Heche Ni Muongo. Mafuta Yamepanda Dunia Nzima. Hayajapandishwa na Serikali wala wafanyabiashara

Heche Ni Muongo. Mafuta Yamepanda Dunia Nzima. Hayajapandishwa na Serikali wala wafanyabiashara

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2022
Posts
40,476
Reaction score
26,173
Ndugu zangu Watanzania,

John Heche Amedhihirisha ni kwanini CHADEMA imekosa Muelekeo kipindi hiki cha uongozi wake, Amethibitisha ni kwanini CHADEMA imepuuzwa na yeye kudharauliwa hadi na wale anaowaongoza, imedhihirika ni kwanini wenye akili Timamu walikataa kuongozwa naye na kuamua kuondoka ndani ya CHADEMA.

Imedhihirika ni kwanini CHADEMA imepoteza mvuto ,kukosa uungwaji mkono na kukimbiwa na vijana na wote wenye akili Timamu na wanaojitambua vyema. Imejidhihirisha ni kwanini hakuna mwenye akili Timamu anayejitokeza hadharani na kuiunga mkono CHADEMA.

Huwezi kuwa na kiongozi aina ya John Heche kipofu, mwenye upeo mdogo ,aliyekosa maarifa na uelewa wa masuala nyeti na muhimu akawa kiongozi halafu utegemee chama kupata mafanikio na kuwa na Dira na muelekeo unaoeleweka. John Heche hakuwa na hana uwezo wala sifa za kuwa kiongozi kuongoza Watu wenye kujitambua. Ni vile tu CHADEMA imekosa watu wenye akili za kiuongozi na kuweza kuongoza na ndio maana akajikuta anapata nafasi ya kuongoza kundi la wenye upeo mdogo, wasio na maarifa wala upeo wala uelewa zaidi ya Uropokaji,ukurupukaji na mihemko tu utafikiri wavuta Bangi ama walevi wa gongo.

Ndugu zangu Watanzania suala la mafuta ni suala la Dunia,ni suala ambalo limeathiri muenendo wa Bei Dunia nzima na katika soko la Dunia. Ni suala ambalo limegusa Mboni za wakubwa wote . Ni suala ambalo hata asiye na akili anajua kuwa nini kimesababisha kupanda kwa nishati hiyo muhimu.

Siyo serikali yetu ya CCM ama chama chetu cha Mapinduzi Tumaini la watanzania kilichopandisha bei. Wala hakuna mfanyabiashara yeyote yule alipanga bei na kuipandisha kwa ajili ya kujipatia Faida ama kuumiza watanzania. Serikali yetu ipo makini na ipo karibu katika kufuatilia jambo hili. Kwa sababu mafuta ndio injini ya Uchumi na Kichocheo cha kila sekta . Ndio kichocheo cha ustahimilivu wa bei za bidhaa nyingi sana. Ni Bidhaa inayogusa kila kitu ambapo inao uwezo wa kuathiri uchumi wa Nchi na bei ya kila bidhaa.

Ndio sababu serikali yetu chini ya uongozi shupavu,makini na madhubuti wa Jemedari wetu kipenzi Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan imekuwa makini sana kusimamia bei zake na kutoa maelekezo na Bei elekezi. Hakuna mwanya wa mtu yeyote yule anayeweza kuhujumu bei za mafuta na kupandishaa bei kwa maslahi yake Binafsi.

Suala la mafuta ni sehemu ya usalama wetu wa Taifa. Bila mafuta hakuna usalama ndani ya Taifa. Kwa sababu Kila kitu kitavurugika.

Hivyo mtu kama Heche anapotokea zake huko na mavitu yake kichwani aliyobugia anakuja na kuanza kuropoka bila ushahidi ni lazima watanzania tuwe wakali na tumkemee sana kwa sababu ni adui wa Taifa letu na mwenye lengo la kuleta uchochezi,mtafaruku ,na uchonganishi. Inaonyesha ni mtu asiye na taarifa ama umbumbumbu umemjaa kichwani ama amekwenda kuongea akiwa kavurugwa akili ama kwa matumizi ya vileo vikali.

Watanzania endeleeni Kumpuuza Heche na msimsikilize kabisa ujinga wake huo usio na mashiko wala ukweli wa aina yoyote ile. Vyombo vya dola vichukue hatua kali dhidi yake ya kumkamata na kumhoji ili athibitishe uongo na uzushi wake huo.

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.

Pia soma: Heche: Ma-cartel wamejimilikisha uchumi wa nchi yetu, kampuni moja ina ubia na watu walioko serikalini ilipewa tenda kuagiza mafuta na kusimamia bei
 
Ushauri wa bure,

Endelea kububujwikwa na machozi ya furaha kwa Samia kupungia wananchi mkono au Bashite kuvaa jeans iliyomtoa shepu.

Huna upeo hata chembe wa kuweza kumjadili Heche. He is beyond you.
 
Ushauri wa bure,

Endelea kububujwikwa na machozi ya furaha kwa Samia kupungia wananchi mkono au Bashite kuvaa jeans iliyomtoa shepu.

Huna upeo hata chembe wa kuweza kumjadili Heche. He is beyond you.
Huyo Lukas namwitaga K.enge asiye na akili. Jamii Forums imefungiwa, anaingia kwa VPN kuja kuwasifia na kuwatetea walioifungia isipatikane Tanzania, huyo ni binadamu wa kawaida!?,halafu anasema Heche ana upeo mdogo, anasahau yeye hana upeo wowote, hata walipouawa ndugu zake Mbeya October mwaka jana alikuja hapa kupongeza.
 
Kwa tunavyokufahamu, jinsi kiwango cha akili yako inapoishia, ulichoandika hakishangazi. Tunakufahamu wewe ni mgonjwa wa akili na nafsi. Uwezo wako wa akili ni mdogo sana, haufikii hata 1% ya uwezo wa akili ya Heche. Heche hapigi riwaya za kiwendawazimu kama hizi za kwako. Yeye alikuja na data za kuonesha mafuta yamepanda kwa asilimia ngapi kwenye soko la Dunia, na nchini yamepandishwa kwa asilimia ngapi. Hakubwabaja kama wewe punguani. Pole sana kwa kukosa maana katika jamii.
 
Tangia lini Heche akawa na akili kichwani zaidi ya Uropokaji na ukurupukaji.
 
Hata Corona ilikuwepo dunia nzima lakini bidhaa hazikupanda Tanzania
Ondoa ujinga wako hapa wewe .Kwani Mafuta ni Corona? Kwamba hukuona Athari za Corona kiuchumi ? Au kwa sababu unarishwa kama kinda la ndege.
 
Huyo Lukas namwitaga K.enge asiye na akili. Jamii Forums imefungiwa, anaingia kwa VPN kuja kuwasifia na kuwatetea walioifungia isipatikane Tanzania, huyo ni binadamu wa kawaida!?,halafu anasema Heche ana upeo mdogo, anasahau yeye hana upeo wowote, hata walipouawa ndugu zake Mbeya October mwaka jana alikuja hapa kupongeza.
Acheni uzushi , uongo na uchonganishi hapa. Watanzania siyo wajinga kama mlivyo ninyi.
 
Back
Top Bottom