Heche: Pressure iongezeke kuwafanya viongozi walio madarakani kufanya mabadiliko

Heche: Pressure iongezeke kuwafanya viongozi walio madarakani kufanya mabadiliko

Parabolic

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2013
Posts
2,922
Reaction score
3,252

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Heche amesema kuna haja ya kuongeza msukumo kutoka kwa wananchi ili kuwafanya viongozi waliopo madarakani kutambua umuhimu wa kufanya mabadiliko ya Katiba.

Heche amesema chimbuko la baadhi ya matatizo yanayotokea nchini linahusishwa na changamoto za uchaguzi, akidai kuwa kuna watu wanaotaka kuendelea kubaki madarakani kwa njia ambazo siyo za kikatiba.

Heche ameyasema hayo Agosti 28, 2026, wakati akizungumza katika Jukwaa la Demokrasia Tanzania lililoandaliwa na Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS).

Amesema mabadiliko ya Katiba ni muhimu katika kushughulikia changamoto zinazohusiana na uchaguzi na uendeshaji wa demokrasia nchini.

Kwa mujibu wa Heche, wananchi wanapaswa kuongeza msukumo kwa viongozi ili suala la mabadiliko ya Katiba lipewe uzito unaostahili.
 
Back
Top Bottom