinu gani hasa....wakisusa uchaguzi vyama vingine vitashiriki...wakishiriki kwa Katiba hiihii bdo watakula za uso hata kwa kuibiwa.....
 
Ubaguzi unaweza kukusaidia kushinda ila bado ni UBAGUZI TU
Kwahiyo hapo ni ubaguzi wa Watanganyika wote na sio Heche pekee.

Shida umechanganya facts na ubaguzi. Je nikisema mtu kutoka kabila langu ni rahisi kumshinda urais kwasababu anatoka kabila kubwa nitakuwa mbaguzi?

Hata wagombea kutoka mataifa makubwa Kama Wanyakyusa, wahaya na wachaga ni weakness kwenye kugombea urais.
 
Kwa hii katiba ilivyo rais atatoka CCM tu haijalishi ni nani hata kama litasimamishwa Jiwe kugonbea dhidi ya binadamu wa upinzani na huo ndo ukweli mchungu.....Heche na Lissu wamekutana pipa na mfuniko....siasa wanazoenda nazo hazitowafikisha popote kutokana na aina ya watu watakaowaongoza....hawahawa wanaomkimbia Mbowe kwny maandamano ndo hao hao watakaowakimbia wao wakiitisha maandamano.....na anaposema Mama hatoshinda wao wakiwa viongozi wa Chama watatumia mbinu gani hasa....wakisusa uchaguzi vyama vingine vitashiriki...wakishiriki kwa Katiba hiihii bdo watakula za uso hata kwa kuibiwa.....

..kauli sahihi ni kwamba kwa Katiba hii iliyopo Mama atashinda kwa kuiba kura na kutumia mabavu ya vyombo vya dola.

..uchaguzi ukifanyika kwa kusimamiwa na Tume na mifumo iliyo huru Mama hawezi kushinda kutokana na sababu mbalimbali mojawapo ikiwa uwezo wake mdogo katika kujenga hoja.
 
Chukua Clips kumi za John Heche msikilize utagundua uwezo wake ni mdogo sana
Watu wenye uwezo mdogo hujificha kwa kutukana Viongozi na Serikali
Huwezi kumfananisha na kizazi cha akina Ester Bulaya, Halima Mdee, Zitto Kabwe, Kafulila, John Mnyika wakijenga hoja bungeni
Heche ni mtupu sana
Labda waliosoma nae waje watupe ufafanunuzi zaidi
Heche huishia kutoa / ku-address challenges bila kuja na Solutions/ Way forward!!
mkuu mimi sifuatilii siasi but the guy is very smart upstairs.!!
prove me wrong, leta clip yoyote anayoaddress public tusikilize kama anahubiri ushubwada au la ukitoa iyo clip ya umbeya isiofuata privacy za watu katika mawasiliano

zipi ni hoja za samia, 4R au? na nani alimpigia kura kuwa Rais wa Jamhuri?
 
Sijui ndo maana sijawa kiongozi Mimi.....Yaani Mimi mtu anitukane na kunibagua hv na uwezo ninao😬😬😬😬😬 Dah!!!
Pole, ndugu. Ndiyo maana hujawa. Hata pesa ombea zisikutembelee. Ungeua maelfu. Halafu kizazi chako kirithi damu isiyo na hatia. Yeye kasema maneno tu, ila wewe ungeutumia Urais kumfanyia lolote.
 
Pole, ndugu. Ndiyo maana hujawa. Hata pesa ombea zisikutembelee. Ungeua maelfu. Halafu kizazi chako kirithi damu isiyo na hatia. Yeye kasema maneno tu, ila wewe ungeutumia Urais kumfanyia lolote.
Kabisa, mi sina simile na mijitu mipumbavu iliyojaa chuki. Ni hatari zaidi kwenye jamii hiyo........miji inaweza kuwaka moto na kubadilika kabisa mkiwaentertain watu kama hao.
 
Kabisa, mi sina simile na mijitu mipumbavu iliyojaa chuki. Ni hatari zaidi kwenye jamii hiyo........miji inaweza kuwaka moto na kubadilika kabisa mkiwaentertain watu kama hao.
But my study inanionyesha kila tabia ikizidi ni ugonjwa unaotaka tiba. Ukali kama wako ni ugonjwa, upole kama wangu ni ugonjwa. Uchawa wa kusifu watu kama MUNGU ni ugonjwa, kufurahia, mateso ya watu wengine ni ugonjwa nk nk. Ila kuna ugonjwa nafuu kidogo kuliko lakini sio ugonjwa wa ukatili kwa binadamu wengine.
 
Anachokifanya Heche sio kizuri hata kidogo. Wenje alisema bajeti ya uchaguzi milioni 700, CDM walikuwa na 300m na Mbowe 250. Akasema wajumbe wa Kamati Kuu walitakiwa kuchanga ili kufanikisha uchaguzi. Lissu aliambiwa achangie 30 milioni na mpaka siku anaongea Wenje alikuwa hajachanga kitu. Heche hajasema amechangia kiasi gani.

Sasa badala ya kumshukuru mtu anaewezesha wajumbe wengi ( ambao wanatuambia kuwa 90% wameahidi kuwapigia kura) kuhudhuria yeye anamlaumu halafu anatoa shutuma kuwa kahongwa mabilioni ya shilingi ili Chadema ife na Samia ashinde . Hiyo njaa Mbowe ameipata baada ya Lissu kutangaza kugombea urais?

Mbowe ni mfanya biashara kwa nini awekeze pesa nyingi katika uchaguzi ambao kila mmoja alijua CCM wameamua kuwa watashinda kwa njia yeyote ile? Si bora kuwekeza katika uchaguzi wao wa ndani utakaotoa fursa kwa CDM kupata viongozi bora? Haka kama atachaguliwa Lissu. Kama Lissu na Heche ni wapiganaji kweli kwa nini hawakuhakikisha kuwa wagombea wao wanatangazwa katika majimbo yao. Halafu wanataka kutuaminisha kuwa watahakikisha kuwa wanatangazwa wakati wanashindana na Amiri Jeshi Mkuu.

Hecha anasema hadharani kuwa kwa jinsi anavyomheshimu Mbowe hawezi kumsema vibaya kumbe anamchimba nyuma ya pazia. Sio mtu mzuri.

Amandla...
 
Kwa washika ngumi ni hoja walioisikia kwa wakijani kwa muda mrefu..umekuwa mwangwi sasa unawatesa.
 
But my study inanionyesha kila tabia ikizidi ni ugonjwa unaotaka tiba. Ukali kama wako ni ugonjwa, upole kama wangu ni ugonjwa. Uchawa wa kusifu watu kama MUNGU ni ugonjwa, kufurahia, mateso ya watu wengine ni ugonjwa nk nk. Ila kuna ugonjwa nafuu kidogo kuliko lakini sio ugonjwa wa ukatili kwa binadamu wengine.
Kwahiyo unaona huu ugonjwa wa heche mdogo?!! Wa kuvumilia?!!!
 
Back
Top Bottom