SI KWELI Heche: Vijana wizara mmepewa sasa ni kujipanga katika kukamatia fursa

SI KWELI Heche: Vijana wizara mmepewa sasa ni kujipanga katika kukamatia fursa

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Wakuu,

Ni kweli kauli hii imetolewa na makamu mwenyekiti wa CHADEMA bara John Heche?.

01.jpg
 
Tunachokijua
Madai

Kupitia mitandao ya kijamii ikiwemo Facebook kumekuwapo na grafiki yenye utambulisho wa Jambo TV huku ikiambatana na ujumbe unaodaiwa kuwa ni wa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Tanzania Bara, John Heche amesema.

"Vijana Wizara mmepewa sasa ni kujipanga katika kukamatia fursa"

Uhalisa wa Madai hayo

Taarifa hiyo inayosambazwa inarejelea hotuba aliyoitoa Heche kwa vyombo vya habari Novemba 19, 2025.

Ufuatiliaji wa JamiiCheck kupitia marejeo ya taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na John Heche Novemba 19, imebainika kuwa taarifa inayosambazwa si ya kweli.

Katika hotuba yake hiyo Heche hakuzungumzia chochote kuhusu uwepo wa wizara ya vijana na kuwataka vijana wachangamkie fursa hiyo.

Aidha taarifa hiyo haijachapishwa na Jambo TV kupitia kurasa zake rasmi za mitandao ya kijamii. Pia grafiki hizo ni za kughushi kwani zometumia aina tofauti ya mwandiko (fonts)
Kama sio.ya kweli.mnaacha ya nini?
Nyie mods na nyie wahaini Tu
 
Back
Top Bottom