Heche usipotoshe; Wanaosema Polepole katekwa ndiyo wanaopaswa kuthibitisha Passport inaonyesha aliingia lini nchini

Ungetumia akili hata kidogo kuchangia badala ya kujitoa ufahamu na kuandika kitu ambacho huna uhakika nacho.
 
Jiandae tu kukimbia nchi fisadi
Kupotea Kwa polepole siyo jambo jema na salama. Lakini swali langu je? Mtu mhimu kama Polepole ambaye amewahi kuwa Katibu mwenezi chama tawala na mara ya mwisho akawa balozi wa kuliwakilisha Taifa na baadaye akaamua kuachia nyadhifa zote alizokuwa nazo na kuanza ukosoaji mkubwa kiasi mpaka Polisi kumuita aje wakae wazungumze. Akasema wamuhoji kwa njia ya mtandao ni vipi aje kwa njia za panya?

Hajulikani aliingia lini na vipi nchini na hakuripoti kwa mamlaka zilizo kuwa zina mhitaji? Je ni kweli alikuja? Kama alikuja kwa stahili hizo alikuwa na lengo gani? Kwa mtu mkubwa na maarufu na mwenye wafuasi wengi?
 
polepole mara nyingi amesema yuko nchini kama ana makosa apelekwe mahakamani
Karma is real and never loses location. Polepole ni mmoja kari ya top 5 members wa Magufuli walioasisi uchafu wote huu; kuteka, kuua, kuzuia shughuli za vyama vya upinzani, kununua wabunge wa upinzani, kunyang'anya fedha za wafanya-biashara. Kwa hiyo muache anywee kikombe alichokuwa anaywesha wengine kama kina Ben Saanane, Tundu Lissu etc
 
Hiyo siku mtajua hamjui. Msije mkavilaumu vyombo vya usalama.
 

Aina za watu kama imhotep ni liability. Hawana mchango wowote. Hawajitambui. Yeriko, retiree na ile timu yote tiifu ya mwamba ni heri ikaishia huko kwenye ubwabwa tu.

Haijui tunapigia nini na haiwezi kuelewa. Misaliti mikubwa. Hatuwezi kupigana na wa namna hiyo wakiwa huku!


Ni heri kuwa na mbuzi meme wenyewe kuliko hizi!
 
Kisa nini hasa? Umempa mtu kazi ya Ubalozi, huyo mtu akajiuzulu. Immediately baada ya kujiuzulu anaanza kuichafua Serikali. Bahati mbaya amekutwa na janga la kutekwa. Hivi kweli Serikali itakayofanya uchunguzi wa nani amemteka itakuwa na akili au matope??

Polepole deserves all that befell upon him. No sympathies
 
polepole mara nyingi amesema yuko nchini kama ana makosa apelekwe mahakamani
Kama alikuwa nchini kwanini hakuitikia wito wa Polisi?? Nayeye ni mtu alikuwa kiongozi mkubwa kwenye chama na Serikali? Hiyo ni collateral damage, kuweni wapole
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…