Kwa ukatili kama huu na mauaji ambayo mmefanya kwa Watanzania leo mnasema mtaongoza?
Mnataka kumuongoza Nani? Mnazungumza eti maendeleo ya nini? Kwaajili ya nani kama mmeua watanzania na kuwatesa hivi?
Maji, umeme, Barabara au kitu chochote bila binadamu kuwepo vina maana gani?
Hili jeshi la polisi wanafundishwa nini huko kwenye vyuo vyao? Kuwa katili? Said Mwema kwenye kitabu chake aliandika kuhusu huu ukatili, Tume ya haki jinai ya Samia imeandika kwamba hili jeshi linapaswa kufumuliwa kwasababu lina element za kikoloni, baada ya haya nani tena anaweza kuwa na imani na jeshi hili? Nani anaweza kubisha.
Lazima tutabadili namna ya utendaji wa jeshi la polisi.
Madaraka ya damu hayatasimama kwenye Nchi yetu.